Fr. Karugendo: Tunayaona Mawingu.. Mvua.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fr. Karugendo: Tunayaona Mawingu.. Mvua..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumaku, Jun 9, 2009.

 1. S

  Sumaku Member

  #1
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Padri Privatus Karugendo

  KABLA ya mauaji ya kimbali yaliyotokea kule Rwanda, nilikuwa nimezeoa kutembelea nchi hiyo na hasa mji mkuu wa Kigali. Kati ya mambo niliyokuwa nikiyafurahia kwenye nchi hiyo yenye vilima vingi na vivutio visivyokuwa na idadi ni magazeti yaliyokuwa yakifanya uchambuzi katika mtindo wa kuuma na kuvuvia; mtindo wa kutawaliwa na unafiki na kuwalazimisha waandishi kubuni mbinu za kuandika kwa mafumbo.

  Mwanzoni mwa miaka ya tisini, magazeti ya Rwanda na hasa la Kinyamateka,(gazeti la kanisa katoliki) nililokuwa nikipenda kulisoma nikiwa Kigali, yalianza kuandika habari zilizokuwa na mwelekeo wa kujenga utamaduni wa kutoaminiana. Iliandikwa kwa mafumbo- lakini fumbo mfumbie mjinga.

  Sisi tuliokuwa wageni, hatukuweza kuelewa vizuri mafumbo yale, wale wandani walielewa; wenye kupenda kusikiliza walitambua na kuzisoma alama za nyakati; wenye uwezo wao walitimuka na kujificha nchi za nje – baada ya mauaji, ndo ujumbe ulikuwa wazi. Ndo tulitambua na kuelewa kazi kubwa iliyokuwa ikifanywa na vyombo vya habari vya wakati ule kule Rwanda.

  Ajali za barabarani na hasa zile zilizosababisha vifo vya viongozi wa serikali au wafanyabiashara mashuhuri kule Rwanda enzi zile zilihusishwa na njama za “Akazu”. Neno hili la Kinyarwanda ambalo ni aina ya fumbo, au kuipamba lugha kwa lengo la kuelezea kitu kikubwa, linamaanisha “Kanyumba”, lakini si “Kanyumba” ka kawaida, si “Kanyumba” ka nyasi wala udongo, ni “Kanyumba” ka aina yake – labda kwa maneno ya kueleweka, “Kanyumba” ka dhahabu.

  Hili lilikuwa ni kundi dogo la Wanyarwanda waliokuwa wameshika “Utamu” wote wa Rwanda: Walikuwa na madaraka, walikuwa na fedha, walitawala uchumi, walitawala siasa, walitawala utamaduni, walitawala “Utu” na walitawala dini! Hakuna aliyeingia kwenye “Akazu” bila kitambulisho. Si kila Mnyarwanda, aliruhusiwa kuingia kwenye “Kanyumba”. Si kila aliyekuwa serikalini aliruhusiwa kuingia kwenye “Akazu”. Kulikuwa na wateule wachache ndani ya serikali, wateule wachache ndani ya chama tawala, wateule wachache wafanyabiashara na wateule wachache viongozi wa dini; walimzunguka Rais wa nchi ya Rwanda na kupenyeza ushawishi wao kwa kila maamuzli aliyokuwa akiyafanya Rais wa nchi. Mfumo huu wa “Akazu” ulitengeneza utamaduni wa kutoaminiana. Ulianzisha matabaka na kuchochea ubaguzi wa kutisha.

  Ajali za barabarani zilizosababisha vifo vya watu mashuhuri, kidole kilinyoshwa kwa “Akazu”. Nakumbuka kusoma makala kwenye gazeti la Kinyamateka, iliyokuwa ikichambua mwenendo wa mambo katika nchi ya Rwanda kwa wakati ule, kwamba ilifikia mahali ambapo hata kama mtu angekufa kwa ugonjwa kama vile malaria, watu wasingeamini kama ni kifo cha kawaida. Kidole kilinyoshwa kwa “Akazu”.

  Iliaminika kwamba wale waliokuwa ndani ya “Akazu” walikuwa na uwezo wa kumpoteza mtu aliyetaka kusambaratisha “Kanyumba” kao; hivyo walitengeneza ajali, walitengeneza magonjwa na walikuwa na uwezo wa kuua kwa njia zozote zile; sumu, risasi, kunyonga nk.; kichocheo cha kulinda uhai wa “Akazu” ni madaraka milele, ni uchu wa watu wachache kutaka kumiliki uchumi wa nchi nzima: Imani kubwa ilikuwa kwamba “Akazu” ulikuwa mfumo wa kudumu kilele yote:Walijigamba, walitamba, walijivuna na kulazimisha watukuzwe.

  Sina lengo la kuandika juu ya Mauaji ya Kimbali. Yaliyotokea tunayafahamu sote. “Akazu” ni mfumo uliosambaratishwa na kupotea kabisa. Maana yake hakuna mfumo wa kudumu milele; maana yake kuna mwisho wa uchu wa madaraka, kuna mwisho wa watu wachache kutaka kumiliki uchumi wa nchi nzima.

  Katika Taifa letu Tanzania, kumezuka mwelekeo wa kujenga utamaduni wa kutaoaminiana kama ilivyokuwa Rwanda kwenye miaka ya tisini. Mbali na nyimbo za rushwa, ufisadi papa na ufisadi nyangumi, kuna matukio ya vifo na ajali za waheshimiwa, ambavyo vinaonyesha dalili zote za kutoaminiana. Akifa mtu anatafutwa mchawi. Hata kifo hicho kama ni cha ugonjwa wa wazi kama malaria,TB au UKIMWI, anatafutwa mchawi. Kama mchawi si Mafisadi, basi ni CCM au vyama vya upinzani.

