Fursa katika ulimbwende - Miss Kinondoni 2024

Nov 6, 2016
65
166
FURSA KATIKA TASNIA YA UREMBO NA ULIMBWENDE

Na Comrade Ally Maftah

20/ Jan 2024. Harakati za Comrade Ally Maftah na Mwl Rashida Kayera ziliifikisha CAM STORE katika ufunguzi wa mashindano ya ulimbwende ya MISS KINONDONI ( UREMBO NA UONGOZI ) yaliyoandaliwa na Rafiki yangu Queen Johnson, mlimbwende mwenye makampuni na taasisi lukiki zilizotoa fursa za ajira na ufahamu katika Jamuhuli ya Muungano akimuunga mkono Dr Samia Suluhu Hasani ( Mama Kizimkazi ) mchumi mkuu wa taifa, mfariji wa Taifa MAMA WA TAIFA.

Hakuna mashaka kwamba tasnia ya ulimbwende imetuletea viongozi lukuki katika taifa akiwemo Jokate, na wengine wengi, imeleta hamasa kubwa kwenye ujenzi wa taasisi zisizo za kiserikari na makampuni ya kibiashara, walimbwende wamekuwa mstari wa mbele kwenye ujenzi wa Taifa letu kiuchumi na ki ustawi wa Jamii.

Mis Kinondoni wamekuwa vinara katika mashindano mbalimbali ya ulimbwende ya Tanzania na Dunia, Kinondoni tuna kila sababu ya kujivunia.

2004 Faraja Kota, 2005 Nancy Sumari, 2006 Wema Sepetu, 2007 Ritcha Avia, 2012 Fridgit Afrey, 2016 Diana, 2018 Queen Elizabert.

Hao ni baadhi ya walimbwende wa Kinondoni waliofanya vizuri kwenye Tasnia hii.

Wito wangu, Tumuunge mkono Queen Peter Johson kwa kumpa ushirikiano wa hali na mali, mwenye kuhitaji taarifa zozote kuhusu Miss Kinondoni akinikaribia nitamuunganisha na waandazi

Vijana wetu wa Chama cha Mapinduzi wa Kinondoni chukueni Fursa mbalimbali za mashindano haya, najua ndani ya chama tuna walimwende wengi sana twendeni sasa.

#ulimbwendesiihuni
#harakatizacomradeallymaftah

Imeandikwa na
Comrade Ally Maftah
-Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam
-Mjumbe Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam
-Mdau na Mwanachama wa BASATA
-Mwandishi wa Mashairi na Mwimbaji
-Mwandishi wa Vitabu - Mwanachama wa Maktaba ya Taifa
-Mkufunzi wa Ujasiliamali
Mwanzilishi wa CAM STORE


 
Inafikirisha Sana "Jamuhuli"
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…