Fomula za Masikini na Tajiri

Nimefanikiwa kusoma Uzi wote..,nilitaka nisome robo Ila nikaona mbali kama tajiri...nikasoma nikamaliza....
 
Lakini Mwisho Wa Siku Wote Tutaachana na Dunia na Kurudi Mavumbini.
 
Lakini Mwisho Wa Siku Wote Tutaachana na Dunia na Kurudi Mavumbini.
Huu ni ukweli na hakuna asiyejua kwamba siku moja atakufa, kufanya kazi, kutafuta maarifa na kufanya mema ni nguzo hapa duniani. Hata Mungu amesisitiza hayo mambo, duniani tunapita ila tusiishi hapa (duniani) kwa shida, ubaya, roho mbaya na kwa uzembe kisa tu tunapita. Masikini na tajiri hata Mungu anatutambua na tunategemeana kwa kiasi kikubwa sana. Mwisho wa siku, lazima tuishi kwa kujituma na kupambana bila kumkwaza mtu yeyote na zaidi kumpendeza Mungu.
 
Mkuu Bob umetisha sana' ulichoongea ni fact tupu' Maisha ni kanuni, na kanuni hizo ndo zitakufanya uwe maskini au tajiri
 
Umenena mkuu! Jamani eti zaa watoto mpaka waishe kiunoni Mungu atawalinda.
 
Maisha hayana formula acheni kupotosha watu
Inawezekana umeona formula kwa usomaji wako. Kilichoandikwa hapo ni tabia za watu wa matabaka tofauti namna akili na utendaji wao ulivyo tofauti katika utafutaji wa mafanikio hapa duniani.
 
dah we jamaa huna ulipokosea kila kitu umepatia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…