Gap kati ya Afrika na Ulaya lipo hapa

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,798
3,766
Kipindi media zote kubwa kubwa zinatangaza mabaya mengi ya nchi za kiafrika na kutaka yapaziwe sauti huku nyuma ya pazia wanakuza teknolojia yao kwa kasi ya ajabu.

Tukimaliza kuchukiana waafrika tunaanza kuwashangaa wazungu kutokana na hatua za maendeleo walizopiga.

Leo Israel inawaza juu ya matumizi ya Artificial Intelligence kwenye Ozone ili kufanya environmental scanning na kupata taashira ya matukio makubwa ya mabadiliko ya kimazingira.

Wanatulisha sumu tunavurugana wanatulia wanafanya yao tukistuka tunashangaa halafu tunavurugwa tena.

Nafikiri falsafa ya UBUNTU inapaswa kuangaliwa sana katika kipindi hiki kama ni kweli inasadifu falsafa ya Afrika.
 
Sumu tulishane wenyewe halafu tuwasingizie wazungu. 100% shida ni sisi wenyewe, mfano umenunua meli mbovu kifisadi, wananchi wakianza kuhoji unaificha Jeshini, sababu vifaa vya kijeshi huwa havihojiwi. Kweli hapo kama Taifa mtapiga hatua?
 
Mzungu ameingiaje hapo eti jirani yako akifanikiwa mfano amenunua gali au kujenga nyumba utashangaa jirani anamloga hivi kwa nini watu weusi wana roho mbaya hivi eti tunasingizia mzungu sisi ni upumbavu wetu ndio umetufikisha hapa
 
Halafu unamsingizia mzungu!
Screenshot_20191029-082139~2.jpeg
 
Tatizo la sisi waafrika kubwa ni moja hatuna wagunduzi wa vitu na teknolojia mbali mbali.Ndipo tatizo kuu lilipo.Swala sio siasa Wala Nini ulaya imetawaliwa na Hadi madikiteta akina Hitler lakini kwenye ugunduzi ilikuwa mbele Hitler akiwepo

China ilijifungia milango kabisa ikawa haiuzi chochote nje Wala kununua chochote nje (closed economy) lakini ilikuwa na wagunduzi kibao haikutetereka kiuchumi kwa kutouza nje.Ilipoglfungua milango ikawa bado kinara wa uchumi.

Nchi bila kuwa na wagunduzi hata uwe na siasa Safi vipi utakuwa lofa tu
 
Waafrika tumelogwa na aliyetuloga kafa. Tuko tayari kulaumu watu wengine wooote ila kukubali udhaifu wetu hatutaki. Tuko tayari kulaumu mvua zinazovunja madaraja badala ya kukubali kwamba tumeshindwa kutunza mazingira.

Tumeacha watu wakalima kwenye miteremko na jirani na mito na matokeo yake maji ya mvua yakang'oa miti na mawe vikaenda kuvunja madaraja na kuharibu barabara ambazo gharama yake ni kubwa sana ukilinganisha na gharama za kutunza mazingira.

Tukiambiwa tunakosea mambo fulani hatutaki kukubali. Tunaji- "mwambafai" weee....na kujifanya tunajua kila kitu-jambo ambalo haliwezekani.

Ni kama tunajitekenya na kucheka wenyewe. Nchi za Afrika ni kama zina "upofu" wa ajabu. Tunafanya sensa za watu na tunajua kila mwaka ni vijana wangapi wanamaliza shule na watahitaji ajira. Lakini sijawahi kusikia nchi yoyote ya Afrika ina mpango kabambe wa kuhakikisha kwamba vijana wao wakimaliza vyuo wana hakika ya kupata ajira.

Zaidi ya hapo viongozi wengi sana wa Afrika ni wanafiki wa kutisha. Wako tayari kabisa hata kuapa kwamba kitambaa cheusi kina rangi nyeupe ili mradi mkuu wake wa kazi anataka kusikia hilo.

Na hao wanaoongozwa wakati tayari kusifia hadharani mambo yote lakini mkuu akiondoka zake wanasema kinyume kabisa na walivyokuwa wanasifia.

Kweli Afrika tumelogwa. Siku hizi, hata viongozi wa dini wanajiingiza katika kuwasifu viongozi wa kisiasa ili mradi wanufaike kwa misaada. Hawana tena ujasiri wa kukemea pale wanapoona kuna uonevu. Onasikitisha. Nchi zote Afrika ziko hivyo.
 
##
Ofkoz keanza kabisa wazungu wana mchango kwa kutokuendelea kwetu

##
wazungu pia wana kitu kinachoitwa "ngozi ya kondoo" wao ni weupe ila kwa nje wamevaa gamba jeupe So waafrika wote tunapowarizama tunawaona wao ni wweupe dhidi yetu na ndio maana watu kama kila lisu and the like wanapopata matatizo ya chumbani kwao huwapelekea wazungu wakijua kua wenzao ni weupe kumbe maskini ni wekundu

##
usalama wetu wa raifa unapaswa uwe na siri nyingi sa kimkakati za kimaendeleo ambazo si lazima zitangazwe mana kitangaza kila kitu tunazidi kuongeza maadau mana hawataki tujitegenee hawa
 
Tatizo la sisi waafrika kubwa ni moja hatuna wagunduzi wa vitu na teknolojia mbali mbali.Ndipo tatizo kuu lilipo.Swala sio siasa Wala Nini ulaya imetawaliwa na Hadi madikiteta akina Hitler lakini kwenye ugunduzi ilikuwa mbele Hitler akiwepo

China ilijifungia milango kabisa ikawa haiuzi chochote nje Wala kununua chochote nje (closed economy) lakini ilikuwa na wagunduzi kibao haikutetereka kiuchumi kwa kutouza nje.Ilipoglfungua milango ikawa bado kinara wa uchumi.

Nchi bila kuwa na wagunduzi hata uwe na siasa Safi vipi utakuwa lofa tu
Hahahah mkuu umeongea matakataka mkuu.
 
Siasa safi inatengeneza mazingira safi hivyo watu wataumiza kichwa lazima wapige hatua
 
Back
Top Bottom