GEITA: Wanawake wawili wauawa kwa kukatwa katwa na mapanga

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Wanawake wawili akiwemo mhudumu wa afya wa zahanati ya Kagu iliyopo kijiji cha Kagu Elizabeth Misango [54] na wa pili Helena Paulo [56] mkazi wa kijiji cha Luhuha mkoani Geita wameuawa kwa kukatwa katwa kwa mapanga ikiwemo kuchinjwa shingoni katika matukio mawili na maeneo tofauti usiku wa April 21.

Matukio hayo yamedaiwa kutokea katika mazingira yanayohusishwa na imani za kishirikina na tayari watu wawili wanaisaidia polisi katika upelelezi wa matukio hayo ambayo yameibua simanzi kubwa katika vijiji yalikotokea na viunga vya mji wa Geita.

Katika tukio la kwanza watu watatu wasiojulikana wakiwa na pikipiki walifika nyumbani kwa Elizabeth Misango karibu
saa mbili usiku katika kijiji cha Kagu na kumuamsha wa kudai wana mgonjwa lakini alipotoka nje na kujitambulisha walianza kumshambulia kwa kumkata kata kwa mapanga na kumchinja shingoni na alifariki palepale na wao kutoweka.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli Rodson amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kufafanua kuhusu mauaji ya Elizabeth Misango.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Hospitali teule ya rufaa ya mkoa wa Geita Dkt Adam Sijaona amezumgumzia kifo cha mhudumu wa Afya Elizabeth Misango.

Katika tukio la pili Helena Paulo [56] akiwa njiani na mumewe Joseph Lubaga saa tatu na dakika 45 usiku katika kijiji cha Luhuha wakirejea nyumbani ghafla walivamiwa na watu wawili mmoja akiwa na panga na kuanza kumkatakata marehemu ambaye alifariki muda mfupi baadaye akiwa hospitalini akipatiwa matibabu.

Kamanda Mponjoli ameiomba jamii kubadilika na kuachana na imani potofu za kishirikina ambazo ndizo zimekuwa chanzo cha mauaji hayo ya kikatili.

Kwa upande wao Diwani Kulubone Pancrasi na Afisa mtendaji wa kata ya Kagu David Makanza wameapa kusaidiana na vyombo vya dola kuhakikisha waliohusika na mauaji hayo wanapatikana.
 
Haya matukio ya kuua kwa kukatakata mapanga yanaendekezwa sana huko geita.Nikikumbuka tukio la Mawazo(R.I.P) na jinsi polisi ilivyolipuuzia naona kabisa yana connection na watu wazito.
 
Maonyo yawe "two way traffic" wawaonye pia washirikina waache ushirikina, maana imeandikwa "USIMUACHE MWANAMKE MCHAWI KUISHI" inaweza kuwaletea msukosuko.

Usikute watu wanatekeleza imani zao kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa tanzania toleo la 1977.

Poleni wafiwa Mungu awape roho ya uvumilivu hasa kipindi hiki kigumu.
 
Back
Top Bottom