Manchester United imeendelea kudondosha pointi baada ya kupata sare ya goli 1-1 dhidi ya Fulham katika Premier League, ikiwa ni mchezo wa tatu mfululizo kutopata ushindi katika michuano tofauti msimu huu wa 2026/27.
Kabla ya mchezo wa leo Septemba 20, 2026, Man United ilifungwa na Manchester City (1-0) katika EPL, ikapoteza 3-2 dhidi ya Brighton katika Carabao Cup, matokeo ambayo yanamuweka katika presha kubwa Kocha Michael Carrick ambapo timu yake ina alama 5 katika michezo mitano ya EPL.