Nimekuwa pia nikiwafikiria hawa vijana wanaoendesha bajaji. Shida ninayoiona ni kwamba wako katika makundi na pia wako idle kwa muda mrefu.
Wakati manispaa inadhibiti wapiga debe, kundi ambalo litakuja kuwa genge la kuogopwa ni madereva taxi na waendesha bajaji. Kama hawatageuka kuwa wezi, basi watakuwa ni washirika muhimu katika maswala ya ujangili mijini.
Wakati wengine wanakazana kuwapa vijana wao elimu nzuri, sisi tunafanya makosa kukwepa gharama za kuwapa vijana ajira zenye kueleweka.
Ni heri madreva taxi wangeendelea kuwepo peke yao bila kuwaweka kwenye competition na hizi bajaji. Hizi quick fixes mimi siafikiani nazo.
Wengine wanasema, "Oh, sasa wao watakula wapi!", ...huwa nashangazwa na kauli hii.
Kwa nini leo tuanze kufikiria kumsaidia gardener, badala ya kupigania elimu bora kwa watoto wetu? Ukimsaidia gardener mmoja leo, kesho idadi yao itaongezeka; what are we going to do next?!
.