safi sana ungewaelea pia raia njia rahis na salama ya kufika uko
Niliwahi Kupeleka TV kama mia hamsini hivi za mitumba basi jamaa waliiteka Boti na kula kichapo sana wakachukua zote na kuhamisha kwenye boti lao,nikabakia na Tv 20 tu ndio nikapata nauli ya kurudia.
Ni Kweli DRC biashara hizo na nyingine zinatoka sana,lakini usalama ndio tatizo.Utapeleka mara mbili basi ya tatu unaingizwa mtegoni
Niliwahi Kupeleka TV kama mia hamsini hivi za mitumba basi jamaa waliiteka Boti na kula kichapo sana wakachukua zote na kuhamisha kwenye boti lao,nikabakia na Tv 20 tu ndio nikapata nauli ya kurudia.
Ni Kweli DRC biashara hizo na nyingine zinatoka sana,lakini usalama ndio tatizo.Utapeleka mara mbili basi ya tatu unaingizwa mtegoni
Waungwana niko hapa DRC na leo nimeona ni vyema kushare fursa za kibiashara hapa.. Kwanza kabisa napenda kuwafahamisha kuwa kuwa Mtanzania hapa DRC hasa hapa Goma ni ujiko,, wacongo wanatupenda sana na wanadhani kuwa sisi ni watu waaminifu na wenye upendo na jasiri. kwa haraka haraka hizi ni bidhaa ambazo waweza uza bila kuwa na shaka
1. Khanga ,, akina mama wa ki congo wanapenda sana khanga ukileta utauza
2. Viatu vya kimasai... vyapendwa sana hapa... kwa wale wenye mitaji midogo hapa ni mahala pake
3. Nguo japo wameeanza kwenye China na Dubai , lakini bado wateja wa anguo jina la Tanzania linauza sana ( sijui kwa nini)
4. Mchele hakuna na kama upo si huu wa Tanzania wenye ladha.. na ukiupata bei haikamatiki wanakula akina fulani tu wengi wanjilia huu unaofanana na makande
5.maharagwe ya bukoba na kigoma utauza hapa
6. Alminium windows na door hakuna na ujenzi unaaza kwa kasi sana .. ukiwekeza utavuna pesa.. sijaona dirisha la alminum hapa.
7. Samaki na dagaa hasa wa mwanza -- waliwa sana hasa huko vijijini na Goma ndo soko kubwa
asante sana kwa leo n
Jaribu Na Muziki...........................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ndo suala nililomuuliza aeleze tu watu wachangamkie fursa Angalizo wale mnaopewa mchongo afu mnataka mtafuniwe kila kitu na mfikie kwa mtoa thread hua siwapendi na naomba ueleze pia lodge au hotel za Goma zinagharim kiasi gani?
safi sana ungewaelea pia raia njia rahis na salama ya kufika uko
Na lugha inayotumika sana Goma ni ipi? Na hujaeleza njia rahisi kufika Goma ni ipi kama ni ile ya kupitia Ngara then Rwanda hadi gisenyi ndo uingie Goma au ile ya kupitia Burundi upande tex hadi Uvilla then uchukue boti hadi Goma ? Na terms za kufika hasa VISA ni shilingi ngapi? Na maisha yakoje exchange Rate kwa pesa ya Tanzania ikoje?
Niliwahi kuku PM juu ya dhahabu per gram ikoje na upatikanaji wake ukoje? Haukuwahi kunijibu zaidi ulikaa kimya tu.
Dhahabu sikushauri ... ziko sana hasa kwa waasi ilawanakuuzia then wanawatonya washikaji wanakuja kuzichukua baadae.. na ujue pia kwa rwanda ukikamatwa 20 years jela unless upitia serekarini ambako sina ujuzi nako.. wapigaji wanatoka lakini ni risk sana.. si dhahabu hata alimasi na mawe menigine GOMA ndo kwao...
haukunielewa hakuna aliyesema afikie kwako ndugu, Kenya Airways walikua na route ya Nairobi To Goma hvo nadhani kama umenunua mzigo unawezapitia Nairobi then ukaanza safari nyingine btw asante kwa maelezo yako.