Freeman Mbowe aiyumbisha dola

mwobho

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
808
352
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Jeshi la Polisi nchini vimeonekana kusua kusua katika kulichukulia hatua sakata la kuhamisha na kumiliki pesa na akaunti nje ya nchi kunakomilikiwa na Mtanzania Freeman Aikael Mbowe.

Kwa muda mrefu sasa, watanzania wa kada mbalimbali wamekuwa wakitaka kujua hatma ya kiongozi huyo wa kisiasa ambaye pia ni mfanyabiashara kwamba ni lini vyombo hivyo vya serikali na dola vitachukua hatua stahiki.

Kila mara ambapo Gazeti hili lilipojaribu kutaka maelezo ya mamlaka ya mapato tanzania TRA kama kiasi cha pesa kinachomilikiwa na Mbowe kimekuwa kikilipiwa kodi, mamlaka hiyo imekuwa kimya na kila mara ambapo Kamishina wa mamlaka hiyo alipopatwa kwa njia ya simu amekuwa akijibu tunashuhulikia tutakujuza muda sio mrefu.

Kusua sua huko kwa TRA kunaenda sambamba na Jeshi la polisi ambapo kila linapoulizwa kuhusu taarifa hizo za mbowe, wahusika wake hikata simu na kukataa kumkaribisha mwandishi wa gazeti hili ofisini kwake.

Tofauti kabisa na Gavana wa benki kuu ambaye bila kuuma maneno alitoa ushirikiano kwa kisema Benki kuu haina taarifa kuhusu akaunti hizo zonazomilikiwa na mwanasiasa huyo machachari.

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili linazo, zinathibitisha kwamba Benki kuu ya Tanzania imeshalifanyia uchunguzi swala hili na kumaliza na kwamba kinachokwamisha kwa sasa ni FIU na Polisi kuchukua hatua bila ya sababu za msingi.

Hivi karibuni Gazeti hili limeripoti juu ya uwepo wa uwezekano wa kukamatwa, kuhojiwa na kupandishwa mahakamani kwa Mwenyekiti huyo wa- CHADEMA, Freeman Mbowe kutokana na kashfa ya kutorosha fedha nje ya nchi baada ya Benki Kuu ya Tanzania kulithibitishia gazeti hili kuwa--benki hiyo haina taarifa zozote zinazohusu umiliki wa akaunti hizo tofauti na sheria inavyoelekeza.

Sheria ya usimamizi na--wa fedha za kigeni ya mwaka 1998 (Foreign Exchange Circular)-inatamka bayana kwamba mtanzania yeyote, hataruhusiwa kumiliki ama kufungua akaunti nje ya nchi bila kwana kupata kibali cha Gavana wa Benki Kuu.

Kifungu namba 3.3 cha sheria hiyo ya waka 1998 kinatamka ??itakuwa ni marufuku kwa raia wa Tanzania kufungua akaunti kwenye benki nje ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama sio mkazi katika nchi hiyo isipokuwa tu aweamepata kibali cha gavana wa benki kuu??

Kifungu hicho cha sheria kinakwenda tofauti kabisa na kitendo cha mtanzania freeman mbowe anayemiliki akaunti kadhaa nje ya nchi zikiwemo zile za kampuni yake ya ARETRAWORLD WIDE LIMITED yenye maskani yake falme za kiarabu ikiwa na akaunti za fedha za kimarekani yaani--dola na fedha ya kiarabu yaani--Riyar kila moja--kwa akaunti namba 001105549660010 na 00110549660010.

Uchunguzi uliofanywa na Jamvi la Habari umebaini kwamba pamoja na sheria kutamka bayana, lakini wafanyabiashara kadhaa akiwemo Mbowe, wanaomiliki makampuni nje ya nchi wamekuwa wakifungua na kumiliki akaunti hizo bila kupata kibali cha gavana wa benki kuu kama ambavyo sheria inaelekeza.

Jamvi la Habari, lilipomuuliza Gavana wa benki kuu ya Tanzania kama ufunguaji wa akaunti hizo zinazomilikiwa na Freeman Mbowe kuwa zimefuata utaratibu na kupata kibali ya Gavana wa Benki kuu, Gavana Profesa Benno Ndullu, alijibu kuwa Benki Kuu haina taarifa yoyote kuhusu akaunti hizo, jambo linaloongeza sintofahamu kuhusiana na uvunjwaji huo wa sheria unaofanywa na kiongozi huyo mkuu wa CHADEMA.

"Benki kuu haina taarifa juu ya akaunti hizi" alisema Gavana ndulu akijibu swali la mwandishi wa gazeti hili.

