Funzo: Nimepitia(nimeishi maisha magumu sana)

mjasiliaupeo

JF-Expert Member
Apr 21, 2013
2,162
3,088
Habari wana Jamii,

Kwa kupitia nyuzi mbali mbali nilizosoma wiki hii nimegundua kuwa vijana wengi hawajiwezi kimaisha, maisha yamekuwa magumu mpaka hawaioni kabisa thamani yao kama vijana na wanaamini kuwa kwa jitihada ambazo tayari wameshazifanya hazijaleta mrejesho chanya, na hawana tumaini la kuongeza jitihada zaidi wala hawana tumaini la kufanikiwa, kwa rugha nyingine waweza sema kuwa hawaiamini kesho yao. ndio maana nimeamua kutumia muda wangu ili kuandika ushuhuda wa kuwatia moyo vijana wenzangu, siamini na wala simaanishi kuwa nina maisha mazuri ambayo hawa vijana hawana, rahasha ila nahitaji kuwapa moyo ili waweke tumaini kwenye kesho yao.

Mimi ni kijana, kwa sasa nina miaka 25, nilizaliwa Mbeya/kyela kabla ya kuamia Dar mwaka 1996 nikiwa na wazazi wangu, baba yangu alikuwa ni mtu mwenye uwezo wa kati, alikuwa ni "injinia" wa balabala na mama yangu alikuwa ni mama wa nyumbani, hivyo tuliishi maisha ya wastani kwa kipindi hicho tuliweza kumiliki nyumba kadhaa pamoja na gari moja la mzee aina ya "one ten". lakini kufika 1998 baba yangu alifariki kwa ajari, hili lilikuwa pigo kwa familia kwa ujumla na tulisafiri mpaka mbeya ili kwenda kuzika na tulizika na kukaa mwezi mmoja kwa ajili ya matanga. Tulipo rudi Dar es salaam ndipo tukakuta kila kitu kimehalibika, ndugu, wadogo wa mama pamoja na baba walishilikiana kuuza mali zote za dar, kitu walichoshindwa kuuza ni nyumba moja tuliyokuwa tunaishi ni kwa sababu mjumbe aligoma kuweka saini kutokana na mazingira aliyashtukia japo walifanikiwa kuuza thamani zote na vitu vinavyobebeka.

Ni kwa mala ya kwanza nilianza kukijua kitu kinachoitwa shida, nililazimika kuamka asubuhi na kuuza mchicha na ikifika saa nne ndio naenda shule, najua inaonekana ni kawaida sana lakini kwa mtu ambaye ameishi maisha ya kiwango cha wastani alafu akaangukia kiwango hiki cha maisha kunakuwa na manung'uniko makubwa kwenye moyo wako, nilikuwa najificha nikiona " school bus" ambayo nilikuwa napanda kwenda shule kwa kuogopa fedheha ya marafiki zangu niliosoma nao kabla ya kuhamia shule ya serikali. Mama yangu alinisisitiza nisome sana, aliamini na aliniaminisha kuwa bila elimu ni kazi bure, na aliniaminisha kuwa hakuna mafanikio bila elimu hivyo nilijitahidi sana kusoma japo sikuwa na kipaji cha akili lakini niliweka juhudi katika elimu kadli nilivyoweza. Nakumbuka mtihani wa mwisho kidato cha nne sikuweza kupata credit, niliumia sana, nilijua ndio mwisho wa ndoto yangu ya kusoma, sijujiona na thamani tena, nilishuhudia wenzangu ambao hawakuweka juhudi sana kama zangu wakipata alama nzuri, kwa mala ya kwanza nilijifikilia kujiua nilikuwa nina miaka 17, nilienda kumwambia mama kuwa nimeshindwa kupata alama zitazofanya niendelee, na yeye alijifungia chumbani na kuanza kulia, kuna kauli moja aliitoa wakati analia ndiyo iliniongezea motisha ya kutaka kujiua "mungu nimekukosea nini mimi?" kitu ambacho kilinichelewesha ni ile hali ya kufikilia kuwa mama yangu atabaki na hali gani, ataweza kuishi bila mimi? maana kila muda aliniona na alinitambulisha kama mimi ndio tumaini pekee alilobaki nalo. nilijaribu kuuvaa uchungu wake kama mama ambaye amempoteza mtoto aliyempenda na kumpigania sana, niliuona uchungu wake ni mkubwa kuzidi majuto yangu, niaghaili kujiua rasmi.

