FT: Mbeya City 2-1 Azam FC | NBC Premier League | Uwanja wa Sokoine

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania NBC Premier League imeendelea tena leo kwa mchezo mmoja ambapo Mbeya City walikuwa wakiwakaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa Sokoine.

Mchezo umekwisha kwa Mbeya City kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Azam FC, ambapo wenyeji ndo walikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Azam FC kunako dakika ya 51' kupitia kwa Juma Shemvuni baada ya kutokea piga nikupige lango la Azam.

Mbeya City waliendelea kuliandama lango la Azam FC kwa mashambulizi zaidi, ambapo kwenye dakika ya 83' Azam FC walijifunga bao kwa mlinzi wake wa kati Daniel Amoah kumpoteza maboya golikipa wake Ahmed Salula, akimuacha akichumpa bila mafaniko.

Kuelekea kumalizika kwa mchezo huo, Azam FC walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Ayoub Lyanga kwenye dakika ya 88' baada ya beki kufinywa na kuachia shuti kali lililogonga mwamba wa juu na kujaa wavuni.

Hadi mwisho wa mchezo Mbeya City mbili na Azam FC moja | FT: Mbeya City 2-1 Azam FC

Azam wanapoteza mchezo wa sita msimu huu kwenye Ligi Kuu Tanzania.

Je una maoni gani kuhusu mwenendo wa Azam FC msimu huu..?
 
Hivi hawa Azam FC ndo wale Haji Manara alisema kuwa ndo wapinzani wa Yanga msimu huu...!?
Ni kweli kwani aliongea akijua utopolo yupo hapo kwa sababu ya bahasha. Kama ni uhalisia ni kweli Azam ndiyo washindani wa Utopolo na akisema hivyo alijaribu kujipa hadhi kidogo ili timu yake ionekane ina utajiri kama wa Azam
 
Leo Azam wamekufa tena bao 2 - 1 kutoka kwa Mbeya City

Kiukweli Azam sasa hivi sio tena timu ya kuiongelea, timu imefanya uwekezaji mkubwa, ina kila kitu, ina uwezo wa kumsajili mchezaji yeyote ukanda huu wa Afrika lakini hakuna chochote cha maana wanachokifanya.

Msemaji wao Zakazakazi amekuwa na maneno mengi kuliko vitendo, wanakula posho na mishahara ya bure tu. Azam ilipoachana na akina Bocco, Manula, Nyoni na Kapombe na baadae ikamuachia Kipre Tchetche, kocha akiwa Stewart Hall, jamaa walikuwa hatari sana, haitokuja tena Azam ya namna ile NEVER NEVER NEVER.

Namshauri Bakhresa aweke nguvu zaidi kwenye nguvu kwenye biashara zake huku kwenye football, hapana, watu wanaongoza Azam lkn wana mahaba na Simba na Yanga.

Simba na Yanga wataendelea kupokeza pale juu hadi siku ya kiama.
 
Mbona hueleweki heading Azam ameshinda 2 kwa 1 maelezo Azam amefungwa 2 embu tueleweshe vzr siyo wote tumeangalia hiyo game
 
Moderator, Tafadhali sana usinilishe maneno, sijasema kama azam ameshinda, tafadhali sana usinivunjie heshima, azam amefungwa 2 - 1 na Mbeya City, we umeandika hapo juu
 
Azam ushindi wake ni kutengeneza bidhaa bora.huku kwenye soka hamna kitu wahuni wanampapasa mwanzo mwisho.
 
Kwa kule South Africa, Azama Fc utaifananisha na Mamelod kwa uchanga wake kwenye ligi na wamiliki wenye pesa, lakini sijui kwanini Azam imekuwa ya kijinga hivi. Hii team ilitakiwa itawale kabisa soka la Tz na Africa ikimbize sijui wanafeli wapi?

Shida ni viongozi wa Azam Fc, kwakuwa kwanamna yoyote ile ni lazima watakuwa ni Yanga au Simba sc.
 
Back
Top Bottom