Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Watoto wawili wamejeruhiwa kwa bomu la kutupa kwa mkono katika Msitu wa Kanyala wilayani hapa walipokwenda kutafuta kuni
Wiki iliyopita msitu huo uliopo wilayani hapa ulitumiwa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kufanya mazoezi
Mtoto Frank Salim (14) aliyeumia miguuni alisema alijeruhiwa alipokuwa na mwenzake Yohana Alex (18) ambaye amejuruhiwa tumboni
Alisema Alex aliokota bomu hilo na alitaka kuligonga kwenye jiwe lakini wakati akimuonya lililipuka na kuwajeruhi
Akizungumza kwa taabu akiwa chumba cha wagonjwa mahututi, Alex alisema alipokiona kipande cha chuma alifikiri ni almasi
Akizungumza jana Alhamisi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema kuwa tukio hilo lililotokea juzi jioni. Alisema chuma cha bomu hilo kilimjeruhi mtoto mmoja na kuingia tumboni na hali yake ni mbaya
Mwabulambo alisema kabla ya tukio hilo, Jeshi la Wananchi lilitangaza kufanya mazoezi katika msitu huo. Hata hivyo, alisema Polisi wamewasiliana nao ili kuondoa mabaki ya mabomu yanayoinekana msituni
Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu aliwatembelea watoto hao waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Geita aliiomba Serikali kubeba jukumu la matibabu
Alisema msitu huo unatumiwa na wananchi kuokota kuni na kuchunga mifugo, hivyo iwapo ukaguzi hautafanyika haraka kuna uwezekano wa kutokea madhara makubwa
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita, Brian Mawala alisema aliwapokea watoto hao saa kumi na moja jioni
Alisema Alex amefanyiwa upasuaji baada ya kubainika bandama lilipasuka na hali yake inaendelea vizuri
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi alisema Kikosi cha Jeshi Namba 663 Mkoani Mwanza kiliomba kutumia msitu huo kulenga shabaha ikiwa ni sehemu ya mazoezi kwa wanafunzi
Alisema eneo hilo ambalo lipo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) haliruhusiwi wananchi kuingia bila kibali.
Chanzo: Mwananchi