Troll JF
JF-Expert Member
- Feb 6, 2015
- 7,804
- 12,233
NI dhahiri kwamba Rais John Pombe Magufuli amechukua hatua zinazomfanya ajizolee sifa za kila aina kutoka kwa wananchi wa Tanzania, pamoja na wachambuzi na wasemaji mbalimbali duniani kote.
Sifa hizo zimetokana na kwamba Magufuli ameonyesha ujasiri mkubwa katika kupambana
moja na moja na mambo mengi ya uovu yaliyokuwa yakifanywa na viongozi na watendaji wa serikali chini ya utawala uliokuwa madarakani huko nyuma.Tumeona baadhi ya hatua za Rais Magufuli na jinsi zilivyozaa matunda mema.
Mbali na hayo matunda yanayoweza kuonekana, pia hatua za Magufuli na wasaidizi wake wakuu, pia hatua zake zimeibua saikolojia mpya nchini kwa maana
kwamba wengi wa watu waliomo serikalini sasa wanaheshimu kazi zao na wanajali ajira na majukumu waliyokabidhiwa, ama na wananchi
ama na mkuu wa nchi.
Hali hii ni njema na inabidi kuwekwa bayana kwamba ni hali inayotuweka mbali kidogo na ile
hali tuliyokuwa nayo kwa muda mrefu sasa ya watu kutojali, kutothamini na kutoogopa wajibu
wao kwa nchi na kwa wananchi. Sasa hivi tunaweza kuwa na matumaini kwamba serikali
itakuwa ni mkusanyiko muruwa wa asasi zilizosimikwa ili kuwatumikia wananchi na wala si kuwatumikia mamangimeza na warasimu waliojijengea himaya binafsi ndani ya idara za serikali na asasi zake.
Ni kweli tulikuwa tumezoea ufisadi kama njia ya kuendesha shughuli za serikali katika ngazi zote. Kila aliyejikuta katika nafasi yoyote ile alitafuta njia zote zilizomuwezesha kuchota na kuchukua kila alichoweza na kutumia kila kilichopita karibu yake bila kujali kama ni halali yake au haramu.
Kulindana ilikuwa ndiyo dira inayoongoza utendaji serikalini: Nikune mgongoni, nami nitakukuna. Hata hivyo ni muhimu kutambua na kujikumbusha
daima kwamba hali hii haikuanza ghafla, na wala haitaweza kuondoka ghafla kwa sababu tu kaja rais anayeichukia.
Hatuna budi kujua kwamba
uovu huu umekuwa ukijengeka kwa miongo kadhaa na kwamba katika kujengeka kwake umeimarisha utamaduni wa kutojali. Alama za kutojali ni nyingi, na wala hatuna haki ya kuzifumbia macho. Ukweli ni kwamba tulikwisha kufikia mahali tukavumilia hata matendo ya jinai ya wazi katika serikali.
Kama tuliweza kuambiwa kwamba watumishi wetu waliketi wakagawana nyumba tulizowakabidhi, ni nini tulidhani wasingeweza kufanya? Mambo mengine yanaonekana hata na kipofu lakini sisi wenye macho tunajifanya kama vile hatuoni. Hakuna jambo lolote ovu linalotokana na hewa ipitayo; kila jambo ovu lina mwanzo, na
kama mwanzo haukuchunguzwa, kubainika na kudhibitiwa, jambo hilo litazidi kuimarika hadi
lifikie hatua kwamba halizuiliki tena, na litamdhuru yeyote atakayediriki kulikabili na
kulipiga vita.
Baadhi yetu tumekuwa wakati wote
tukitanabahisha jamii yetu dhidi ya kukubali kuvumilia aina yoyote ya ufisadi alimradi tu umefanywa na watu wenye mabavu na ambao
wanao uwezo wa kuwabamiza wale wanaowapinga. Baadhi yetu tumeumizwa katika jitihada hizo, na wale wezi na mafisadi tuliowapinga wamezidi kuzawadiwa kwa vyeo na mali. Leo wanachekelea, lakini mimi nasema
kwamba vyeo hivyo na mali hizo ni laana kwao, kwani ni damu za Watanzania walizonyonya na
siku moja zitawageukia na kuwasuta hapo zitakapoanza kutunga usaha.
Nasema ni damu za wananchi zilizonyonywa ili wachache waweza kujijengea ukwasi usioelezeka, na waweze kumiliki akaunti za mapesa zilizofichwa ughaibuni zinazotokana na fedha
zilizotakiwa zinunue dawa za akina mama wazazi, vichanga vyao na vizee wanaokufa kwa magonjwa yanayozuilika. Ni fedha hizo hizo
ambazo zimekwapuliwa na wale ambao bila shaka wanajiona ni wajanja sana –na sisi wengine ni mabwege – ambazo zingeweza
kusomesha watoto wa nchi hii, kuweka maji katika kila kaya, na kujenga jamii yenye afya, furaha na staha.
