Wana Jamii, jana nilitembelea banda la Tanzania Investment Bank katika maonyesho ya Nane Nane hapa Dodoma na nikakutana na watengenezaji wa boat za kisasa za uvuvi (SONGORO MARINE BOAT YARD) ambao wanapatikana Mjini Mwanza.
https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=60973&stc=1
https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=60974&stc=1
Hawa jamaa wamefanya makubaliano na benki ya TIB kwamba mvuvi (mfanyabiashara) anaweza kupata boat ya uvuvi kutoka kwao kwa mkopo ambapo mvuvi atatakiwa kulipia asilimia 20% ya gharama na benki watamlipia asilimia 80% iliyobaki kwa mkopo. Boat inaweza kugharimu kiasi cha Tsh. 68,000,000/= inategemea na ukubwa, hivyo basi mvuvi au mfanyabiashara anatakiwa kulipa kiasi cha Tsh. 12,000,000/= na kiasi kinachobaki kulipwa na benki; dhamana itakuwa ni hiyo boat (hakuna dhamana nyingine).
Huyu jamaa wa kutengeneza hizi boat aliyekuwa ananipa maelezo alisema kwamba kwa biashara ya uvuvi ndani ya mwaka mmoja utakuwa umerudisha pesa yako, kama kuna mwanajamii ambaye anafanya biashara ya uvuvi anaweza kutusaidia huu upembuzi yakinifu juu ya hiyo return.
duh! mil 68?
Bei za kujenga meli kwa kweli si mchezo, lakini milioni sitini na nane kwa mtumbwi huu...dah! labda waje wataalam!
Lakini kwa vile ni mkopo (wa muda mrefu) ni fursa jamani mnaofanya uvuvi changamkieni deal hilo, dhamana si mtumbwi wenyewe, isipokulipa wanachukua chao hauna hasara!
View attachment 173941
kununua nje na kulisafirisha nako tabu tu..dah!
hahaha mkuu umesema la maana sanasidhni kama kuna wavuvi walio wengi wanaoweza kuweza bei ya hiki kifaa!
kama kweli serikali iko serious bwana iachane na kufukazana na mwenge itoe sponsorship kwa vitu vya msingi kama hivi watu wapate ajira!
TU NA FANYA MA ZUNGUMZO NA MADHMNA WA SEREKLI ILI KWA HARKA TUJE KUTENGENEZA MA BOTI HUKO TANZANIA
gombessamsa@gmail.com
kobali556@gmail.com
duh! mil 68?
umechangia vizuri ila umeharibu kwa hao ulio wa cc zitto,malecele na mdee wao ni nani katika nchi hii hawana mamlaka wala madaraka wala maamuzi yoyote ni vidampa tusidhni kama kuna wavuvi walio wengi wanaoweza kuweza bei ya hiki kifaa!
kama kweli serikali iko serious bwana iachane na kufukuzana na mwenge itoe sponsorship kwa vitu vya msingi kama hivi watu wapate ajira!
cc Zitto kabwe W. J. Malecela, Halima Mdee, angalieni hili kwa maslahi ya taifa.