PreGE2025 Geita: Erick Shigongo atoa msaada wa vifaa vya michezo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,755
Reaction score
2,861
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, ametoa msaada wa vitendea kazi vya michezo kwa wanamichezo wa Jimbo la Buchosa. Hafla hiyo ilifanyika katika kata ya Bupandwa, ambapo Shigongo alikabidhi mipira kwa ajili ya wanamichezo wa kata hiyo.

Shigongo alikuwapo kupitia diwani wa kata ya Bupandwa, Masumbuko Bupamba, na alisisitiza umuhimu wa wanamichezo kuendeleza vipaji vyao. Aliahidi kuwa atakuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanamichezo hao wanapata fursa ya kufikia malengo yao.

Aidha, alitumia fursa hiyo kuwataka wanamichezo hao kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya katika kutumikia wananchi wa Tanzania.
Your browser is not able to display this video.

Soma Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025​

 
Aisee!! mwaka wa uchaguzi ndo anatoa vifaa vya michezo miaka mingine holaaa🙄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…