Framework au CMS nzuri kwa kutengeneza simple System

Jitu jeusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2015
Posts
1,722
Reaction score
2,401
Habarini wataalam,
Ningependa kufahamu techology gani nzuri sana kwa kutengeneza simple web system kama:-

System ya Saccoss
System ya Phamarcy
Nk

Ipo nzuri kati ya hizi kutumia :-
Laravel
Nodejs
Angularjs
Django
Yii
Au yeyote unaweza kuweka kwa msaada zaidi..

Pia au kupiga code za PHP kavu mwanzo mwisho.

Msaada wa mawazo tafadhari
 
Wadau naona kimya

Sent from my GT-N7000 using Tapatalk
 
kuna mdau kashakujibu vyema hapo. Kama upo vyema PHP kavu piga mwanzo mwisho achana na hizo framework
 
Swali muhimu nikuulize umeshajifunza lugha zipi na ulizionaje au ndo unajifunza ukijibu ntakupa jibu la swali lako
 
tumia php(Object oriented) kavu mix na AJAX ili kutoa page refresh endapo data zikiwa submitted, lkn pia kama ww sio mpenzi wa "From scratch" nakushauri utumie django coz iko vizuri kwenye security na ina community support kubwa github ukilingaanisha na laravel ya php




happy coding.....
 

Unataka umpoteza mdau. Django na PHP wapi na wapi.
Django ilikua designed mostly for Python.
Kwa PHP frameworks tatu kubwa ni Laravel, CodeIgniter na Symphony basi.
 
Unataka umpoteza mdau. Django na PHP wapi na wapi.
Django ilikua designed mostly for Python.
Kwa PHP frameworks tatu kubwa ni Laravel, CodeIgniter na Symphony basi.
Mama Debora, Debo my first daughter kumbe umekulia mitaa hii? Haya karibu kimodole kimoja haka cha codeigniter umpelekee mwanangu Debo
 
Me nnasysterm kibao ila zipo kama source code zpo kwenyemfumo wa zip kama nkitaka kuziedit inawezekana???
 
Haujaeleza madhumuni yako ni kujifunza au ni kutengeneza systems za production.
- Kama nia ni kujifunza development, bora uanze from scratch ili uwe na ufahamu mpana wa shughuli yote nzima.
- Lakini kama ni systems za production, usithubutu from scratch utapoteza muda na kuchelewesha miradi ya watu. Tafuta framework moja maarufu, komaa nayo kishenzi yaani, wadau wengi wanasifia sana Laravel ila pia hata Yiii sio mbaya.

Binafsi mimi hufanya customization za Joomla maana yenyewe inakuja na features kibao, sihangaishi akili, yaani nachomoa bonge la system industrial level ndani ya muda mfupi sana, mteja anaridhika na maisha yanaendelea.
Cha msingi ni kuhakikisha unachomoa system iliyo robust, secure, fast, scalable n.k. tena kwa muda mfupi.

Miaka yote ambayo nimekua kwenye hii industry, wateja wengi hawana muda na teknolojia unayochagua, wengi wanataka system nzuri tu iliyosheheni features zao zote na unaipokeza ndani ya muda wa mkataba. Vijana wengi hupumbazwa na hivi vita vya frameworks, unampa mradi anachelewesha kishenzi, unajikuta kwenye full ugomvi na wateja. Jamaa siku inaisha yupo anapiga codes kwenye laptop, jioni ikifika hamna kikubwa amefanikisha.
 

Umetema points nimezikubali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…