KaKweli kabisa pamoja familia yake, CDM na Watanzania kwa ujumla. Ili kauli ya Mama iwe na mashiko " Tusahau yaliyopita tuanze ukurasa mpya..."
Kauli ya Mh Rais kuwa tusahau yaliyopita ni maombi ya msamaha kwa kupandisha mabega. Unajua umemjeruhi mtu halafu unamuomba msamaha huku umemfunga pingu halafu kwa kejeli.
Kauli yake ingekuwa na dhamiri njema isiyobeba jeuri ya madaraka ni nzuri na inatia moyo. Rais wetu namuona ana dhamiri njema ila kuna msukumo nyuma yake toka kwa wahafidhina ndani ya chama chake na serikalini.
Mheshimiwa Rais wangu dhamiri yako ikiifuata na kuitii ndio itakayokuweka huru na kukupatanisha na Mungu wako. Kindly heed to your internal commands milango yote ya baraka itakufungukia. Hutapata kazi kujinadi uchaguzi ujao na utaweka kumbukumbu kimataifa.