assadsyria3
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 6,909
- 4,057
Waziri Mkuu wa zamani wa serikali ya
awamu ya tatu, Frederick Sumaye
(Kushoto), mgombea ubunge wa
Jimbo la Bumbuli kupitia CCM,
January Makamba (Kulia)
Soni: Waziri Mkuu wa zamani wa
serikali ya awamu ya tatu, Frederick
Sumaye amemsifu mgombea
ubunge wa Jimbo la Bumbuli kupitia
CCM, January Makamba na kusema
kuwa haelewi kwa nini anaendelea
kungangnia CCM wakati yeye si
fisadi.
January wewe si mwizi, kwa nini
unangangania chama hicho,
alisema Sumaye wakati akizungumza
katika mkutano wa kampeni
kumnadi mgombea urais kupitia
Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Edward
Lowassa, katika jimbo la Bumbuli
jana.
Sumaye alikuwa akiwaambia
wananchi wamuulize mbunge wao
(January) kuhusu suala la wizi wa
pembe za ndovu zilizokamatwa Hong
Kong na madeni makubwa ya taifa
kwa sababu anaweza kuwapa majibu
kwasababu yeye ni msafi.
Katika mkutano huo, waziri mkuu
huyo wa zamani alimtaka mgombea
huyo na watu wengine wanaotaka
kuhama wasiogope kufanya hivyo.
Aliwataka wananchi wapime
wenyewe kama wanaamini kuwa
CCM imetekeleza walioahidi basi
wakichague na kama hakikutekeleza
wafanye mabadiliko kama zilivyo
nchi nyingine duniani.
Sumaye alisema kuwa CCM iliahidi
maisha bora kwa kila Mtanzania
lakini kimeshindwa kuetekeleza yale
ambayo wamehidi hivyo Watanzania
wanapaswa kukiweka kando na
kufanya mabadiliko kama vile
ilivyofanyika Kenya, Malawi na nchi
nyingine walipoona vyama tawala
havikuleta maendeleo.
awamu ya tatu, Frederick Sumaye
(Kushoto), mgombea ubunge wa
Jimbo la Bumbuli kupitia CCM,
January Makamba (Kulia)
Soni: Waziri Mkuu wa zamani wa
serikali ya awamu ya tatu, Frederick
Sumaye amemsifu mgombea
ubunge wa Jimbo la Bumbuli kupitia
CCM, January Makamba na kusema
kuwa haelewi kwa nini anaendelea
kungangnia CCM wakati yeye si
fisadi.
January wewe si mwizi, kwa nini
unangangania chama hicho,
alisema Sumaye wakati akizungumza
katika mkutano wa kampeni
kumnadi mgombea urais kupitia
Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Edward
Lowassa, katika jimbo la Bumbuli
jana.
Sumaye alikuwa akiwaambia
wananchi wamuulize mbunge wao
(January) kuhusu suala la wizi wa
pembe za ndovu zilizokamatwa Hong
Kong na madeni makubwa ya taifa
kwa sababu anaweza kuwapa majibu
kwasababu yeye ni msafi.
Katika mkutano huo, waziri mkuu
huyo wa zamani alimtaka mgombea
huyo na watu wengine wanaotaka
kuhama wasiogope kufanya hivyo.
Aliwataka wananchi wapime
wenyewe kama wanaamini kuwa
CCM imetekeleza walioahidi basi
wakichague na kama hakikutekeleza
wafanye mabadiliko kama zilivyo
nchi nyingine duniani.
Sumaye alisema kuwa CCM iliahidi
maisha bora kwa kila Mtanzania
lakini kimeshindwa kuetekeleza yale
ambayo wamehidi hivyo Watanzania
wanapaswa kukiweka kando na
kufanya mabadiliko kama vile
ilivyofanyika Kenya, Malawi na nchi
nyingine walipoona vyama tawala
havikuleta maendeleo.