  CHANZO: kwanzajamii.com
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mauaji ya kimbari ndio msemo sahihi, si mauaji ya kimbali.

  Mwandishi ametumia sehemu kubwa ya makala kuelezea kitu atakachofananisha na hoja yake kuliko kuiendeleza hoja yenyewe inayokuja jitokeza mwisho, na kwa ufupi, bila ya kusaidiwa na mifano maalum na uthibitisho wa kutosha.

  Inawezekana msingi wa anachokiandika haupingiki, lakini napata hisia kuwa angeweza kufanya kazi nzuri zaidi, hususan kwa kutumia uchumi wa maneno mzuri zaidi katika kuelezea.
   
 3. K

  Keil JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Padri Karugendo nae anauma na kupulizia, anaogopa akiuma bila kupulizia anaweza kushitukiwa, so na yeye ameungana na hilo gazeti la Kinyamateka.

  Kuna ujumbe anatamani kuufikisha serikalini, lakini anawiwa ugumu kuufikisha ukiwa uchi sana kwa kuchelea ama kuhojiwa au kufungiwa gazeti.

  Kujenga hoja kwa kutumia mauaji ya Kimbari inahitaji ujasiri wa kutosha kwa kuwa viongozi wetu hawachelewi kusema kwamba makala hiyo imekaa kichochezi chochezi na hivyo mwenye gazeti anaweza kuogopa kuweka hoja ikiwa uchi sana. Lakini wenye kusoma katikati ya mistari wanaweza kugundua kwamba ujumbe ulio hapo unaeleweka.

  Maelezo ya "Aka-nzu" yanashabihiana kwa kiasi kikubwa sana na "mtandao". Imejengeka imani kwamba mtu hawezi kupata post serikalini bila ya kuwa na connection ya mtandao. Mtu akiteuliwa utaambiwa ni connection ya RA, JK, au EL, imani hiyo iko kwenye threads mbalimbali hapa JF na hata huko mitaani. Imefika mahali watu wanaamini kwamba teuzi haziangalii merits tena bali connection na wana mtandao walio kwenye core.

  Kwenye biashara ni mambo hayo hayo tu. Tumeona juzi juzi kwenye tenda ya vitambulisho jinsi Masha na Luhanjo walivyokuwa wanashitakiana. Tuliona jinsi mambo ya Richmond yalivyokwenda, tumesoma juu ya umeme wa upepo huko Singida, tumeona mkataba wa TICTS jinsi inavyopigwa dana dana. CAG kasema mkataba ni batili, Bunge limesema mkataba ni batili, Waziri wa Fedha anasema hakuna mwenye ubavu wa kuvunja mkataba zaidi ya Rais. Hivi huo mkataba wa TICTS una nini? Kampuni zilizohusika na EPA ziko kibao, lakini zilizofikishwa mahakamani mpaka sasa ni kama nusu tu, na wengine bado wanadunda mtaani na hakuna dalili za kwamba wanaweza kupelekwa mahakamani hivi karibuni.

  Ukienda mbali zaidi, unaweza kusema kwamba ukiwa mwana mtandao unaruhusiwa kufanya ufisadi na serikali itakulinda kwa nguvu zote, kwa kuwa ni serikali ya wanamtandao, imewekwa madarakani na wana mtandao, kwa ajili ya maslahi ya wana mtandao. Lakini ukiwa siyo mwana mtandao ukikumbwa na kashfa ujue kwamba umeumia na utatoswa, hata kama wako wengine ambao wamefanya ufisadi unaofanana na ufisadi wako.

  Yaliyotokea Rwanda yanaweza kutokea Tanzania lakini siyo kwa misingi ya ukabila, bali yanaweza kutokea kwa misingi ya matabaka ya matajiri na masikini na hasa pengo litakapokuwa kubwa sana kiasi kwamba masikini haoni sababu ya kushinda njaa ama kukosa makazi wakati kuna watu wanakula na kusaza na mabaki wanapelekea mbwa wao ama kutupa kwenye mapipa ya taka.
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sawa sawa Keil,

  Kwa kutumia dhana zitokanazo na mauaji ya kimbari muandishi ana ya-"shortchange" mapambano dhidi ya ufisadi wa mtandao.Ningetegemea mtu anayetafuta sympathy on mtandao atumie mfano wa Rwanda huku akiwatahadharisha wananchi dhidi ya mgawanyiko katika jamii na chuki dhidi ya ruling class.Ukiwa unataka kuu-discredit mtandao kamwe huwezi kutumia mfano wa mauaji ya kimbari, kwa sababu unampa mtu yeyote anayetaka kupigana na ufisadi hisia kwamba anataka kuanzisha mauaji ya kimbari.

  Turns out si poor economy of words tu, bali - unless anataka kusema "by any means necessary, including mauaji ya kimbari, which I highly doubt to be the message- makala haya yana poor choiceof analogy pia.
   
  Last edited: Jun 9, 2009
 5. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Naona blogs na forums zimefanya kila mtu awe anaandika.
   
 6. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Fr.Karugendo,unayo hoja nzuri ya kuandika,na kwa kweli umeanza vizuri, lakini hujamalizia vizuri.Ulivyoanza diagnosis yako ni sawa kabisa.Tulipo sasa Tanzania ni sawa na Rwanda wakati ule wa miaka ya tisini.Kama Tanzania tutapona ni Mungu tu,Mungu aepushie mbali.

   
 7. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #7
  Jun 10, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Do you have any problem with this?
   
Loading...