VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Suala la Forbes limewatofautisha viongozi waandamizi wa CCM na kupelekea mkutano na waandishi wa habari kuahirishwa. Mkutano huo na waandishi wa habari ulilenga kutoa uchambuzi wa kiindi cha waka mmoja wa Serikali ya Awamu ya tano iliyo chini ya Rais Dr. John P. Magufuli. Ilipangwa kusifu kila idara na kuwaomba wananchi wamuunge mkono Rais Magufuli.
Nyaraka za mkutano huo na waandishi wa habari zinaonesha kuwa CCM imeuchambua mwaka huo na kwa ujumla, kumemiminwa sifa za kutosha na kutisha. Pia, CCM ilipanga kugusia mwenendo wa chama kwa ujumla kwa kudurusu kesi mbalimbali za uchaguzi zilizopo mahakamani kwa sasa na hata Uchaguzi wa Meya wa Kinondoni na Ubungo.
CCM pia ililenga kuzungumzia 'kuongoza' kwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dr. Magufuli kwenye shindano la 'Mtu Mahiri Afrika wa mwaka 2016' linalosemekana kuendeshwa na Forbes. Suala hilo limewagawa viongozi waandamizi chamani hapa Ofisi Ndogo za Lumumba na kupelekea kuchafuka kwa hali ya hewa kwa muda. Suluhisho lilikuwa ni kuahirisha Mkutano na waandishi wa habari.
Eti mambo ya mitandao inaahirisha Press Conference! PC ni kesho saa tano asubuhi hapa hapa Lumumba!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam!