Fursa nzuri sana kwa wafanya biashara.....Ingekua na muendeleza katika nchi zenye fursa zaidi nakubwa kuliko comoro yenye idadi ndogo ya watu uchumi mdogo tuekeeni bussiness trip nchi kama Sweden UAE nkHuenda unafanya biashara na raia wa Comoro au ulijaribu ila ukakutana na changamoto za hapa na pale. Au pengine ulikuwa unatamani kufanya biashara aidha kuuza au kununua bidhaa kutoka Comoro. Kuwa na amani, suluhisho limepatikana. )
Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro na ubalozi wa Comoro nchini Tanzania wakishirikiana na UCCIA na Coso Marketing & PR solution LTD wanakuletea FURSA wewe mfanya biashara.
Ni Fulsa ya kuweza kufanya biashara nchini Comoro.
UTAKUTANISHWA na wafanya biashara wakubwa , wadogo , na wa kati wa kuaminika kabisa wa nchi ya Comoro.
Hii ni USO kwa USO, tunatoka Tanzania, tunafunga safari hadi Comoro.
Note : KABLA YA SIKU YA SAFARI KUTAKUWA NA SEMINA MAALUM KWA WAFANYA BIASHARA ITAKAYOFANYIKA KWENYE UBALOZI WA COMORO.
Usikubali kupitwa na hii.
TANUA WIGO wa BIASHARA YAKO.
Kwa mawasiliano
Contact :
0684771367
Email :
coso@communicationsolution.co.tzView attachment 1107977
Tofauti ipo hata kiuandishi[emoji1787] (Jokes dear).Mi huwa napata shida sana kuweka tofauti kati ya Comoro na Morroco
BTW all the best kwa watakaoparticipate
Asante rafiki..Tofauti ipo hata kiuandishi[emoji1787] (Jokes dear).
Morroco ipo kaskazini mwa bara la Afrika wakati Comoro ipo kusini mashariki mwa Afrika.
aggyjay kwa kukusaidia unaweza kuondoa neno Comoro na ukaweka neno Ngazija na utakuwa hujakosea Wakomoro aka wangazija ni wenzetu sana hao
Ooh asante mkuu..halafu hicho kingine ndo waarabu?
Hapana, sio waarabu kwa mambo mengi kiutamaduni wacomoro aka Wangazija wamefanana sana na wazanzibari, waliwahi kutawaliwa na wafaransa na ndio maana idadi kubwa ya wacomoro wapo ufaransa na wengi wanaongea kifaransa.
Sawa.naulizia hicho kingine(morroco)
Ndo wana asili ya uarabu?
Mweee[emoji2297] itabidi nitumie bakora sasa, watu wengi wa Moroco wana asili ya Arab wakati Comoro ni Washiraz (Nadhani ndo hao wangazija kama mdau mmoja alivyosema hapo juu)Asante rafiki..
Ila bado kabisa hujanibadilisha hahahaa
Hao wengine (Morocco) ni waarabu si unamkumbuka Mfalme Mohammed VI na mke wake Pricess Lalla Salma walivyokuja Tz? hao ni waarabu ingawa hawamo katika Jumuiya ya nchi za kiarabu GCC
Mweee[emoji2297] itabidi nitumie bakora sasa, watu wengi wa Moroco wana asili ya Arab wakati Comoro ni Washiraz (Nadhani ndo hao wangazija kama mdau mmoja alivyosema hapo juu)
Ramani hiyoMi huwa napata shida sana kuweka tofauti kati ya Comoro na Morroco
BTW all the best kwa watakaoparticipate
Vipi mtu kupata passport ya kule na kuingia ulaya ni kazi?na kwa kuongezea tu biashara ya comores ina msimu kuanzia jun july na august kwa sababu ni holiday ya wale wanaokaa ulaya huja comores kufanya maharusi yao ya mila zao hapo panakua na biashara nzuri sana hususan kwa biashara ya chakula kama vinywaji biscuit sukari ungangano basmati rice tomato paste , nazi ya unga, kanga za sare, mafuta ya kupikia , majani ya chai, hiliki, mdalasini, uzile , nk