Gari la Chenge lagonga tena, LAUA!

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
chengecrop.jpg

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi mkoani Shinyanga (CCM), Andrew Chenge

Zulfa Mfinanga, Shinyanga na Ramadhan Semtawa, Dar

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi mkoani Shinyanga (CCM), Andrew Chenge ameingia matatani tena baada ya gari lake kudaiwa kumgonga mwendesha pikipiki na kusababisha kifo wakati akitoka kwenye kampeni.

Tukio hilo limetokea wakati mwanasheria huyo wa zamani akiendelea na kesi ya mashtaka mawili ya kuendesha kizembe na kugonga pikipiki ya matairi matatu na kusababisha vifo vya watu wawili na jingine la kuendesha gari ambalo bima yake ilishaisha.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa katika ajali ya jana waziri huyo wa zamani wa Miundombini hakuwa akiendesha gari hilo, bali alikuwa ndani.

Habari zilizopatikana jana kutoka wilayani Bariadi zimeeleza kuwa Chenge akiwa anatokea Kijiji cha Namisagusa na Kilalo alikokuwa na mkutano wa kampeni kuelekea mjini Bariadi, alipata ajali hiyo katika Kijiji cha Mbiti kilicho Kata ya Mhango, Tarafa ya Ntunzu.

"Hii ajali imetokea majira ya saa 1:00 usiku, Chenge baada ya kuona gari lake limegonga alishuka na kuhamia katika gari jingine na kuondoka eneo hilo. Wananchi walipofika hapo walilizuia gari hilo, lakini baadaye wakatimuliwa na polisi ambao waliliondoa gari hilo," alieleza Patrick Liyuba mmoja wa wananchi wanaodai kushuhudia ajali hiyo.

Chenge mwenyewe alipoulizwa kwa njia ya simu kutoka jimboni kwake, alianza kutoa maneno makali akisema ''andikeni umbea wenu kama mnavyotaka''.

''Sitaki umbea wenu. Niko kwenye jukwaa naomba kura kwa wananchi, ninyi mnaniambia umbea wenu. Tumeshawachoka na umbea wenu mnaoandika kila siku,'' alisema waziri huyo wa zamani wa Afrika Mashariki.

Mgombea huyo ubunge alihoji: ''Kwani polisi wamesameje.''

''Kama wenyewe wenye mamlaka ya kusema wameshasema, mnanipigia mimi ili iweje. Muda wangu ni muhimu sana kuliko kusikiliza umbea wenu wa magazeti, tumewachoka kuwasikiliza, muulizeni huyo aliyewatumia.''

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi alikanusha kuhusika kwa Chenge na kudai kuwa mwendesha pikipiki huyo alipinduka mwenyewe kutokana na mwendo mkali na hivyo kusababisha kifo chake.

Kamanda Siasi alidai kwamba pikipiki hiyo aina ya SUNLG iliyokuwa ikiendeshwa na Penga Machunga, 30, mkazi wa Gamboshi ilipinduka na kusababisha kifo chake papo hapo.

"Ni kweli kwa mujibu wa taarifa za maofisa wangu huko wilayani Bariadi wameripoti kuwepo kwa ajali hiyo ya pikipiki, lakini kama inahusisha gari la Chenge au la nani, basi naomba wananchi ambao wameshuhudia watoe taarifa hizo na sisi tutachunguza na kubaini ukweli," alieleza Kamanda Siasi.

Alisema kama kuna watu ambao wanajua kuwepo kwa tukio hilo na wanaweza kutoa maelezo ya kina, wafike kituo cha polisi na kueleza hayo ili jeshi lake liendelee na uchunguzi.

Katika miaka ya karibuni, Chenge ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali, amejikuta akikumbwa na mikasa mikubwa kuanzi ule wa kuhojiwa na Taasisi ya Makosa Makubwa ya Uingereza (SFO) iliyokuwa ikichunguza kasfa ya ununuzi wa rada kutoka Kampuni ya BAE Systems.

