GB WhatsApp ni toleo lililobadilishwa (modded) la WhatsApp rasmi, linalotengenezwa na developers wasio rasmi. Kivutio chake kikubwa ni kwamba lina features ambazo WhatsApp ya kawaida haina, kama vile kusoma meseji bila kuonyesha blue tick, kutuma mafaili makubwa zaidi, kubadilisha themes na fonts, au kuficha status ya online. Hii ndiyo sababu watu wengi husifia kuwa halisumbui na linaonekana rahisi kutumia.
Hata hivyo, changamoto kubwa ya GB WhatsApp ipo kwenye usalama. Kwa sababu halijatengenezwa na Meta, haina security patches wala end-to-end encryption ya uhakika. Hii inamaanisha data zako meseji, picha, na namba za simu ziko wazi kudukuliwa. Mbaya zaidi, kuna matoleo mengine ya GB WhatsApp yaliyowekwa spyware na malware kwa makusudi, hivyo simu yako inaweza kudhibitiwa au kuibiwa taarifa zako binafsi.
Kwenye upande wa matumizi, WhatsApp rasmi pia huchukua hatua dhidi ya accounts zinazotumia GB WhatsApp. Wamekuwa wakizifungia au kutoa onyo mara kwa mara kwa sababu matumizi yake ni kinyume na masharti yao ya huduma. Kwa hiyo unaweza kujikuta siku moja account yako rasmi imefungiwa bila tahadhari kwa sababu ya kutumia hii app isiyo rasmi.