Gavana: Uchumi wetu unakua

kupelwa

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
1,087
450
BENKI Kuu ya Tanzania imesema kuwa uchumi wa nchi unakua kwa asilimia 7.1 ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika ambazo zipo katika kiwango cha asilimia 5 ya ukuaji.

Hayo yalisemwa jana na Gavana wa Benki Kuu, Prof. Benno Ndulu mara baada ya kuzindua matumizi ya teknolojia katika uuzaji wa hati fungani na dhamana za serikali kwa kutumia kompyuta.

Gavana alisema kulingana na Shirika la Takwimu uchumi umekua ukilinganisha na nchi kama za Kenya, Uganda na Burundi, isipokuwa Rwanda ambayo imefikia kiwango cha asilimia 7.7.

Alisema hata mfumuko wa bei umepungua na kufikia asilimia 15.7 ambapo kwa mwezi Julai ulikuwa juu kwa asilimia 19.8 huku akiahidi kuwa utaendelea kushuka.

"Nazungumzia kitaalamu na si kisiasa, maana mwezi wa nane mwaka huu kila mtu ameona, hata unapopita sokoni bei za bidhaa zimeshuka hadi mafuta pia yameshuka bei, sijui kwa hapo baadaye endapo kutatangazwa bei nyingine, lakini matumaini yangu ni kuendelea kushuka zaidi," alisema Prof. Ndulu.

Akizungumzia kushuka kwa thamani ya shilingi, alisema kwa mwaka jana hali ilikuwa mbaya kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi ambapo ilifikia sh 825.40 lakini kwa sasa ni kati ya sh 1,573 hadi 1,590 kwa soko la kijumla.

"Mfumuko wa bei kwa upande wa Tanzania uliokuwa kiburi ni chakula na wenzetu hao hata Wakenya wao wanategemea sana ‘sukuma wiki' ambao upatikanaji wake ni rahisi, sisi tunategemea mchele, mahindi ambapo pengine takwimu zao zinatokana na uvushaji wa vyakula hivyo kwao," alisema Prof. Ndulu.

Aidha, Gavana Ndulu jana alifungua rasmi matumizi ya teknolojia katika uuzaji wa hati fungani na dhamana za serikali ambapo hapo awali wawekezaji walilazimika kubeba vikapu vya hela kufanya malipo Benki Kuu.

Alisema katika kipindi hicho chote kilihusisha utoaji wa hatimiliki na utumiaji wa masanduku kwa ajili ya kupokea maombi ya uwekezaji katika hatifungani na dhamana za serikali.

Ndulu alisema mfumo huo ni njia salama na rahisi ya umilikaji wa dhamana ukilinganisha na umiliki kwa kutumia hati.


CHANZO: GAZETI LA TANZANIA DAIMA - 1/9/2012
 
Back
Top Bottom