FT: Simba Sc 1-0 Stade Malien | CAF CL | Februari 14, 2025 | Benjamin William Mkapa Stadium| Saa 1:00 usiku

FT: Simba Sc 1-0 Stade Malien | CAF CL | Februari 14, 2025 | Benjamin William Mkapa Stadium| Saa 1:00 usiku

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Hii hapa mechi ya kukamilisha ratiba kwa Simba SC dhidi ya Stade Malien kutoka Mali, ambao tayari wameshafuzu hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAFCL) katika Kundi D.

Kwa Simba, huu ni mchezo wa heshima, kwani ushindi utawafanya wafikishe alama 5 badala ya 2 walizonazo sasa, ingawa tayari wameshathibitisha kumaliza katika nafasi ya mwisho ya kundi hilo.

NB: Simba haijafanikiwa kushinda mchezo wowote katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2025/2026.

Petro Atletico De Luanda na Esperance De Tunis timu itakayopata ushindi itasonga mbele kuungana na Stade Malien katika hatua inayofuata ya michuano hiyo.
IMG_0084.jpeg
IMG_0085.jpeg
 
Leo Mnyama anaunguruma kama kawaida. Simba oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
 
DAKIKA 15'
Mnyama leo anatambaza soka la kikubwa na hadi sasa inaongoza

SSC 1 - 0 SML
A. Oura 4'
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Dakika 20'

Koulibaly anamimia krosi ktk goli la Simba lakini Simba wanaondosha hatari

SSC 1 - 0 SML
 
Dakika 22'

Kocha Barker mSouth wa SSC hadi sasa anatabasamu hali ilivyo hadi sasa
 
Dakika 27''
Kameta anamimona krosi inakuwa kona lakini Traore golikipa wa Stade Malien anaundaka kiulaini kona hiyo ya Simba

SSC 1 - 0 SML
 
Dakika 30'
Hadi sasa Simba wanasukuma mpira kwa pasi za taratibu sana, tofauti na mechi ya Mamelodi Sundowns vs MCA iliyopigwa Pretoria Sauzi mapema leo mechi ilikuwa ya kasi sana

SSC 1 - 0 SML
 
Dakika 37'

Krosi ya Kameta inatolewa kona, Chama anamimina kona isiyokuwa na matunda Stade Malien wanaondosha kiulaini

SSC 1 - 0 SML
 
Dakika 40'
Koulibaly wa Stade Malien anajaribu kumzunguka Conte wa Simba lakini anasimama imara

SSC 1 - 0 SML
 
Back
Top Bottom