Katika uchunguzi huo, akaunti moja ya Chenge ilionekana kuwa na kiasi cha S1.2 bilioni, ambazo mbunge huyo wa Bariadi alizielezea kama vijisenti

Source: MWANANCHI.
 
Huu utawala wa sheria Tanzania una maana gani? Mashuhuda wameona kwa macho yao, polisi wameona kwa fikra zao (rushwa) na wanakuja publicly kusema pumba. no wonder yule jaji asishtakiwe kwa kugonga na kuua pamoja na kujeruhi dar..... UTAWALA WA SHERIA
naomba mtu anielimishe hapo
 
Huyu jamaa huyu mabalaa hayamwachi tu?
Bungeni alishikwa akimwaga uchawi,
anakesi ya kuua kwa kugonga kibajaji, kisa amekataliwa.
Haya sasa kaenda kumimina damu nyingine huko jimboni kwake.
Kweli kazo anayo
 

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi alikanusha kuhusika kwa Chenge na kudai kuwa mwendesha pikipiki huyo alipinduka mwenyewe kutokana na mwendo mkali na hivyo kusababisha kifo chake.

Kamanda Siasi alidai kwamba pikipiki hiyo aina ya SUNLG iliyokuwa ikiendeshwa na Penga Machunga, 30, mkazi wa Gamboshi ilipinduka na kusababisha kifo chake papo hapo.

"Ni kweli kwa mujibu wa taarifa za maofisa wangu huko wilayani Bariadi wameripoti kuwepo kwa ajali hiyo ya pikipiki, lakini kama inahusisha gari la Chenge au la nani, basi naomba wananchi ambao wameshuhudia watoe taarifa hizo na sisi tutachunguza na kubaini ukweli," alieleza Kamanda Siasi.

Tayari wameshachakachua!!!
 
wananchi walitakiwa wamtandike kama paka mwizi. huyu jamaa anakiburi sana
 
Hii ni LAANA inamuandama huyu mzee na mimi nachikiona ni mwisho mbaya wa kutisha na wa aibu unamnyemelea , muda huu angetubu dhambi zake na kujiweka mikononi kwa mungu, makubwa yatampata muda sio mrefu
 
Siyo kila nayepata majaribu ni laana, bali ni mapenzi ya Mungu.
 
Huyu jamaa huyu mabalaa hayamwachi tu?
Bungeni alishikwa akimwaga uchawi,
anakesi ya kuua kwa kugonga kibajaji, kisa amekataliwa.
Haya sasa kaenda kumimina damu nyingine huko jimboni kwake.
Kweli kazo anayo
Mganga wake jasiri kweli kweli.
si bure jamaa anakiburi kwa sababu ana walinzi wasioonekana
 
Nimekugongea thanks lakini habari hii pia ipo kwenye forum ya habari mchanganyiko.:A S thumbs_up:
 
Unauhakika na unachik-i-n-e-na. Au huwa mnakutana naye huko, mimi hata hiyo avata yako siielewi, kama hirizi vile! au ndo walinzi wenyewe wasioonekana?:biggrin1:
 
'Ameua, halafu akashuka akahamia gari lingine...!' Huu ni ufidhuli kama kawaida yake, badala ya kumbeba aliyemgonga hata amuwahishe hospitali kuokoa uhai wake, yeye anaukimbia ushahidi...uhai wa kijana ukaachwa inaangamia! Ndiyo maana LAANA ya MUNGU ITAWATAFUNA TU! Ndiye aliyesema Kibajaji alichokigoga, eti ndicho kiliacha njia kikafuata gari lake...! Kodi za Watanzania anachota kupeleka account za nje, anapoulizwa anasema mnadani nini? eti Vijisenti? MWACHENI MUNGU ATENDE HUKUMU ZAKE!
 
Chonde chonde jamani. Mambo ya kumsingizia Mungu kwa matukio mliyoyafanya wenyewe ufe kabisa.
Kinachofanyika ni kwamba anapata malipo yake hapa hapa!
 
Back
Top Bottom