Gazeti HOJA lazidi kuiandama CHADEMA.

Gazeti HOJA lazidi kuiandama CHADEMA.

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Gazeti la HOJA linalomilikiwa na anayedaiwa kuwa ni kada mashuhuri wa CCM limeendelea kutoa taarifa mbalimbali za kukichafua chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA.

Gazeti hilo linalotoka kila Ijumaa limekuwa likiandika taarifa na makala mbalimbali zinaonekana wazi ni za kisiasa zenye lengo la kuichafua CHADEMA mbele ya Jamii.

Gazeti hilo hivi karibuni lilitoa kile linachodai ni njama za viongozi wa chama hicho kutaka kumfukuza uanachama mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.Pia wiki nyingine iliyofuata lilishambulia operesheni M4C kwa madai kwamba ni feki na ina lengo la kuvuruga amani ya nchi.

Pia siku chache zilizopita gazeti hilo lilishambulia wabunge wa CHADEMA kwamba ni wabunge wa hovyo na wasiojua kanuni wala sheria na kuwaomba watanzania wasichague tena wabunge wa chama hicho.

Wiki iliyopita gazeti hilo la HOJA lilidai makao makuu ya CHADEMA yanamwandaa Josephine Slaa kugombea ubunge jimbo la Kawe.Lengo kubwa la habari hiyo ni kuleta vurugu kati ya Josephine na Halima Mdee na kuwachanganya wanachama.

Katika toleo lake la Jana gazeti hilo lilidai CHADEMA kinajiandaa kumfukuza uanachama mbunge wake John Shibuda kwa kile walichodai waliona ripoti ya Marando kwenda Kamati kuu inayodai Shibuda ni mamluki wa CCM na anapaswa kufukuzwa mara moja.Pia kwa unafiki mkubwa gazeti hilo lililaani viongozi wa CHADEMA wenye kadi za CCM kwa madai wanahujumu demokrasia ndani ya vyama vingi.

Kwa mifano hii niliyotoa hapo juu ni wazi gazeti hili linaonekana wazi lipo kwa malengo maalum.
 
Watanzania wa leo wanauwezo wa kutenganisha ukweli na uwongo,so majamaa na magazeti yao uchwara wanajizingua
 
Ni kweli kabisa mkuu, kazi hii inafanywa kupitia magazeti rafiki na CCM na mitandao ya kijamii. Ushahidi wa kutosha ni kuibuka kwa kundi la wana - CCM maslahi kuibuka na hoja hizi ili CDM wajadili migogoro ambayo haipo na kuacha hoja za msingi kama ugumu wa maisha na wizi wa mali za umma unaofanywa na CCM. Kinara wa Kampeni hizi ni katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Bwana neppie nnauye!
 
Watanzania wa leo wanauwezo wa kutenganisha ukweli na uwongo,so majamaa na magazeti yao uchwara wanajizingua

Na sasa hivi magazeti ya aina hii yanayoandika habari za majitaka yanazidi kuongezeka.
 
Ni kweli kabisa mkuu, kazi hii inafanywa kupitia magazeti rafiki na CCM na mitandao ya kijamii. Ushahidi wa kutosha ni kuibuka kwa kundi la wana - CCM maslahi kuibuka na hoja hizi ili CDM wajadili migogoro ambayo haipo na kuacha hoja za msingi kama ugumu wa maisha na wizi wa mali za umma unaofanywa na CCM. Kinara wa Kampeni hizi ni katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Bwana neppie nnauye!
Hii ndiyo kazi ya kitengo cha propaganda cha CCM ambayo hata hivyo itashindwa vibaya. Watanzania wa leo wana uelewa mpana na si rahisi kudanganyika. Kwani hawauoni umasikini, dhiki na dhuluma zinazosababishwa na chama cha mashetaani hawa wanaojiita CCM? Wizi unaofanyika kweupee, ufisadi ulioliangamiza taifa wa kuuza na kugawana ardhi, viwanda zaidi ya 400, madini, kuhujumu uteendaji wa asasi muhimu kwa wananchi kama Tanesco (Richmond/Dowans) EPA na mengineyo bado yanatutia kichefuchefu hata kulisikia hilo dude linaloitwa CCM.

Hii ndiyo demokrasia ya CCM; kufungia magazeti na vyombo vinavyosema ukweli tupu na kuviacha vyombo vinavyoandika *****! Hapa unajitokeza umuhimu wa CHADEMA kuanzisha vyombo vyao vya habari kama ilivyo kwa vibaka hawa wanaomiliki Redio, magazeti na hata Runinga inayoendeshwa kwa gharama ya kodi zetu (TBC). Down with CCM!
 
wabongo wa leo sio km wale wa mwaka 47. wanajua kuchambua pumba na mchele. hawampati mtu ng'o.
 
