Nipe Maji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 335
- 190
Halmashauri ya Wilaya ya Geita imetoa mikopo ya Shilingi Bilioni 1 na Milioni 156 kwa vikundi 111 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Mikopo hiyo imetolewa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali la kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia mikopo isiyo na riba.
Hafla ya kukabidhi mikopo hiyo imefanyika katika makao makuu ya Halmashauri hiyo yaliyopo Kata ya Nzera, na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Abala Komba.
Pia soma: Kuelekea Uchaguzi Mkuu: Utekelezaji wa ahadi, Uzinduzi wa Miradi na utatuzi wa ghafla wa kero za wananchi
Katika hotuba yake, Mkuu wa Wilaya ameishukuru Serikali kwa jitihada zake za kuwaepusha wananchi dhidi ya mikopo umiza yenye masharti magumu na riba kubwa.
Aidha, amesisitiza kuwa vikundi vilivyopokea mikopo vitumie fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili ziweze kuleta tija na mafanikio ya kiuchumi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Karia Rajab Magaro, amewataka wanufaika kusimamia kwa umakini dhamira zao na kufanya kazi kwa bidii ili waweze kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
Amekumbusha kuwa mikopo hiyo haina riba, hivyo ni fursa adhimu ya kuimarisha maisha yao.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jonas Kilave, akiwasilisha taarifa fupi ya utoaji wa mikopo hiyo, amebainisha kuwa jumla ya vikundi 155 viliomba mikopo, lakini baada ya mchakato wa uchambuzi, vikundi 111 pekee ndivyo vilivyokidhi vigezo na kuwa kati ya hivyo, 65 ni vya wanawake, 40 vya vijana na 6 vya watu wenye ulemavu.
Kwa upande wao, wanufaika wa mikopo hiyo wameishukuru Serikali kwa kuwapatia fursa hiyo na kuahidi kuzitumia fedha hizo kwa ufanisi, pamoja na kuhakikisha wanarejesha mikopo kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.
Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kuimarisha maendeleo ya jamii na kuinua hali ya kiuchumi ya wananchi hasa kutoka makundi maalum
DC