Nikapata mdhamini wa kunisomesha, nilifanikiwa kujiunga chuo cha elimu ya biashara posta, katika fani ya teknologia ya habari na mawasiliano, ninashukuru Mungu kuwa alikuwa mwaminifu na nilifanikiwa kumaliza chuo ngazi ya stashahada mwaka 2013.

Katika harakati za kutafuta ajira ndipo hapo nilikutana na mambo ya kuvunja moyo na kukatisha tamaa kama hawa vijana wenzangu wanavyopitia hii hatua, kwa kweli wenzangu wengi wamekuwa walevi, wamechanganywa sana na hali wanayokutana nayo mtaani baada ya kumaliza vyuo. nilisota mpaka 2015 mwanzoni bila mafanikio yoyote, kuna muda ninakosa hata nauli ya kupeleka barua za maombi ya kazi au kuwahi usahili, najua ni wengi wamepitia hatua hii.

SASA INABIDI TUJIFUNZE KITU HAPA;
Tokea nianze kusikia kesi za watu kuumizwa na suala la maisha ni kesi chache sana kumsikia mtu ambaye hana elimu kabisa akafikia hatua ya kujiondoa uhai kutokana na ugumu wa maisha, kesi nyingi sana ni za wasomi ambao wamekosa au wamefukuzwa kazi.

NIKAGUNDUA TATIZO;
Tatizo ni kwamba, watu waliokosa fulsa ya elimu mazingira yanawabeba kuliko waliopata hiyo elimu, mtu aliyokosa elimu ana wigo mpana wa kuendelea kufanya kazi ndogo ndogo wakati watu walioelimika wamefungwa katika minyororo ya taaluma zao, JARIBU HII; Mtafute huyo kijana ambaye amegraduate TEHAMA anayelalamikia ugumu wa maisha alafu mwambie kuna kazi ya kuuza duka hapa, angalia muitikio wake, elimu zetu zimetufunga minyororo bila wenyewe kujijua, aliyesomea shelia anasubili mahakama ziteme, walimu pia wanasubili tamisemi wateme, madocta wanasubili muhimbili wateme, hili ndilo jipu ambalo hatujawahi kuliongelea na ni kubwa sana.

NILICHOKIFANYA MIMI ILI KUJIKOMBOA NA USHAULI KWA VIJANA WENZANGU.
Niliamua kufanya uchunguzi, ni kitu gani kinaweza kunitoa ukiachana na taaluma niliyokuwa nayo, niliamua kuwa fundi rangi, nilitumia muda mfupi sana kujifunza masuala ya kupaka rangi majumbani, niligundua kuwa ukiwa na elimu hata kama utaamua kuwa dalalali watu watakuamini, watu bado wanaheshimu sana elimu, elimu sio kitu cha kubeza, ndio maana hatachezaji akiwa na elimu anapewa hata unahodha, fanya chochotw kile elimu itakupa back up, sio lazima uwe engeneer, dokta sijui mwanashelia, jambo kubwa ni kuwa unapoenda kwa client wako ongea, fanya reasoning za kisomi ili akutofautishe na hawa wa mtaani, nimepata respect kwenye field yangu nina back up ya vijana zaidi ya kumi and i am thir boss, na nyumba zinajengwa kila siku na kila siku naingiza kazi, tunafanya marketing nyumba hadi nyumba tunatuma project zetu kwa maboss thru emails zikikubali naenda kusign pesa, sifikilii tena TEHAMA hii ufundi imenifanya nipange nyumba ya 300,000/= at my age na kila siku niko busy kwenye mtandao kuangalia design nnzuri zinazo trend uko Arabs an europe ili nionekane tofauti na wa mtaani. Guys kuna muda nasoma malalamiko ya watu then ninajiuliza wamekosa kabisa kazi ya kufanya au wamekosa kazi wanazozipenda wao?

MUHIMU;
Tafuta njia yoyote, taaluma yoyote ya mtaani, jifunze then tumia elimu yako kujitofautisha alafu ukija hapa jf jitangaze fungua page insta jitangaze alafu subili feedback. mimi nilianza hii kazi nikiwa na nia na sasa nafanya hii kazi to the next level unaweza kuona kazi zangu thru instagram @finaltouch_painting_pro au nichek whatsap #0713553387 nitakutumia.