Hivi bado kuna watu wanaolisoma gazeti hilo na kukiamini kilichoandikwa ndani yake?
 
Mungu wangu hvi nchi hii ina gazeti linaloitwa HOJA? walahi mi naishi iringa mjini mwaka wa 20 sasa cjawahi linaona hilogazeti,
 
Siku zote tunasema ugomvi wa wa Tz na CCM ni dhuluma ambazo tunafanyiwa na serikali hii , bila kuondoa dhuluma ( kitu ambacho hakiwezekani ) ccm imekwenda ! That man Nape is very transparent , hakuna atakachopanga kisijulikane , hana uwezo wa kuokoa ccm kwa njama , it is over .
 
Gazeti la HOJA linalomilikiwa na anayedaiwa kuwa ni kada mashuhuri wa CCM limeendelea kutoa taarifa mbalimbali za kukichafua chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA.

Gazeti hilo linalotoka kila Ijumaa limekuwa likiandika taarifa na makala mbalimbali zinaonekana wazi ni za kisiasa zenye lengo la kuichafua CHADEMA mbele ya Jamii.

Gazeti hilo hivi karibuni lilitoa kile linachodai ni njama za viongozi wa chama hicho kutaka kumfukuza uanachama mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.Pia wiki nyingine iliyofuata lilishambulia operesheni M4C kwa madai kwamba ni feki na ina lengo la kuvuruga amani ya nchi.

Pia siku chache zilizopita gazeti hilo lilishambulia wabunge wa CHADEMA kwamba ni wabunge wa hovyo na wasiojua kanuni wala sheria na kuwaomba watanzania wasichague tena wabunge wa chama hicho.

Wiki iliyopita gazeti hilo la HOJA lilidai makao makuu ya CHADEMA yanamwandaa Josephine Slaa kugombea ubunge jimbo la Kawe.Lengo kubwa la habari hiyo ni kuleta vurugu kati ya Josephine na Halima Mdee na kuwachanganya wanachama.

Katika toleo lake la Jana gazeti hilo lilidai CHADEMA kinajiandaa kumfukuza uanachama mbunge wake John Shibuda kwa kile walichodai waliona ripoti ya Marando kwenda Kamati kuu inayodai Shibuda ni mamluki wa CCM na anapaswa kufukuzwa mara moja.Pia kwa unafiki mkubwa gazeti hilo lililaani viongozi wa CHADEMA wenye kadi za CCM kwa madai wanahujumu demokrasia ndani ya vyama vingi.

Kwa mifano hii niliyotoa hapo juu ni wazi gazeti hili linaonekana wazi lipo kwa malengo maalum.

Sawa wanaandika lakini inabidi wajiulize, je linasomwa? maana mimi tangu nizaliwe sijawahi kuliona kwa hiyo wanachokifanya ni kazi bure kwani wanaolisoma ni hao hao CCM kwa hiyo ujumbe hauwafikii walengwa unabaki kwao wenyewe.
 
Nigazeti la usalama wa taifa ambalo ukilinunua mara moja hutalinunua tena maana kwa vyovyote utagundua ni uongo. wanachapisha nakala 1000 zinanunuliwa 200 kati ya hizo ofisi za CCM wananunua 100 na 800 zinabaki kufungia maandazi, kwa kweli yanasaidia sana wajasilia mali kupata vifungashio
 
Ni gazeti la propaganda la UVCCM, mhariri wake ni naibu meya wa Kinondoni, Songoro.

SAM_1202.JPG

Mbunge wa Kinondoni Azan akiwa na Songoro mhariri mkuu wa gazeti la HOJA
 
CCM Wanajisumbua, watanzania wameshaamua kubadilika, hawasikii wala hawaoni, wao wanaiamini CHADEMA na WANAIHITAJI.
 
Sasa nimejua kwa nini walifuta mwanahalisi ili magazeti yao ya udaku wapate nafasi ya kuchefua umma wa watanzania HATUDANGANYIKI NG'O!
 
Ni juhudi za lumumba za mfa maji haishi kutapatapa.

Wana mikakati mingi sana kila kona inabidi watanzania wapenda mabadiliko kuwa nao macho hawa mafisadi.

Watafisadi kila kitu lakini hawataweza kufisadi akili zetu!
 
Back
Top Bottom