Medecin
JF-Expert Member
- Nov 29, 2011
- 8,221
- 22,431
afrika ni ndugu alisema hata nyerere na mandela. kwa kuwa sisi watanzania tuna rasilimali nyingi sana ila viongozi wetu hawajui jinsi ya kutunufaisha watanzania nashauri baadhi ya rasilimali tuwaachie wenzetu ili tuone kama watazichezea kama sisi. hili ziwa nyasa tuwaachie malawi na kenya tuwaongezee kipande cha ziwa victoria na kwa kuwa congo ni kubwa kuliko tz basi tuwaongezee eneo la ziwa tanganyika na kwa kuwa mlima mlima kilimanjaro unaonekana vizuri zaidi kenya basi bora tuwape tu ili kukuza uhusuano wa jumuiya yetu ya afrika mashariki. na kile kilichosababisha kupigana na uganda mwaka 1978 nacho tuwape wachukue hilo eneo. na zanzibar tuwape uhuru wao waungane na kisiwa na mafia waunde nchi yao na mpaka wa znz na tz uwe feri kivukoni. na mkwa kumalizia kwa kuwa rwanda na burundi ni ndogo kieneo basi mkoa wa kagera tuwape wagawane wananchi tutawahamishia mbuga wa mikumi ili wasipate tabu ya kuwinda. nimesikia kuwa ikulu itakuwa dodoma basi ni vyema majengo ya ikulu ya dsm iwe hostel ya wahamiaji haramu kutoka ethiopia ili wapumzike wakisubiri kuendelea na safari ya kuelekea south.
fumbo la uzalendo,tukishindwa kuvitumia tuwape wenzetu uchoyo sio desturi yetu
pamoja na rasilimali zote ni aibu kuendelea kuwa masikini tukishindana kukomoa wapinzani,kutetea vyeti vya bashite na nani mkali wa shilawadu.
Kama mtafuata ushauri wa Sizonje wa kufyatua tu basi endeleeni ila ushauri wangu ni bora kupunguza kuzaa ili kupunguza idadi wa watakaotulaumu miaka 50 ijayo kwa kuchagua elimu bure mpaka darasa la 12 na kukataa elimu bure mpaka vyuo vikuu.
Mwisho msinipangie cha kupost kwa sababu nilivyoenda kununua vocha dukani sikwenda na nyie na hela ya bando hamkunichangia tena mkinipangia ndo mnaharibu kabisa.
Jembekillo
Paka Mweusi Gizani