Gardaworld zamani KK Security

Gardaworld zamani KK Security

monotheist

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
887
Reaction score
1,596
Kuna mdau alitoa bandiko anatafuta kazi nilimuelekeza aende pale Gardaworld kuulizia kama intake mpya imeanza hatimaye wadau wengi walikuja PM ili niwape taarifa za hiyo kampuni nimeona niwajuze hapa ili iwe faida kwa wote

Gardaworld zamani KK Security huwa kila mwezi inaanza intake mpya nafikiri mwezi huu wa 12 wanaweza wakawa mapumziko japokuwa sina uhakika kwa sababu ratiba hubadilika ila mwezi wa kwanza utaratibu wao utakua unaendelea.

Muwe mnapita pale kwa ajili ya kuulizi kama kuna taarifa mpya kwa kweli hawa jamaa kwa upande wa malipo pesa inatoka muda muafaka tofauti na makampuni mengine ya ulinzi ambayo ni local pesa ya tarehe 30 unapewa tarehe 6 hadi 10.

Ofisi ipo Mikocheni B kituo kwa Mwinyi ukishuka ulizia ofisi za Gardaworld zamani KK Security na usaili unafanyika kila siku ya Alhamisi na Ijumaa.

Kwa upande wa malipo ni 250k na zaidi inategemea na lindo.

Hakikisha unakuwa na urefu wa foot 5.7 kwa mwanaume na 5.6 kwa mwanamke, umri kuanzia miaka 23+, uwe na elimu kuanzia form 4 na kuendelea, uwezo wa kuandika na kuongea kimombo pamoja na Kiswahili.

Mengine mtayafahamu pindi mtakapofika eneo husika.

Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom