Gazeti la MwanaHalisi latuhumiwa kwa kueneza uongo suala la Askofu Malasusa

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
18,173
13,776
Gazeti la Upendo, linalomilikiwa na Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la KKKKT, limekuja na kulituhumu la gazeti la Mwanahalisi kwa kueneza uongo usiothibitika juu ya Askofu Malasusa.

Gazeti hili la Mwanahalisi liliandika katika Makala zake zaidi ya wiki moja iliyopita kuwa ati Ask Malasusa kakamatwa ugoni na mume wa mtu mmoja aitwaye Mwakilima.

Lakini kuna mambo mengi ambaya gazeti hili aidha limekuwa kama chachu ya kueneza uongo na kuchochea ufarakano ndani ya kanisa kwa kusema ati Malasusa amekuwa mgoni wa mke wa Mwakilima ambaye ni mchungaji katka kanisa la KKKT.

Aidha ni kweli kuwa Mwakilima alimpiga mke wake na kumpeleka hospitali ya TMJ, ambako baada ya Malasusa kwenda pale na MKE WAKE(mke wa Askofu) walimhamishia Muhimbili.

Pamoja na mke wa Askofu hapo Muhimbili, alikuwapo pia Mmissionari mmoja mzungu. Hilo Mwanahalisi haliongelei kabisa.

Na habari mbazo hazijathibitishwa ni kwamba mke wa Mwakilima ndiye alifungua shtaka la kupigwa na mumewe, wakati Mwakilima alifungua shtaka la mke kutoonekana nyumbani(bada ya kipigo) pamoja na watoto.

Vil vile wanandoa hawa wawili wameamua kufuta kesi hizo kwa ridhaa zao.
Na mbaya zaidi Mwakilima inasemekana yaliyoongelewa na MwanaHalisi anayakana kabisa kuwa ni uongo na hajawahi kwenda gazeti hili kuliongelea juu ya ndoa yake, licha ya kuombwa na waandishi wa gazeti hili kwa simu juu ya ugomvi ndani ya ndoa yake.

MY TAKE
Shetani wa mapembe anatumika kupitia gazeti hili
 
Waandishi wa habari za aina hii mara nyingi kama sio mara zote huwa wanakuwa na record ya mazungumzo kwa hiyo mwakilima hawezi kuruka hapo, lakini malasusa akanushe yeye mwenyewe maana hii sio kashifa ndogo
 
Hivi Bishop Malasusa hajasikia tuhuma hizi?
Je ni ndogo kumfanya apuzie?
 
Ukweli ni kwamba dhambi ya uzinzi ipo sana makanisani na yakifanywa na hao hao viongozi wa dini. Hata kama hakuna ushaidi wa kudhibitisha lakin ukweli utathibikika siku moja
 
hahaha zamu zamu, sasa hivi ni zamu za malaxuxa, zamani zilikuwa zamu za mwumini wake lowaxa kuandamwa na mwanahalisi, acha nae askofu aipatepate joto ya jiwe ya magazeti ya udaku ya mwanahalisi, hahaha cheze elimu ya hapa na pale wewe!!!!
 
Mwanahalisi wamejidhalilisha sana!...Hawana budi kuliomba Kanisa na MUNGU msahamaha haraka!
 
  • Thanks
Reactions: F9T
Hivi Bishop Malasusa hajasikia tuhuma hizi?
Je ni ndogo kumfanya apuzie?

Askofu Malasusa haangaiki na mambo ya ulimwengu huu wa kwako. Yuko ulimwengu mwingine wa Roho. Alisema Anamtumikia zaidi yule aliyemtuma kazi, na ndiye anayejua ukweli. Hamtumikii Kubenesalam.
 
Waandishi wa habari za aina hii mara nyingi kama sio mara zote huwa wanakuwa na record ya mazungumzo kwa hiyo mwakilima hawezi kuruka hapo, lakini malasusa akanushe yeye mwenyewe maana hii sio kashifa ndogo
i vema mwandishi wa Mwanahalisi akiweka hadharani clip ya kumkamata mgoni wae ili mwongo ajulikane.
Kama ile ya polisi wa Mahiga ingekuwa poa!!
 
Hivi Bishop Malasusa hajasikia tuhuma hizi?
Je ni ndogo kumfanya apuzie?
Ni ukweli hizo tuhuma Si mdogo. Mpaka hapo tu. Lakini tuhuma zile zinaacha maswali Mengine, na sijui kilichomkereketa mwandishi kuandika habari ya namna ile.

Naamini hata kama ni ukweli Askofu hakutoa "ushirikiano",
mwandishi alitakiwa aende mbele zaidi(ajiongeze) kujiridhisha na mambo haya mawili:

Mosi: Je, kuna mwanafunzi anayeenda kusoma kusoma Makumira bila kupitia mkondo wa ufadhili wa Dayosisi, ili kuthibitisha maelezo kuwa mlalamikaji aliingia "gharama" kubwa kumsomesha make wake?

Pili: Kama mlalamikaji alizua tafrani, alipokamatwa, tena eti kwa kwa amri ya Mkuu wa mkoa, pale Muhimbili, ilikuwaje akapelekwa Wazo Hill, ukizingatia kuwa mtuhumiwa anashikiliwa eneo alikofanyia tuhuma, katika suala hili amani Msimbazi au Central?

Tatu: Hivi mwandishi aliandikaje maelezo kuwa mlalamikaji alipata "amri" kutoka Mahakama ya Mwanza Kibaha "kutaka Kamishna wa Uhamiaji kuzuia watoto kutoroshwa? Amri ya kumzuia afisa wa Serikali asifanye kazi yake inaitwa "prerogative order" na hutolewa na Mahakama Kuu tu.