Kutokufuatwa kwa matakwa hayo--ya sheria hiyo kwa mfanyabiashara huyo kunamuweka katika hatihati ya kukutana na kifungo cha miaka 14 jela ama kutozwa faini ya kulipa mara tatu zaidi ya fedha alizotunza katika akaunti hizo zilizopo nje ya nchi kama sehemu ya 13(4) ya sheria--namba 14 ya mwaka 1992 ya fedha za kigeni--inavyosema.

Hivi karibuni gazeti hili liliandika uwezekano wa jeshi la--Polisi Nchini kumkamata Mwenyekiti huyo--wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa kudaiwa kutorosha mabilioni ya fedha kwenda nchi mbalimbali za Bara za Asia.

Uchunguzi uliofanywa na JAMVI LA HABARI, umebaini kwa kiasi kikubwa uchunguzi uliokuwa unafanywa na Kitengo cha Uchunguzi wa Fedha--kilicho chini ya Wizara ya Fedha (FIU) kimekamilika huku Polisi ikitarajia kuanza kuchukua hatua zaidi.

Taarifa ilizozipata gazeti hilo kutoka FIU, ilisema tayari kila kitu kimemalizika na kilichobaki ni suala hilo, kulipeleka Polisi kwa ajili ya kuchukua uamuzi zaidi wa jambo hilo.

"Tumemaliza kila kitu na kilichobaki ni Polisi, lakini mie sio msemaji wa suala hilo, ungezungumza na watu wa FRAUD kutoka Polisi, ambao watakupa nafasi nzuri ya suala hilo, ambalo ni kubwa sana,''alisema.

Hata hivyo, Gazeti hili liliwasiliana na mmoja wa askari wanaoelezwa kulishikiria suala hilo, Salum Kisai, ambapo alisema yeye sio msemaji na kumtaka mwandishi awasiliane na Kamanda wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ZCO Costastine Massawe na kukata simu.

"Embu wasiliana na ZCO mie sio msemaji wa suala hilo,''alisema na kukata simu.

Mbowe, ambaye alisafirisha fedha hizo mwanzoni mwa mwezi wa Agosti, mwaka huu baada ya kuamisho mabilioni ya fedha kwenye akaunti yake hivi karibuni bila kuwa na vielelezo vya kufanya hivyo na kutakiwa kukamatwa na kumfikisha katika vyombo vya dola.

Mbowe, ambaye pia--ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mbunge wa Hai na mfanyabiashara mwenye makampuni mengi hapa nchini, amefanya uhamisho huo wa fedha kwa kutumia kampuni isiyofahamika sana ijulikanayo kwa jina la Aretra World Wide Limited na imethibitika kwamba--amefanya uhamisho huo wa fedha kwa kumtumia mtu anayeitwa Junaid Ali, ambaye ni Meneja wa Mahusiano ya Wateja wa Benki ya Noor--ya Falme za Kiarabu mwezi huo.

Taarifa zaidi zinathibitisha kwamba, Kwa kumtumia Ali, Mbowe aliagiza fedha hizo zipelekwe katika akaunti tatu tofauti ambazo zote ziko nje ya Tanzania.

Kampuni hizo na kiasi cha fedha kilichopelekwa ni Puku Hong Kong Limited iliyotumiwa dola 230,555 (shilingi milioni 461), TanChin Trading Co. Limited iliyotumiwa dola 302,614 (shilingi milioni 605) na Hong Kong Da Web International Tradings Limited-iliyotumiwa dola 489,860 (shilingi milioni 980). Jumla ya fedha zote zilizohamishwa ni zaidi ya shilingi bilioni mbili.

Makampuni yote yaliyotumiwa fedha yana ofisi zake nchini Hong Kong na yote yamefunguliwa akaunti katika benki maarufu ya HSBC.

Junaid Ali ambaye amepewa maelekezo ya kufanya malipo hayo ni mtaalamu wa masuala ya kufungua makampuni yanayojulikana kama offshore ambayo mara nyingi hutumiwa na wafanyabiashara kufanya malipo pasipo kujulikana na watu.

Taarifa zinaendelea kusema kwamba makampuni ya namna hii hufunguliwa katika nchi zenye usiri mkubwa kwa watu wanaohifadhi fedha na ndiyo maana wakati wa sakata la ununuzi wa rada, Andrew Chenge na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Idris Rashid, walitumiana fedha kupitia akaunti zao zilizo katika nchi zinazoongoza kwa kuwa na makampuni mengi ya namna hii.

Akimwandikia Junaid, Freeman--Mbowe alisema; "Tafadhali, nakuomba na kwa haraka, ufanye uhamishaji wa fedha kutoka katika benki yako na kwenda kwenye akaunti zifuatazo; Puku, TanChin na Hong Kong Da Web," aliandika Mbowe.

