Habari JF
Maisha ukiyatafakari unaweza shikwa na mfadhaiko daima.
Liko jambo kila nikilitafakari mwisho wake huniachia maswali mengi.
Jambo hilo ni UKWELI
Nenda kaskazini, magharibi au rudi Kusini na kaskazini, utasikia watu wengi wakionesha kuupenda ukweli.
Ila unapoingia kwenye maisha ya kawaida ni wachache sana wanaouish ukweli kwa vitendo.
Ukienda makazini, mtu mkweli upendwa kwenye vikao kwa maneno ila akijaribu kuutenda ukweli, mfano akijaribu kuzuia dili za watu, au akifichua maovu, hakika ujikuta ktk vita kali sana na wakubwa. Wengi wamefukuzwa kazi, wameshushwa vyeo, wamehamishwa ofisi n.k kwa kuwa tu wakweli.
Nenda kwenye biashara, huku ndo usiseme, asilimia kubwa ya shughuli za kibiashara zimejaa kona na magendo sana. Ukifungua biashara ukataka kuifanya kwa mstari ulionyoooka, usishangae ukakata mtaji, kuja kushituka wenzako kumbe wanapiga dili na kukwepa kodi, then sokoni hatoweza kushindana nao.
Kwa upande mwingine utakuta sheria zinaharamisha biashara nyingi, na kama nchi mnasema hii haikubaliki, ila cha ajabu watu ndo uzifanya shughuli hizo. Chukua mifano ya pombe haramu, bangi na madawa mengine ya kulevya, ukahaba n.k......sasa rudi kwenye maisha ya kawaida utashangaa wakazi wengi wa mijini na vijijini hizo ndo kazi zinazo waweka mjini.
Rudi kwenye siasa, kiongozi mkweli huwa kipenzi cha watu majukwaani, ila maisha yake yamejaa giza na mipango ya kuangamizwa, atapangiwa mipango ya kufukuzwa, kuzibiwa fursa na hata njama za kushambuliwa na kuuawa.
Ktk hili mifano ni mingi zitoeleza zaidi.
Rudi kwenye familia zetu, mtu mkweli anayezuia uvivu, ukosefu wa maadili na kutaka watu wawe wawajibikaji na kujitegemea, ghafla hujikuta ndo mtu atakaye lahumiwa sana na kuitwa mwenye roho mbaya.
Kuna jamaa, aliwahi kukata mawasiliano na kuwawekea vikwazo vya kiuchumi Ndg zake baada ya kusimamia kuwa hayuko tayari kuona dada zake, wajomba zake waliokuwa wanaishi na wazazi wake, wanazalishwa na mijanaume kisha mimba na watoto wao wanaletwa kulelewa kwa babu na bibi( ambao ni wazazi wa jamaa). Alichoambulia ni kushutumiwa sana.
Tatizo liko wapi:
Mbona watu uupenda ukweli lakini hawataki kuuishi?
Watasifu kwa maneno ila kimatendo ufanya kinyume?
Je kweli na haki ni dhana za kufikirika tu?
Karibuni wana JF kushare uzoefu.