Geita, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu atembelea Kambi ya wagonjwa wa Kipindupindu

Peter Dafi

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
389
272
WAZIRI UMMY MWALIMU AZURU GEITA KUKAGUA HALI YA KIPINDUPINDU

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu ametembelea kambi ya wagonjwa wa Kipindupindu ya Nyankumbu, Wilayani Geita leo tar 4 Jan 2015.
Pamoja na kukagua kambi hiyo, mh Ummy Mwalimu amezitaka Halmashauri ya Mji wa Geita na Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuhakikisha wanathibiti maambukizi mapya ya ugonjwa wa Kipindupindu.
Pia amewaagiza kuongeza jitihada katika kuelimisha wananchi juu ya ugonjwa huu wa mlipuko unaohatarisha maisha ya wananchi na kupoteza nguvukazi ya taifa.
Aidha, mh. Ummy Mwalimu amewaasa Wananchi wa Mkoa wa Geita kufuata kanuni za usafi wa mazingira ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu.


Habari zaidi check www.peterdafi.blogspot.com
 

Attachments

  • 1451928112370.jpg
    1451928112370.jpg
    55.8 KB · Views: 23
  • 1451928269893.jpg
    1451928269893.jpg
    50 KB · Views: 21
  • 1451928298561.jpg
    1451928298561.jpg
    72.7 KB · Views: 42
  • 1451928314581.jpg
    1451928314581.jpg
    80.7 KB · Views: 37
  • 1451928386400.jpg
    1451928386400.jpg
    58.3 KB · Views: 21
Back
Top Bottom