Rai yangu ni kwamba kwa mtu yeyote anayetumia hata muda kidogo kuwaza, haiyumkiniki kwamba ili kuondoa uozo wote huu tunachohitaji ni amri za mkuu wa nchi na wasaidizi wake wachache
wanaorukaruka kutoka tukio moja hadi jingine wakifuatiwa na kamera za televisheni.
Siamini hata kidogo kwamba hatua hizi zitaleta mabadiliko ya kudumu, tukiacha ukweli kwamba watu wengi wataonyesha utii wa hofu na
nidhamu ya woga, na hii itaendelea kwa muda mfupi tu, mpaka pale mafisadi wazoefu watakapopata mbinu mpya za kuwaficha wao na
matendo yao maovu. Ndiyo maana nasisitiza kwamba hakuna njia ya mkato ya kukabiliana na uozo uliogandana ndani ya mifumo yetu.
Nimemsikia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitangaza rasmi kuanzishwa kwa “mahakama ya
mafisadi.” Naelewa kwamba huo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Magufuli, lengo lake likiwa ni
kujaribu kuharakisha kesi dhidi ya watu wanaodhaniwa na kutuhumiwa kuwa “mafisadi”.
Sina budi kusema mwanzoni kabisa, kabla mahakama hii haijazinduliwa kwamba ninaipinga
hatua hii kwa sababu ni hatua yenye hatari kubwa kwa mustakabali wa nchi yetu. Mahakama kama hizi zinaweza kutumika kuwakomoa watu
wasio na hatia kwa sababu tu kuna mahali wamewaudhi wakuu wenye uwezo wa kuwaumiza. Kwa maana nyingine mahakama hii inaweza kugeuzwa kuwa “kangaroo court”
ambayo kazi yake itakuwa ni kutafuta wachawi na kuwapeleka “mchakamchaka” hadi jela bila
kujali umadhubuti wa mashitaka dhidi yao.
Tukianza na “mahakama ya mafisadi” ambayo ni mahakama ya makosa ya jinai, ni kwa nini tusianzishe mahakama nyingine kwa ajili ya makosa mengine ya jinai. Kwa mfano mahakama mahsusi kwa makosa ya ubakaji, unajisi, usafirishaji haramu wa binadamu, ugaidi, dawa za kulevya, na kadhalika? Utawala wetu leo unauona ufisadi kama ndilo kosa kubwa kuliko yote kiasi cha kutaka kuuundia mahakama. Sawa. Lakini miaka michache ijayo, mathalan, tukikuta kwamba tunakabiliwa na janga kubwa la ugaidi, tutaanzisha mahakama ya ugaidi? Na baadaye, nyingine ya mihadarati, na kadhalika? Napenda kueleweka kwamba haya niyaandikayo
si ya mwanasheria, bali ni mawazo ya mtu anayesoma na kutafakari historia, tangu tulikotoka hadi hapa tulipo, na pia kwa kuangalia historia za wenzetu ulimwenguni.
Tuliwahi kushangilia kuanzishwa kwa kosa la jinai la “Uhujumu Uchumi” ambalo baada ya muda mfupi tu, yakageuzwa kuwa mashitaka la kuwabambikizia wote tuliotaka kuwatesa, kwa sababu shitaka hilo halina mdhamana.
Sasa hivi, yako mashitaka mengine ambayo yanatumika waziwazi kuwakomoa wale tunaowaona kama “wasumbufu”, “wakorofi”,
“wabishi”. Madhara yake ni kwamba tukiisha kukubali kutumia mbinu chafu ili kuwakomoa wale
tunawaona kama wakorofi, na tuwe tayari sisi wenyewe kujikuta katika kizimba cha mshitakiwa na tukikabiliwa na tuhuma zile zile.
Kadri ninavyoziangalia shughuli za mahakama zetu ndivyo ninavyozidi kuamni kwamba mahakama zetu haziko kwa ajili ya kutenda haki
bali kwa ajili ya upande mmoja kushinda na upande mwingine kushindwa.
Mwendesha mashitaka hana hata chembe ya kutaka kutenda haki bali mtuhumiwa “wake” afungwe tu. Wakili wa utetezi hana nia ya kujua iwapo haki inatendeka bali mteja wake aachiwe. Huu si mfumo unaotafuta haki kwa ajili ya jamii;
ni mfumo wa mawakili na waajiri wao. Mwendesha mashitaka akishinda kesi nyingi anaonekana ndiye mweledi na atapandishwa
cheo. Wakili wa utetezi akishinda kesi nyingi kubwa, bei yake inapanda na anapata mashauri
mengine makubwa ya fedha nyingi. Hakuna haki hapa.
Katika mfumo huu na utamaduni wake, hata tungeanzisha mahakama maalumu kwa ajili ya
kila aina ya jinai, tutakuwa tunawatengenezea “ulaji” mawakili bila kufikia malengo ya kutenda
haki. Tutawafunga wezi-uchwara wasiojua kuiba sawasawa na wasiojua falsafa ya “kula na watu”,
lakini mafisadi wa kweli kweli.. hatumpati hata mmoja.
Nitaendelea na hoja hii wiki ijayo