Bila kukubali au kukataa tuhuma, nadhani baada ya maelezo hayo, ambayo mwandishi hakujishughulisha kujiridhisha nayo, nashindwa kuelewa habari hii maana yake ilikuwa nini?

Just thinking aloud!!
 
Ni ukweli hizo tuhuma Si mdogo. Mpaka hapo tu. Lakini tuhuma zile zinaacha maswali Mengine, na sijui kilichomkereketa mwandishi kuandika habari ya namna ile. Naamini hata kama ni ukweli Askofu hakutoa "ushirikiano", mwandishi alitakiwa aende mbele zaidi(ajiongeze) kujiridhisha na mambo haya mawili:
Mosi: Je, kuna mwanafunzi anayeenda kusoma kusoma Makumira bila kupitia mkondo wa ufadhili wa Dayosisi, ili kuthibitisha maelezo kuwa mlalamikaji aliingia "gharama" kubwa kumsomesha make wake?
Pili: Kama mlalamikaji alizua tafrani, alipokamatwa, tena eti kwa kwa amri ya Mkuu wa mkoa, pale Muhimbili, ilikuwaje akapelekwa Wazo Hill, ukizingatia kuwa mtuhumiwa anashikiliwa eneo alikofanyia tuhuma, katika suala hili amani Msimbazi au Central?
Tatu: Hivi mwandishi aliandikaje maelezo kuwa mlalamikaji alipata "amri" kutoka Mahakama ya Mwanza Kibaha "kutaka Kamishna wa Uhamiaji kuzuia watoto kutoroshwa? Amri ya kumzuia afisa wa Serikali asifanye kazi yake inaitwa "prerogative order" na hutolewa na Mahakama Kuu tu.
Bila kukubali au kukataa tuhuma, nadhani baada ya maelezo hayo, ambayo mwandishi hakujishughulisha kujiridhisha nayo, nashindwa kuelewa habari hii maana yake ilikuwa nini?
Just thinking aloud!!
Huyu mwandishi wa Kubenea ni kama ana visasi na Malasusa, kama alimvhukulia mke wake na aseme tu.
Baada ya kufuatilia habari ya Mwanahalisi haina mbeke wala nyuma.
Ukanjanja mtupu.
Ugoni ulifanyika gesti gani?
Nani mashahidi?
Umbea ni kuambiwa bibi fulani kalalea na kibosile fulani, Mwanahalisi mbio kuachapisha bila ushahidi!
Habari yote ina only circumstancial asuumed evidence badala ya factual evidence.
Na hilo ni tatizo la waandishi wenye elimu ya hapa na pale.
 
Huyu mwandishi wa Kubenea ni kama ana visasi na Malasusa, kama alimvhukulia mke wake na aseme tu.
Baada ya kufuatilia habari ya Mwanahalisi haina mbele wala nyuma.
Ukanjanja mtupu.
Ugoni ulifanyika gesti gani?
Nani mashahidi?
Umbea ni kuambiwa bibi fulani kalalwa na kibosile fulani, Mwanahalisi mbio kuachapisha bila ushahidi!
Habari yote ina only circumstancial assumed evidence badala ya factual evidence.
Na hilo ni tatizo la waandishi wenye elimu ya hapa na pale.
Du nimejitekenya...
 
Tatizo hujaleta habari za ukanushi tu bali umeleta habari za utetezi.
Sawli langu kwako, je huyo jamaa alipewa taarifa za kuhamishwa mke wake kwenda muhimbili na nani? Wewe kama una mke halafu chanzo cha ugomvi ndo unasikia kashiriki kumhamisha mkeo hospitali utapata jawabu gan?
Anyway Malasusa ni binadam na sio Mungu kukosea ni kawaida.
 
hahaha zamu zamu, sasa hivi ni zamu za malaxuxa, zamani zilikuwa zamu za mwumini wake lowaxa kuandamwa na mwanahalisi, acha nae askofu aipatepate joto ya jiwe ya magazeti ya udaku ya mwanahalisi, hahaha cheze elimu ya hapa na pale wewe!!!!

hahaha zamu zamu, sasa hivi ni zamu za malaxuxa, zamani zilikuwa zamu za mwumini wake lowaxa kuandamwa na mwanahalisi, acha nae askofu aipatepate joto ya jiwe ya magazeti ya udaku ya mwanahalisi, hahaha cheze elimu ya hapa na pale wewe!!!!
Mkuu ungeacha kwanza kunena kwa lugha ndipo uje uandike vizuri
 
Clinton alipopata ile Scandal ya Monica Lewinsky Ikulu yao haikujibu kitu maana walisema iyo ni personal affairs ikulu haiusiki fanyeni uchunguzi na muwe huru sasa huku kanisa linaingilia kujibu ikionekana ni kweli mtasemaje...binadamu tuu huyo na mtihani wa kutokuoa ni mkubwa sana..tusubiri muda ndio utakao ongea..
 
Tatizo hujaleta habari za ukanushi tu bali umeleta habari za utetezi.
Sawli langu kwako, je huyo jamaa alipewa taarifa za kuhamishwa mke wake kwenda muhimbili na nani? Wewe kama una mke halafu chanzo cha ugomvi ndo unasikia kashiriki kumhamisha mkeo hospitali utapata jawabu gan?
Anyway Malasusa ni binadam na sio Mungu kukosea ni kawaida.
Ni kwei ni utetezi kwa vile waliotajwa kwa kiasi fulani wote nawafahamu.
Hi stori ya Mwanahaisi hana ushahidi wowote licha ya kuchafua watu.
Angeleta iron cad proof tungeliaini, hakuna binadamu asiye na mapungufu, ila hapa ni kuchafuana tu.
 
Back
Top Bottom