Gen Z Madagascar wakataa wito wa Mazungumzo na Rais, Watishia Maandamano ya Kitaifa

Gen Z Madagascar wakataa wito wa Mazungumzo na Rais, Watishia Maandamano ya Kitaifa

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Waandamanaji nchini Madagascar wamekataa kushiriki mazungumzo yaliyotangazwa na Rais Andry Rajoelina Oktoba 8, 2025, wakimtuhumu kiongozi huyo na serikali yake kwa vitendo vya ukandamizaji.

Rais Rajoelina alikuwa ametoa wito wa kufanyika kwa “mazungumzo ya kitaifa” akiwashirikisha viongozi wa dini, wanafunzi, na wawakilishi wa vijana, ili kutafuta suluhisho la mzozo unaoendelea nchini humo.

Hata hivyo, kupitia ukurasa wao rasmi wa Facebook, waandamanaji walitoa tamko wakisema wanakataa kile walichokiita “mazungumzo ya maigizo.”

Badala yake, wameitisha mgomo wa taifa, kufuatia kumalizika kwa 'ultimatum ya saa 48' waliyompa rais bila hatua kuchukuliwa.

Chama cha madaktari wachanga nchini hum kimeunga mkono wito huo, kikilaani pia matumizi ya nguvu ya polisi wakati wa maandamano yao ya Jumanne.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyotolewa wiki iliyopita, watu wasiopungua 22 wamepoteza maisha na zaidi ya 100 kujeruhiwa tangu maandamano hayo yaanze

Vuguvugu hili linaloongozwa na kizazi cha Gen Z lilianza tarehe Septemba 25, 2025, likichochewa awali na hasira juu ya ukosefu wa maji na umeme, kabla ya kugeuka kuwa wimbi pana la kupinga umasikini uliokithiri na ufisadi serikalini

Licha ya rais kuchukua hatua za kisiasa ikiwemo kuvunjilia mbali baraza la mawaziri na kumteua waziri mkuu mpya kutoka jeshi hatua hizo zimeonekana kushindwa kutuliza hali, huku waandamanaji wakiendelea kufurika mitaani wakimtaka Rajoelina ajiuzulu



Source: African news
 
Back
Top Bottom