[B]Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi alikanusha kuhusika kwa Chenge na kudai kuwa mwendesha pikipiki huyo alipinduka mwenyewe kutokana na mwendo mkali na hivyo kusababisha kifo chake.[/B][/QUOTE]
Hayo maneno yamenisikitisha sana sana sana. Yaani badala ya kuwa responsible na alichokifanya anasingizia ati marehemu amepinduka mwenyewe...........this is unbeliavable!!! Sikujua kuwa ufisadi unaweza kuondoa utu wa mtu na kuweka unyama ndani yake. Na hao polisi wanaotumika kuficha makosa ya ufisadi....... dhambi yao ni ile ile sawasawa na ya chenge na Mungu hatawaacha wapate amani kwa kudhulumu mali na maisha ya wanyonge wa TZ.
Mganga wake jasiri kweli kweli.
si bure jamaa anakiburi kwa sababu ana walinzi wasioonekana
Huko Gambosh inadaiwa ni kijiji cha misukule, usishangae kusikia maiti imetoweka!
Kama hilo suala halimuhusu mheshimiwa, hakuhitaji kujibu kwa hasira.
Mizumu ya wale wadada wawili alioua kisa anawafuatilia kwa mbali baada ya kushindwa kuelewana walipokuwa wanachapa maraha usiku wa manane haitamwachia. Halafu anakana na tena kukana kabisa kuwa hakuwa na uhusianao na mmoja wao. Kweli ukishakuwa marehemu huna thamani. Kweli na kilio cha roho kimsute huyo Chenge a.k.a mzee wa tujisenti.
...........kafara la uchaguzi au kesi?
Huu utawala wa sheria Tanzania una maana gani? Mashuhuda wameona kwa macho yao, polisi wameona kwa fikra zao (rushwa) na wanakuja publicly kusema pumba. no wonder yule jaji asishtakiwe kwa kugonga na kuua pamoja na kujeruhi dar..... UTAWALA WA SHERIA
naomba mtu anielimishe hapo
'Ameua, halafu akashuka akahamia gari lingine...!' Huu ni ufidhuli kama kawaida yake, badala ya kumbeba aliyemgonga hata amuwahishe hospitali kuokoa uhai wake, yeye anaukimbia ushahidi...uhai wa kijana ukaachwa inaangamia! Ndiyo maana LAANA ya MUNGU ITAWATAFUNA TU! Ndiye aliyesema Kibajaji alichokigoga, eti ndicho kiliacha njia kikafuata gari lake...! Kodi za Watanzania anachota kupeleka account za nje, anapoulizwa anasema mnadani nini? eti Vijisenti? MWACHENI MUNGU ATENDE HUKUMU ZAKE!