Form six Uliyemaliza chukua hili

TOHATO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,170
3,775
Poleni na mitian kwa wale wote mlomaliza salama. Kufanya kwako mtiani huu nadhani umepata picha halisi ya matokeo unayoyasubiria. Yafuatayo ni baadhi na utakayo kutana nayo kwa miezi mitano iliyoko mbele pia na ushauri je lipi zuri la kufanya kwa muda huo.

[HASHTAG]#MIKOPO[/HASHTAG]

Kwenye swala la uombaji mikopo jitaidi kuangalia kwa makini vigezo vilivyotumia kwa mwaka huu kwani vingi vimekuwa vigeni tofauti na kawaida. Miaka ya nyuma ilizoeleka hata kama una mzazi mwenye uwezo ila bado mtu unaomba mkopo mradi tuu kupata hela ya matuzi(boom) , Japo yaeza kuwa tofauti na mwaka huu kwa vigezo vitakavyotumia kuwa vigumu kwa wengi hasa mlowahi soma Shule binafsi O au A lever.
Ushauri kwa hapa:
Kwanza; Kama una mzazi ambae anauwezo hata japo kidogo jitaidi kumshawishi kuamini yaezekana usiupate mkopo hivyo bas ajiandae kwa hali zinazoweza kuja kutokea kwan wazazi wengi swala la chuo huona wao hawausiki wakijua utapata mkopo
pili: Kwa huu muda wote hadi wakat wa chuo jitaidi kujiweka sehemu yoyote inayoweza kuingizia kitu chochote kile na kukihifadhi hadi muda wa chuo utakapo fika. Usiweke usista du au usharabaro hali wajua wazazi wako uwezo ni mdogo wanaeza feli chochote .NB UWE UNAUWEZO AU HUNA UWEZO MKOPO OMBA MANA WAKATI MWINGINE SWALA LA MKOPO NI BAHATI.

[HASHTAG]#CHUO[/HASHTAG]

Kwanza: Huwa wanafunzi wengi huona sifa kusoma vyuo vikubwa kama UDSM MUHAMS, SUA ,UDOM na vyuo vingine bora. Tatizo hapa ni uchaguzi wako utakuwa sahih? Vyuo yingi kwa kozi nyingi huandika Principle pas ni D mbili ila uhalisia wanaeza wakachukua kuanzia B mbili kutokana na ushindan unavyokuwa mkubwa,, Jiaidi kwenye swala la uombaji chuo kuwa karibu na wanayoyajua hayo,Ili ujue jee miaka iliyowahi kupita hi kozi nayoitaka chuo flan walichukua wenye maks gani. Usipo zingatia hili unaeza kosa chuo kizembe. Mfano mwaka 2016 kuna mwanafunzi alikuwa ana one ya 7 na ni PCB akachagua MD ya muhms na udsm bila kuomba Kcms na bugando . Alikosa hizo nafasi huku chuo cha bugando na kcms wakiwa wamechukua hadi one ya 9.

Pili: Usikimbilie kozi flani kisa umeskia ina ajira mana hicho chenye ajira hadi usome umalize ajira zake zaeka kupotea, Mfano zaman ilionekana sheria ina ajira sana watu wakakimbilia wakaisoma mwisho wa siku hazipo hivyo hivyo hata kwa walimu wa Arts na waliosemea petrolium Engineer. Kwahiyo soma kozi ambayo unauwezo nayo kwani swala la ajira nchini mwetu linaeza kwenda kupotea kabisa.

[HASHTAG]#MATOKEO[/HASHTAG]

Mwezi wa saba unaenda kupokea kile ambacho uliwahi kukipanda kwa miaka miwili. Yatakapo kuja mtokea yenye kukurusu kuendelea na degree au kwenda diploma basi zingatia hayo ya kuhusu chuo usije kosa kile ukipendacho. Yanapokuja vibaya jichunguze jee una uwezo wa kurudia tena ukaja fanya vizuri? Japo hili siliafiki kwan mara nyingi form six wanaporudia mitian ndo wanazidi haribu matokeo zaidi ya mwanzo. Unaeza kujieka kwenye Utafutaji mwingine na si lazima kusoma tena kwa hiyo miaka mi 3 au 4 mwenzako wanayokuwa chuo na kukutambishia boom wanaeza kuja mtaani wakakuomba push mana utakuwa uko mbali na mifano iko mingi juu ya hili. Ila juu ya hili lazima kujitoa na kuweka usharobaro usista duu pembeni.

Kila la heri katija kutimiza wajibu wako hapo dunia

NB: MENENO YANGU SI SHERIA
 
Ni ushauri mzuri ingawapo ingependeza zaidi kama ungefungua nyuzi mbili tofauti ya MIKOPO na ya pili juu ya UCHAGUZI wa VYUO.
 
Wale wote mliosoma private na mnataka mkopo jibu ndio hili tafuta mwenyekiti wa mtaa wako akuandikie barua kuwa wewe umesoma kwa msaada wa shirika furani inaweza tafuta shirika lolote lile ukaattach na barua yao

Jiongeze
 
Wale wote mliosoma private na mnataka mkopo jibu ndio hili tafuta mwenyekiti wa mtaa wako akuandikie barua kuwa wewe umesoma kwa msaada wa shirika furani inaweza tafuta shirika lolote lile ukaattach na barua yao

Jiongeze

Mkuu mimi niliomba mkopo nakufata vigezo kama vyako kuhusu mdhamini wangu ambaye aliandika barua ya kustaafu tokea 2014 na ikathibitishwa na serikali za mtaa chini ya mwenyekiti kuwa nilisomeshwa na mdhamini tokea form1 mpka 4 nikachaguliwa kuendelea na 5-6 kwenye shule za Serikali lakini mpaka saivi sijapata(sio mnufaika wa mkopo japokuwa copy zangu zote zilipigwa muhuri na ngazi izo mfano barua ya mstaafu(mdhamini na barua ya kujielezea kuwa amestaafu na kushindwa kulipia chuo kikuu) mpaka saivi nashukuru tumefunga mkanda na wazazi wanalipa kidogo kidogo ila pengine mkopo ni bahati.
 
Back
Top Bottom