Gari ipi nzuri kati ya Harrier240G na Klugger

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,251
Watalaamu wa Magari naomba ushauri wenu wa kitalaamu Juu ya masuala ya Magari kati ya hayo Mawili toka injini mafuta vipuri Na uimara wake .
 
Chukua harrier mjomba iko very comfortable na imara suala la vipuri wala usiwaze ni hela yako tu.
 
kwa uimara ni harrier,kwa muonekano na fashion ni klugger maana harrier wengi sana wanazo
 
Chukua Harrier, hutasumbuka spare, spare ni rahisi kuzipata na kwa bei poa pale Ilala used na new one, mafundi wa Harrier mtaani ni wengi kuliko Klugger
 
Hakuna tofauti baina harrier na kluger isipokuwa body. Engine na chassis ndio hizohizo. Lkn kama unajali muonekano basi bora harrier.
 
Lkn uzuri kabla hujaamua zigoogle zote mbili. Utapata info nzuri ya kutosheleza. Mimi nilifanya hivyo na saivi nafurahia harrier yangu...
 
Nimenunua hivi karibuni ya 2006. Nimefurahia sana comfort, pamoja na build quality. Bila ya shaka zina nguvu ya kutosheleza barabarani kiasi cha kwamba overtaking haikupi shida kabisa. Ila cha kushangaza zaidi ni kuwa matumizi ya mafuta ni wastani. Hayatofautiani na gari zenye engine za lita 2. Clearance ni nzuri sana kwa barabara zetu. Mashimo madogomadogo inafunika vizuri. Na engine ukiitunza ndio mnakwenda nayo mpaka kilomita laki tatu bila ya shida. Ina drive chain. Ktk gari niliowahi kuwa nazo(honda crv, nissan xtrail, na toyota 4runner)mi naona hii ndio best. Nimejaribu kukuekea links zenye specification ila nashindwa kwa ushamba...unaweza ukani pm for more info
 
Back
Top Bottom