Gawio kwa wanahisa wa CRDB na NMB

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Nimesoma kupitia vyombo vya habari kuwa gawio kwa hisa moja ya CRDB ni Tshs.8.00 na gawio la NMB ni Tshs.66.00 mwaka huu. Hivi Benki kubwa kama CRDB inatoa Tshs.8.00 wakati Benki shindani inatoa Tshs.66.00. Hili ni jambo lisiloweza kuvumiliwa kwa Benki ya CRDB na inabidi Benki hii ijitafakari sana.
 
Mkuu, is it really that simple?

Mimi sina ujuzi na hisa and what not lakini mbona kama unalifanya lionekane rahisi sana, kwamba competiting businesses zote ziwe na dividend zinazoendana?

Haitegemeani idadi ya hisa, faida, bei ya hisa, na vitu vingine?
 
Fanya hesabu kidogo ujue kwa kila shilingi ya hisa unapata faida kiasi gani ili uweze kulinganisha benki tajwa kiuwekezaji.

Sasa ukiangalia Bei ya hisa nmb ni 2000, crdb ni 120.

Kwa Nmb 66/2000 unapata 0.033 kwa maana kila shilingi mia unapata shilingi tatu faida

Kwa crdb vilevile, 8/120 unapata 0.066 yaani kila mia unapata shilingi 6.

Maana yake ukiwekeza shilingi mia, unapata gawio mara mbili zaidi crdb ukilinganisha na nmb
 
Gawio lolote lile linategemea idadi ya hisa ambazo mmbia amewekeza. Kuna wanahisa wengine hutumia sehemu ya gawio kuongeza mtaji.
 
Tuambie kwanza magawio ya miaka ya nyuma ilikuaje anza na 2014-2018 hapo tunaweza kusema lolote,hapa ulipotuweka what if magawio ya nyuma wamezoea 2Tsh au hata Tsh 5?

Back
Top Bottom