Wakubwa saiz ndo nimetoka garage na kazi bado ,,, unajua ilikuaje ?
Mwaka jana kuna jamaa alikuwa anauza gari yake aina ya noah , ambayo ilikuwa inapiga route za kule nyumbani kutoka kijijin kwenda mjini , na aliamua kuuza baada ya kuona watoto wa shule wamemtinga kidogo hivyo kwasababu na mimi nilikuwa naupenda ule mradi ikabidi niinunue ile noah lakin baadae nikatafuta noah mpya , hivyo mwezi Jan 2025 ikabidi nitoe kule kujijini niilete mjini kufanyiwa marekebisho ,, kuna jamaa yangu mmoja tumesoma wote muhas aliniunganisha na huyo fundi na mara kadhaa amewahi nirekebishia nisan yangu hivyo sikuwa na mashaka na ufundi wake , hivyo ikabidi nimtume aende akachukue ile gari kule kijijin ili ifanyiwe matengenezo ya maana mjini , dogo akaenda kuichukua ile gari tarehe 5 Jan 2025 ,, kumbuka kuwa mim niko mbali na huo mkoa ambako dogo ndo inabidi atengeneze hiyo gari , dogo alipoichukua gari na kufika mjini akaifungua na kuniambia vifaa vinavyotakiwa na alinipigia hata picha na kweli gari ilichakaa , hivyo akanitumia kwa njia ya wasap mahitajio yote ya vifaa na mim kwasababu nilikuwa na mwamini nikampa first phase 1M na baadae akaja kunidai tena 500k maana jumla ya garama ya vifaa ilikuwa tsh 1.5M hapo mbali na bodi repaire , wakubwa to make the story short nikaomba ruhusa kazini ili nije hapa mbeya kufuatilia gari langu aisee nimeshangazwa kwa kweli japo wa kunyosha na kupiga rangi alifanya kazi yake vizuri , ila shida huyu niliyemwamini kwa vifaa vya upande wa chini wa gari ni balaa kumbuka mpaka saiz gari imekaa miez 2 garage
Nimekuta gear box ndo kwanza anahangaika nayo kwasabu ameona nimekuja physically , nikajua maybe ndo kilibaki kidogo badae nikaona tari la kushoto la mbele ni kama lina together nikamuliza hii vip akasema ukienda kufanya wheel alignment itanyoka , so ikabidi niende kufanya will alignment kufika pale na kuwakuta baadhi ya mafundi aisee ndiyo kimbembe kikaanza baada ya hata wao kuanza kulikagua na kubain kuwa ile gari haijafanyiwa chochote cha maana kule chini na hata ingetokea nikaanza safari lolote lingenitokea , na imebidi nianze kununulishwa spare upya maana yule dogo wakati nampigia akawa yuko mbali amenikimbia anaishia kusema nisamehe tu bro ,, na ndiyo mda ule nikawambia niombeeni maana imebidi nianze upya tena
Ushauri wangu kwenu ,, ukiwa unatengeneza gari kaaa hapo hapo uone spare unayonunulishwa inakuja na unashihudia inafungwa kwenye gari lako ,, na ikiwezekana fundi akikwambia kinahitajika hiki nenda mwenyewe dukani ukajiridhishe hata bei ,,, silalamikii sana pesa ila dogo alitaka nipate matatizo makubwa njiani nashukuru Mungu ambaye alinifanya niende kufanya wheel alignment na ndipo mafundi wengine wakabain matatizo lukiko
Nimejaribu kueleza kwa kifupi ila mwenzenu nimepigwa aisse