Katika barua hiyo ambayo JAMVI LA HABARI imefanikiwa kuona nakala yake, Mbowe ameitambulisha kampuni yake kwa anuani ya S.LP 293816, iliyopo katika jengo la World Trade Centre, Mtaa wa Sheikh Zayed, Dubai--falme za kiarabu.-

Kwa kuwa kampuni hiyo ya Mbowe ni offshore, gazeti hili limeshindwa kufahamu ni kiasi gani cha fedha Mbowe amehifadhi au ameweka kwenye akaunti hiyo na chanzo cha mapato hayo ni kipi kwa vile biashara zake nyingi anafanya hapa nchini, ingawa ameanza kujitanua kimataifa.

Sambamba na hilo , uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba Mbowe alitakiwa kupokea kiasi cha dola 330,000 (shilingi milioni 660) -takribani sawa na fedha aliyoihamishia TanChin Hong Hong, kutoka kwa wafadhili wa chama hicho waliopo nchini Japan.

Kwa mujibu wa mawasiliano baina ya viongozi wa juu wa Chadema na wafadhili hao wa kijapani kupitia kwa mtu anayefahamika kwa jina la Naomi pamoja na Mchungaji Mariko Morikubo, Chadema ilikuwa ichangiwe fedha za kijapani (Yen), milioni 40 ambazo ni sawa na dola 330,000 kabla ya mwisho wa Julai mwaka huu.

Ndani ya CHADEMA, ni viongozi wakuu watatu ndiyo wanaonekana kushiriki katika mazungumzo hayo; Mbowe, Slaa na Reginald Munisi ambaye ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho.-

Mpaka sasa haijafahamika mara moja ni kwa nini Mbowe amehamisha kiasi kikubwa namna hiyo cha fedha na kukipeleka nje ya nchi na kwamba imeendelea kutia mashaka kama kuna kodi halali ya serikali imekatwa katika muamala huo.

Wakizungumza na gazeti hili lilipotaka kujua mtazamo wao kuhusu kinachoitwa "utumbuaji majipu wa magufuli"--wananchi kadhaa wamesema hicho nacho ni moja kati ya kipimo kikubwa cha uimara wa serikali ya magufuli na kwamba kama ataweza kumkamata Mbowe basi ataonekana kweli amedhamiri kulikomboa taifa letu na kuthibitisha msemo kwamba sheria ni msumeno.

Omary Mwinshehe, mkazi wa msamvu Morogoro amesema, ili nchi yoyote inayofuata na kuheshimu utawala wa sheria ni lazima watu wote waishi misingi na utaratibu wa nchi hiyo, Mwinshehe amesisitiza ikiwa Mbowe ameweza kufanya hivyo na kama hatua haitachukuliwa dhidi yake, basi kuna uwezekano mkubwa wa wanasiasa wengine kutumia uanasiasa wao kufanya biashara halali na haramu kujinufaisha.-

"Tanzania sisi sijui tumerogwa na nani,mtu--kama mbowe anaweza kusafirisha zaidi ya bilioni mbili kiharaka haraka hivyo, unatarajia kuna uhalali hapo" ,nani amekagua hizo hela na kuthibitisha ni halali na hazina madhara wala viashiria vya rushwa?.

Ameendelea kushangaa na kuonyesha taadhari ya hali ya juu na kumtaka Rais Magufuli kuhakikisha anaendelea kutumbua majipu na kusisitiza kwamba asimuangalie mtu yeyote usoni na kwamba ni lazima sasa vyombo vya dola vikachukua nafasi yake na kuthibitisha uhalali wa fedha hizo .

Mara kadhaa Mbowe amekaririwa kama mtu anayetetea sana uwepo wa utawala wa sheria na kwamba amekuwa akiilaumu serikali na taasisi nyingine zisipofuata sheria, jambo ambalo yeye pia anakabiliwa nalo hivi sasa.

Kutokana na FIU kukamilisha uchunguzi wao huo na kulikabidhi jeshi la polisi kama ambavyo sheria inaelekeza, basi ni wajibu kwa- jeshi la polisi kumkamata na kumfikisha mahakamani kwa tuhuma za usafirishaji fedha isivyo halali.

Gazeti la Jamvi la habari linaendelea na ufuatiliaji wa suala hili kwa undani na kuendelea kutoa taarifa kwa umma kwa kadri itakavyohitajia kama sehemu ya kumsaidia Rais John Pombe Magufuli kutumbua Majipu.


CHANZO : GAZETI JAMVI LA HABARI
 
Mbona wale wanaosafirisha meno ya tembo hamuandiki au hao wana kibali?
 
falme za kiarabu zinatumia dirham sio riali. Huu uandishi wa bila research ni tabu sana.
 
na Zile 320 za escrow wamekuambia account zake zinakibali na zimegeuka financial art ipi

na account mnazoanika mnakibali cha bank ipi kuu

nilitaka asiwe na hela mnavyotaja hizo bilion nyie za kwenu mnaweka Saccoss ipi?
 
