Waislamu tumeingia mwezi 9 dhul hijja ni siku iliyotiliwa mkazo sana kufunga kwa aliekua hajaenda hijja
Funga ya kesho ukiifunga na kukubaliwa basi Mja husamehewa madhambi ya mwaka ulopita na ujao unakosaje fursa hii ewe muislamu?
Ndugu zangu wapendwa, kesho ni siku tukufu ya Arafa siku yenye rehema, maghfira na kujibiwa dua. Tusiiache ipite kama siku ya kawaida.tuzidisheni
kumtaja Allah (dhikr), kuomba msamaha (istighfar), kumswalia Mtume ﷺ,
na kuomba dua kwa ajili yetuu, familia zetu na Ummah mzima.
Siku ya Arafa ni miongoni mwa siku bora zaidi za dua. Tumnyenyekee Mola wetu, kwani huenda dua ya siku hiyo ikawa sababu ya kufunguliwa kheri zetu kuondolewa huzuni zetu, au kusamehewa madhambi yetu.
Usiseme sina la kuomba… mwombe Allah kila kilichomo moyoni mwako.
Hakuna dua ndogo mbele ya Allah, na hakuna jambo gumu kwake.