FYA KUTOA HUDUMA KWA NJIA YA TEHAMA

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
618
1,000
1552047922263.png


SEKTA ya Afya inatarajiwa kuwa na mabadiliko makubwa ya kiteknolojia nchini na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutoa huduma kwa njia ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) huku ikiikinga jamii na maradhi mbalimbali.

Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Bakari Kambi alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia kongamano na maonesho ya awamu ya saba ya afya, sayansi na biashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashakiri (EAC).

Kongamano hilo ambalo ni la saba linaloandaliwa na Kamisheni ya Afya na Utati ya Afrika Mashariki linajumuisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, likitarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza nchini kuanzia Machi 27 hadi 29, mwaka huu na kufunguliwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan

Akizungumzia hilo, Profesa Kambi alisema teknolojia kwa ajili ya kubadili mifumo ya afya ili kutimiza Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Umoja Mataifa. “Tanzania imepokea jukumu la kuandaa kongamano hilo ambalo hufanyika kila baada ya miaka miwili, ikijikita kuonesha maisha ya kesho ya afya kujikita zaidi katika Tehama,” alisema Profesa Kambi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom