cDNA
JF-Expert Member
- Nov 10, 2016
- 353
- 350
Habari zenu wana JF!
Nilikuwa na mwaliko wa dinner juzi kati, Sweden. Nikaoneshwa mti ambao wenyeji wangu wanasema ndio ulikuwa watumika kuwaadabisha watoto ktk generations za zamani. Ila kwa sasa ni marufuku kumpiga mtoto/mwanafunzi kwa namna yoyote ile, ukikiuka unapelekwa Segerea (kulupango). Wakasema baadhi ya nchi kama Uingereza adhabu ya bakora bado ipo mashuleni na hata wazazi kuwakanya watoto kwa kuwapiga vibao n.k. Wao wakasema wanapotembelea nchi za Ulaya kama Uingereza na kuona hivyo huwa miili yao inazizima!
Nikataka kujua zaidi namna wanavyowarekebisha watoto wao wanapokosea wakanambia ni kwa njia ya kumwambia mtoto ukiendelea hivyo (tabia mbaya) sitakununulia kitu fulani mfano gari, tablet, iPad n.k.
Mazungumzo yakanoga mpaka tukajikuta twazungumzia maswala ya uzazi.
Wakasema baadhi yao (waswidi) huamua kutokuzaa kabisa, wengine huamua mtoto 1 au 2 basi. Ktk jitihada za serikali kuwashajihisha wanandoa kuzaa ili kuongeza population imeweka sheria maalumu ya kuwalipa raia wake kulingana na watoto watakaowazaa (angalia Table hapo chini).
Nikasema huu motisha utakuwa hauwahusu waafrika waliopata uraia wa Sweden na kuishi nchini. Wakasema ni kwa raia yeyote bila kujali mwafrika au mzungu alimradi tu analipa kodi!
Table: Motisha wa kuzaa Sweden (1SEK=240 Tsh)
Wakasema pia ukifikisha watoto 5 serikali inakustopisha majukumu ya kazini kwa kuwa kuwalea hao watoto ni kibarua tosha bali unaendelea kupata mshahara wa kibaruani kwako jumlisha posho yako ya kila mwezi kulingana na watoto ulionao hadi watoto wafikishapo miaka 18.
Kumbuka elimu kwao ni bureee.
Wakasema pia ktk changamoto walizonazo wanandoa ambazo pia huchangia kutozaa watoto kadhaa ni pamoja na ndoa kuvunjika...ambapo takribani 50 % ya ndoa zote huisia kuvunjika.
Kumbe raisi JPM alikuwa sahihi aliposema fyatueni watoto...nitawasomesha.