Kwa maelezo yako (1.6 Litre engine) haikutakiwa kuwa na ulaji wa mafuta mbaya. Labda uangalie mambo mawili.
1) Ifanyie service gari yako huenda ina matatizo
2) Angalia unavyoendesha gari, hapa ninamaanisha mambo kama vile kuondoa gari kwa kasi kubwa, kukanyaga sana mafuta n.k, ukiwa "dereve mpole" inasaidia sana kuokoa mafuta. Kama unayo manual ya gari soma zaidi kwani kampuni nyingi huandika kipengele cha namna ya kuokoa mafuta katika matumizi ya gari.