Fundi Samweli na kisa chake cha 'ufundi'

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,318
Samuel Lundström 'Fundi Samweli' ni mtayarishaji wa Muziki kutoka nchini Sweden ambaye kwa miaka kadhaa amekuwa akifanya kazi hapa nchini, Project ya Muziki iliyofahamika kama Sauti za Afrika, kabla yake kuondoka mwaka 2012.

Tayari Fundi amerejea nchini na baadhi ya kazi zake mpya zimeanza kuruka hewani. Yangu si hayo, yangu yanahusu kisa cha yeye kuitwa 'Fundi'.

Akizungumza kwenye kipindi kimoja cha televisheni miaka ya nyuma, mwenyewe alisema kuwa alilipata jina hilo siku moja alipokuwa Bagamoyo kwa shughuli za muziki.

Matata yalianza baada ya kiatu cha Fundi kukatika, wakati huo akitumia majina yake ya Kiserikali, ndipo jamaa Mbongo waliyekuwa nae kwenye ziara hiyo akamwambia kuwa yupo mtu anaweza kutengeneza na kiatu kikafaa tena kwa matumizi.

Wakaenda kwa mshona viatu, kiatu kikatengenezwa na kikafaa tena na akakivaa.

Kwa mshangao Samweli akauliza jina la yule aliyetengeneza kiatu (ujuzi ambao hakuwahi kukutana nao), akajibiwa kwa ufupi, "Fundi!", naye akasema kuwa kuanzia siku hiyo na yeye ni 'Fundi' wa Muziki, na jina Fundi Samweli likazaliwa.

Licha ya utayarishaji, Fundi Samweli pia ni mwimbaji, anafanya kazi ya Bendi ya Veonity ya Sweden na ameimba nyimbo kadhaa ka kushirikiana na wasanii wa Tanzania kama Niki wa II, Joh Makini, Linex na wengineo...

Wimbo wake wa karibuni ni Nikumbatie, alioshirikishwa na Joh Makini, msanii wa Bongo Fleva kutoka Jijini Arusha.
 
Kuna mambo Mengi ya kujadili: hebu angalia jamii inayokuzunguka inakabiriwa na tatizo gani halafu lilete hapa tujadili!!
 
Kuna mambo Mengi ya kujadili: hebu angalia jamii inayokuzunguka inakabiriwa na tatizo gani halafu lilete hapa tujadili!!
Nimeangalia na nimeona moja, watu hawajui kwanini Samuel Lunderstom anaitwa Fundi Samweli. Nimeamua kulishughulikia, au wewe ulikuwa unajua?
 
Back
Top Bottom