Kila saa mbowe!mbowe mbowe! Tushawachoka bana
Mwacheni ajenge chama bana
 
Halafu rais anasema tu move on kwa sababu uchaguzi umeisha wakati chama chake kinaendeleza propaganda za kipuuzi!!!
 
Kama Escrow, EPA, Kagoda, Deep Green, Meremeta, Rada NK. Hazikuyumbisha Dola Leo hata kama Ni Kweli Mh. Mbowe

Kuweka fedha Halali Tatizo Lipo wapi.Kigezeti Gani Uchwara Hiki Hata K'Koo Wahuni Hawakisomi na Mamalishe /Vitumbua Hawafungii Vitumbua
 
Wwe ni mpumbavu. Huna uzalendo wala uchungu wowote kwa taifa bali umejaa wivu, chuki na majungu ya kipumbavu. Umejuaje Mbowe hajafuata taratibu zinazotakiwa?

Ungelikuwa na moyo huo, ungeanzia na malumbesa yaliyobebwe kutoka Stan Bic na meno ya tembo, twiga kupanda ndege, biashara ya Loliondo nk. ambayo hata magufuli hathubutu kuizungumzia badala yake watuhumiwa anawapa vyeo bila kuwafikisha mahakamani japo wakasafishwe.

Pumbavu usituuzie upumbavu wako hapa peleka jikoni kwa mkeo na mishenzi myenziyo.
 
Naona hii habari inarudiwa kwa kubadilisha aya chache za mwanzo.
Kwani gazeti la nani
 
Unafanyia kazi swala la mbowe au wote waliopeleka nje? Naona kila kukicha ni post yako kuhusu Mbowe uchunguzi wako ni juu ya Mbowe au unachunguza wote walioficha pesa nje?

Je weee umegundua Mbowe tu?

Majibu tafadhali!
 
​Mbona humuandiki mzee wa vijisenti ambaye yeye mwenyewe alisema na kudhibitisha!!!! Au unaliogopa Joka la makengeza!!!!
 
Baqdala ya kuanzia apesa za watu binafsi, Tusaidie kufichua ukweli kuhusu fedha za umaa zilizoporwa kwama vile EPA< ESCRO, n.k. Uchunguzi wako ni mzuri lakini ulipoanzia si penyewe. Zipo pesa za UMMA zinazowakera wananchi.
 
Napendekeza ukaguzi wa vyeti halali vya kitaaluma ufanyike kwenye tasnia hii ya UANDISHI WA HABARI. Maana tumechoshwa na MAKANJANJA ....
 
Kwa mtindo huu JPM ataanza kufukuza mawaziri wake si muda mrefu!

Yaani jamaa mmeanza kazi juzi badala ya ku deal na sensitive issues mimsaidie Rais wenu atumbue majipu makubwa makubwa ndani ya CCM na serikali yenu, mmeona tatizo kubwa la nchi hii ni Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Bwn Freeman Mbowe!!

Are you really serious kumsaidia Rais au mnataka kumtoa ktk njia sahihi anamopita sasa???

Badala tuumize kichwa namna ya kuwapata wahalifu wa TEGETA/ESCROW ACCOUNT waliochota mapesa mabilioni katika magunia, viroba na kupakiwa ktk pickups na fuso kutoka benk ya StanBic, na kashfa za EPA, watorosha makontena bandarini pasi na kulipa kodi, waatorosha wanyama wetu kwa madege ya kiarabu nk, tumekalia Mbowe, Mbowe, Mboweeeee.....!

This is not right at all.

After all Mbowe is not stupid to this extent kwa nafasi aliyonayo ktk opposition party camp huku akijijua wazi kuwa is the most hunted politician ever ktk uwanja wa siasa za Tanzania!

Nakumbuka muda mchache kabla ya harakati za uchaguzi mkuu hazijaanza mwaka jana na hata kabla hata Edward Lowassa hajakaribishwa CHADEMA na watu kufikiri tu kuwa angejiunga, watu hawahawa walianza kuzagaza ktk mitandao ya kijamii kuwa Mbowe ni mkwepa kulipa kodi za serikali kupitia ktkbiashara zake za hotel (AIKA PROTEA HOTELS na biashara zingine)

Sijui hii move ilishia wapi maana hatukuona TRA wakichukua hatua zozote na jamaa aligombea ubunge ktk jimbo lake la Hai Kilimanjaro na kwa kampeni za siku tatu tu akawagaraza CCM kwa mbaali saana!

Hizo propaganda zililenga kumzuia jamaa azuiliwe kugombea ubunge huko kwao, lakini wapi bwana. Sina hakika hizi za kina Kashindye Ngalu zina lengo gani!

Ni wazi kuna jambo linataka kuzuliwa kwa njia za kijinga kama hizi, eti tuaminishwe kuwa hata Mbowe naye ni fisadi tu.........lol, hatarii!!
 
Back
Top Bottom