Mwisho kabisa, mimi ni fundi rangi #ThePaintToTheNextLevel kwa mahitaji ya #Skimming na #Painting ni pm au nicheki kwa hiyo namba.

Asanteni.
 
Mi nilimaliza chuo degree mwk 2013 nikatafuta kazi mwezi 1 mwaka 2014 nikaona najichosha nikajiingiza kwenye biashara ya kwenda minadani kununua kuku wa kienyeji na kusupply kwenye mabar na hotelini arusha hawatumii kuku wa kisasa mtaji ukakuwa haswa.

Baadae nikapata wazo la kwenda iringa kutafuta kazi nikiwa kule nikapata fursa ya kuchukua mkaa kwa gari kuja kuuza Dar kwa jumla, baadae nikafungua store Dar baada ya mvua kukata mamikaa yakawa mengi mjini hapa.

Naendelea vizuri nimenunua viwanja viwili, nimejenga self safi, nimenunua gari ya kutembelea, namilikI hisa TBL.

Sifikirii tena kuajiriwa nasonga mbele kwa mbele.
 
Mi nilimaliza chuo degree mwk 2013 nikatafuta kazi mwz 1 mwk 2014 nikaona najichosha nikajiingiza kwenye biashara ya kwenda minadani kununua kuku wa kienyeji na kusupply kwenye mabar na hotelini arusha hawatumii kuku wa kisasa mtaji ukakuwa haswa

Baadae nikapata wazo la kwenda iringa kutafuta kazi nikiwa kule nikapata fursa ya kuchukua mkaa kwa gari kuja kuuza dar kwa jumla, baadae nikafungua store dar baada ya mvua kukata mamikaa yakawa mengi mjini hapa.

Naendelea vzr nimenunua viwanja viwili, nimejenga self safi, nimenunua gari ya kutembelea, namilikI hisa tbl.

Sifikirii tena kuajiriwa nasonga mbele kwa mbele
hongera sana mkuu, kuna jambo la kujifunza hapa.
 
Dah, mmenifanya nijitathmin upya wazee japo sio kila mtu akifuata njia yenu atafanikiwa, binafsi nilikuwa sipendi kabisa kuajiriwa nikapata mtaji wangu, kunabiashara nikaianza, nilikula hasara vibaya sana na nikarudi zero kabisa, hatimae nimeanza kuapply kazi tena kwa fujo, kiukweli malengo yangu yapo pale pale kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa japo kwa sasa mtaji ni changamoto. Hongereni sana wakuu na wengine wote waliojiajiri na wakatoboa, tulioshindwa tusikate tamaa, tukomae
 
Mawazo mazuri sana haya na yatasaidia sana kupunguza tatizo la ajira ktk nchi yetu yenye kila aina ya fursa lakini imeendea kuwa na job seekers wengi kuliko job creators kama nyinyi! Big up sana.
 
Well said., unajua ukikutana na story kama hizi zinajenga sana tofauti na za kila siku watu wanalalamika tuu kwenye mitandao maisha Magumu
Nawapongeza sana Vijana wenzangu kama tutakuwa wakweli kila atakae pita hapa itamjenga.
Nawatakia kila la here katika ujasiriamali
 
Yaani kuna watu kujiajiri wanaona kama laana vile hii yote ni uvivu wa fikra na wizi wa muda sababu anaamini akiajiriwa hawezi kuwa committed na kazi yake yeye kusubiri mwisho wa mwezi tofauti na kujiajiri inabidi kichwa kiwe cha moto.Hii elimu ya ujasiria mali bado haijatuingia kisawasawa ila kwa ushuhuda kama huu inatia moyo kwa vijana hongera.
 
'kipaji cha elimu' kama ulivyokiita kweli hauna kama maandishi yako yanavyoakisi uhalisia...LAKINI...Hiyo spirit uliyonayo ni ya thamani ya juu kweli...
wazazi pia mjifunze, maneno yenu kwa wana wenu pindi wanapofeli yawe ya kujenga..maana ukimponda mjinga yeye, hana akili yeye n.k, haimsaidii kitu chochote. Mpe moyo..msaidie awekeze kwenye vipawa vyake.
 
kaka hongera sana,mimi ni mtumishi wa umma lakin kazi ninayo fanya sina furaha nayo hata kidogo,ndoto yangu kubwa ni kuwa mfanyabiashara tu.nawaza biashara muda wote,umenipa nguvu ya kutenda,stay blessed
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom