Fujo mechi ya simba na kagera sugar polisi washitakiwe

Fujo mechi ya simba na kagera sugar polisi washitakiwe

LEGE

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2011
Posts
5,122
Reaction score
9,223
kiukweli mimi nishabiki na mpenzi wa mpira wa miguu.ila kwakilichotokea kwenye mechi ya simba na kagera sugar nikitendo cha kipuuzi sana na kama ni mwanamichezo mpenda naendeleo huna budi kulaani kwa nguvu zote hata kama wewe ni mpenzi wa SIMBA.
je mwajua garama ya viti mlivyo haribu? je wewe ni nani na unahisa kiasi gani na tim ya simba mpaka mlipo fungwa ndio mharibu viti?i
kumbukeni huu uwanja sio mali yenu nyie mnaojiita wapinzani wa jadi kwani ni mali ya watanzania wote umejengwa kutokana na kodi zetu.

mwisho nawalaum sana polisi na wanausalama wote walio kuapo uwanjani sina uhakika ila naimani huwa wanapewa chochote iwe wao binafsi au mabosi wao huwa wanapokea chochote kuhusiana na ulinzi.
inakuwaje wao wanalinda usalama wa raia na mali za uwanjani kwa kujazana kama viazi au nyanya kwenye tenaga?

inamaana huwa hawaoni polisi wa wenzetu huwa wanajipanga tena kwa kuwaangalia mashabiki na sio kutazama ana mpira na tena huwa wanatawanyika uwanja mzima?

ukiangalia vizuri clip ya zile fujo utagundua kua ni mashabiki tena wendawazim wachache sana ndio waliokuwa wanafanya zile fujo tena nikipande kidogo sana cha mashabiki na sio jukwaa zima hivyo ilikuwa ni rahisi sana kuwazuia kama wangekuwa wanatawanyika uwanja mzima na ikiwezekana na kukaa kule kule majukwaani na hao mashabiki inakuwa raisi kuzuia fujo?
kuliko wao wanavyojazana upande 1 na fujo zikianza upande wa 2 basi nilazima wafanye safari mpaka upande mwingine??

TAFADHARI huu uwanja sio mali ya simba au yanga au azam fc ni mali ya watanzania wote so kidogo kidogo mwishowe tutabakia na pango/gofu.

USHAURI mm ningeomba waliofanya fujo watafute na wawajibishwe kwa kulipa garama za uharibifu uliotokea ikiwa pamoja na kuwafutia uwanachama wa klub husika na kuwafungia kuto ingia uwanja wa taifa .ikiambatana na adhabu kali kwa tim husika ambayo mashabiki wake walio leta fujo.na nilazima tim husika ambayo mashabiki watafanya fujo na kusababisha hasara tim ilipe hasara husika bila huruma
 
Wale ni washamba tuu,wamesahau kuwa michezo ni urafiki.Simba walipe gharama za uhalibifu uliotokea
 
Huo mfano unaoutoa wa polisi wa nje kutoshughulikia mpira kabisa ni sawa. Lakini umepeleleza wanakuwa wangapi kwa kila mita moja? Polisi wetu wakiingia kwa idadi hiyo, si ndio mgao wavilabu utapozidi kupungua? Wewe na vilabu unavyovishabikia hamtolalamika?
 
Back
Top Bottom