Fursa za wilaya ya Kishapu ni zipi?

neyfento

Senior Member
Mar 24, 2020
129
305
Nimepata ajira huko kutoka kwa taasisi fulani, naomba mnielezee fursa zilizopo ili nikatia kambi huko nipate namna ya kujiongezea kipato. Nawasilisha.
 
Mkuu hiyo wilaya iko shinyanga ni ngum sana kwanza jiandae kisaikolojia mazingira yake yanaweza kukusumbua mwanzoni.

Ni wilaya ambayo iko nyuma sana zaid sana, ukame wa hapo hata kilimo hakikubali,,, labda ukafungue duka la jumla na rejareja kama mtaji unao ili uwasogezee huduma karibu..
 
Asante ntapambana mdomdo.

Asante sana hii inantia nguvu sana, nimeshadhamiria kuweka kamb popote coz kungangania town ilhali huna cha kufanya hakuniingzii chochote. Acha nikapambane
Mungu akubarik, kukaa mjin wakat huingiz chochote haina maana yoyote na dunia hii hakuna anaeweza kukuthamin kama hauna chochote.. mm pia nlishafanya kaz hiyo wilaya miaka miwil iliyopita
 
Kwa sasa Kishapu wanakaribia kuvuna pamba.

sasa basi wale wasukuma wewe wanunulie viatu tu pale karume zile namba 8,9,10 na 11 kwa buku 5 tano kisha kauze huko. Hutojuta

Fursa nyingine sitakwambia maana na mimi nimetoka kariakoo jana tu kufuatilia mzigo. Ni hot sana.. ukipenda njoo pm tuyajenge..
(Faida ni mara 2 ya mtaji ukiwa mvumilivu)
 
Kishapu utakutana na watu wakarimu sana;
Ni i moja ya wilaya za mkoa wa shinyanga yenye ukame wa kutosha maji shda!! Ila just relax and chill utapapenda tu amani ipo ya kutosha kuhusu fursa utaamua cha kufanya ukifika; kwa miez hii wanakua wanavuna pamba, kwahy harusi Ni nyingi mnoo!!

Chukua zile nguo za spesho na viatu vya spesho ziwe za watoto,mwanaume na wanawake changanya mzigo nenda nao pale kishapu kuna mnada kila alhamisi nenda mnadani uhakika hutajuta kila la kheri mkuu kama unaswali zaid karibu Pm
 
Kwa sasa Kishapu wanakaribia kuvuna pamba.

sasa basi wale wasukuma wewe wanunulie viatu tu pale karume zile namba 8,9,10 na 11 kwa buku 5 tano kisha kauze huko. Hutojuta

Fursa nyingine sitakwambia maana na mimi nimetoka kariakoo jana tu kufuatilia mzigo. Ni hot sana.. ukipenda njoo pm tuyajenge..
(Faida ni mara 2 ya mtaji ukiwa mvumilivu)
Mkuu
 
Back
Top Bottom