Friends of Membe UK kukutana siku ya Jumamosi

LEMONT BISHOP

Member
Oct 29, 2014
85
88
Mikakati ishakamilika na kwa taarifa za uhakika kuwa friends of Membe wanakutana London siku ya Jumamosi tarehe 6.

Mkutano huo utatumika kuzindua rasmi hili kundi na pia utawapa wanachama taarifa za kiasi cha pesa ambacho kimepatikana (inasemekjana washakusanya karibu dola milioni 2 toka kwa watu na mashirika mbali mbali ambao washajiweka sawa kutawazwa kwa Mh Membe kuwa rais wa awamu ya Tano.

Cha ajabu ni kuwa kundo hili linaongozwa na watu waliodhaniwa kuwa ni mahasimu wakubwa wa membe (lakini kama wanavyosema kuwa kwenye siasa hakuna permanent friends au enemies bali kuna permanent interests).

Ilele kundi la FRIENDS OF LOWASSA UK liliingia kwenye mfarakano baada ya wale vijana 4 walioaminiwa na mapesa kujinunulia nyumba mortgage free huku wakisingia kuwa Fred aliwapa idhini.

Chanzo cha hii habari ni whatsapp messages toka kwa friends of Membe UK.
 
Hii nchi hivi sasa haina kiranja.....ndio maana tunahamasisha wananchi wenyewe wawe viranja....
 
kwani hamkusikia Makongoro katia nia???
mnahangaika ila ni MAKONGORO kwa ccm 2015
 
Membe anatangaza nia take juma2 mkoani Lindi. Tayari maandalizi yameshafanyika. Hafla hiyo ya kutangaza nia ilikuwa ifanyike J1 lakini imesogezwa mpaka tarahe 7.6.2015.

Inavyoonekana mwaka huu ili kupunguza makali ya chama kusambaratika baada ya uteuzi Wa mgombea, huwenda wale wote waliosimamishwa miezi 12 kwa kuanza kampeni mapema safari zao zikaishia kwenye vikao vya awali!

Huenda pia wimbi kubwa la wanachama wengi wa CCM kutangaza nia ni mkakati uliyosukwa vizuri, ili kuwakabili baadhi ya makada wenye nguvu ndani ya chama.

Hii Ina maana kwamba wakienguliwa wengi wale wakose hoja za kulalamika. Hata hivyo wadadisi Wa masuala ya kisiasa wanashauri kuwa, mbinu inayotakiwa kutumika itakiacha CCM hoi na vipandevipande.

"Ni bora wakawasikiliza wananchi wanamtaka nani, matokeo ya kura za maoni, ya vijana waliotumwa mikoani na Chama ingetumika kumpitisha mgombea anayekubalika" alisema mchambuzi mmoja wa kisiasa. Aliongeza kuwa " Kizazi cha Leo hakifahamu CCM, wengine wamekuwa wakati chama hiki hakina nguvu na upizani una nguvu, kwa hali hii, haijalishi ni mtume au malaika atateuliwa na Chama. Muhimu kupitia yote ni mtu ambaye Watanzania wenyewe wanayemtaka, hiyo ndiyo itakayokuwa salama ya chama".
 
Back
Top Bottom