Fredrick Sumaye, Laurence Masha na Lazaro Nyalandu nahisi wanatamani wangesubiri kidogo

DALA

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
2,212
4,517
Hawa wanasiasa baada ya kusoma upepo ulivyo na misukosuko iliyoikumba nchi hususani chini ya Mwendakuzimu.

Mwendakuzimu aliwakaba watu, kila mpinzani alikabiliwa na tishio la kesi isiyo na dhamana jambo ambalo liliwafanya watu wengi waone bora waunge juhudi kuepusha shari.

Ni katika kipindi hicho ndo tumeshuhudia wanasiasa tuliowaamini kama Lijwalikali, Joshua Nasaari na Silinde kuomba kijiunga na Chama Cha Majizi kila mtu kwa staili yake. Lijualikali alilia machozi mbele ya kamera!

Ile hatujakaa sawa, hao hapo Halima Mdee kaingia bei na kuzoa wenzake 18 ndani ya BAVICHA,

Hakika haikuwa rahisi kwetu wapigania haki.

Naamini wote hawa nafsi zinawasuta leo, maana hawakutegemea kwamba Mwendakuzimu angeondoshwa na UVIKO. Laiti wangejua, wangesubiri ila ndiyo hivyo wamekwisha kusaliti nafsi zao.

Naamini wanatamani kurudi ila ndo basi tena, ushawishi umeisha, kwa sasa wengi wanalazimika kukaa kimya maana hawawezi kuongea tena kwa ujasiri ule wa zamani kabla ya kulamba damu.

Sisi wengine tuliweza kuyastahimili vishawishi vya Mzee wa V8 aka Slwo slow aka mhadhiri wa masuala ya uongozi. Jamaa alitwikwa mzigo wa jukumu la kununua miamba ya upinzani. Hakika akacheza kama yeye, wanasiasa wakaingia bei mpaka Katibu Mkuu wa CHADEMA akatupa silaha mwishowe ameambulia zawadi ya ukuu wa wilaya.

Ahsante sana UVIKO kwa kucheza kama wewe!
 
Jambo moja unalopaswa kujua ni kuwa mwanasiasa hana nafsi ya kujutia. Mwanaisiasa anaangalia maslahi yake binafsi tu kwa wakati husika.
Hao wote uliwataja wana uwezo wa kubadilika na kurudi walikotoka endapo kimaslahi itawafaa. In short siku zote mwanasiasa msikilize lakini usimuamini.
Kwao wao kuwepo ama kutokuwepo kwa Mwendazake ni fursa kama fursa nyingine tu.
 
Ila Magu alikaza kinoma,wakaonekana wale upinzani kweli,na wale feki,feki wakasepa kinoma kumgwaya asiwape mateso,hadi kifo kinamkuta,chamoto kilikua kimewakuta CHADEMA kwelikweli.Naona akina Mdee hata kwenye kesi wanakosa ujasiri wa kwenda,Lwakatare namsifu,hana maneno mengi,leo nimemuona.2025 CCM asilia watawatenga wale CCM waliokimbia harakati wakaunga juhudi na kupewa vyeo,naona mtifuano utakua wa hatari.Kifo cha Magu kwakweli ni pigo hasa,mategemeo ya wale waliokua wanamtumainia ilikua ni had I 2025 na walitegemea angeweza hata kuongeza muda waendelee kula mema ya nchi.Pole yao.
 
Back
Top Bottom