marveljt
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 1,503
- 1,479
Watu 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi Geita waokolewa wakiwa hai.
Kwa mujibu wa habari watu hao wamepelekwa hospitali ili kupatiwa matibabu zaidi.
Ikumbukwe kuwa watu hao walifukiwa na kifusi hicho wakati wakiwa kazini katika moja ya migodi iliyoko chini ya wachina.
Chanzo: radio one/ itv
Tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano ya wiki hii ambapo jitihada za kuwaokoa zilikuwa zikifanyika kwa takriban siku 4 mfululizo hadi siku ya jana ambapo waokoaji walifanikiwa kucharanga mwamba na kupata upenyo uliowezesha mawasiliano kati ya waokoaji, na watu hao.
Zoezi limekamilika leo majira ya saa 5:02 asubuhi na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.
Zoezi hilo limeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani pamoja na Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali Ezekiel Kyuga.
Mara baada ya zoezi hilo kukamilika, watu pamoja na wanahabari waliokuwepo katika eneo hilo walionekana kulipuka kwa shangwe na kuwapokea wachimbaji hao ambao kati yao walikuwemo wenye uwezo wa kuongea ambao walisimulia tukio lilivyokuwa pamoja na kusema kuwa walikuwa wamajawa na hofu wakiamini kuwa wasahaulika.
Awali kabla ya kuokolewa, yalifanyika mawasiliano ya kuwatumia ujumbe kwa kutumia waya ili waseme wako wangapi na majina yao, ambapo walisema kuwa wako 15 na kwamba walikuwa na njaa na walihitaji maji, soda, uji n.k
Watu hao akiwemo raia wa China wamepatiwa huduma ya kwanza na kisha kupelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi.