Fomu za Uongozi CHADEMA hizi hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fomu za Uongozi CHADEMA hizi hapa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MAMA POROJO, Jul 22, 2010.

 1. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Taifa la Tanzania halitaongozwa tena na wapiga ramli na washirikina.


  Kiongozi mzuri ni wewe chukua hatua sasa, fomu za uongozi kupitia chama BORA zipo hapa chini
  .
   
 2. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Thanx man,kuna vigezo vya aina gani kwa watu wanogombea udiwanican anyone please assist me?
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  Sifa na Masharti ya Mgombea Udiwani

  Sifa za mgombea Udiwani

  • Awe raia wa Tanzania


  • Awe na umri usiopungua miaka 21


  • Awe mkazi wa eneo la Halmashauri inayohusika


  • Awe anaweza kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza


  • Awe mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na Chama cha Siasa


  • Awe na kipato halali kinachomwezesha kuishi


  • Awe hajatiwa hatiani na Mahakama yoyote kwa kosa la kukwepa kulipa kodi katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi

  Kupoteza sifa za kuwa mgombea
  Hata kama mtu ana sifa zote zilizotajwa hapo juu haruhusiwi kugombea Udiwani kama:-

  1. Ana uraia wa nchi nyingine
  2. Amethibitika kisheria kwamba hana akili timamu
  3. Amehukumiwa kifo na Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa ya Tanzania
  4. Anatumikia hukumu ya kifungo cha zaidi ya miezi sita
  5. Yumo kizuizini kwa mujibu wa Sheria ya kuwaweka watu kizuizini ya mwaka 1962
  6. Yuko uhamishoni, kwa zaidi ya miezi sita kwa mujibu wa Sheria ya Uhamishoni (Deportation Ordinance)
  7. Ni mfanyakazi wa Halmashauri inayohusika au Serikali ya Jamhuri ya Muungano isipokuwa yule ambaye ameruhusiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa kifungu cha 40(1)(f) cha Sheria ya Uchaguzi namba 4/79
  8. Kama amezuiliwa na Sheria yoyote nchini kujiandikisha kuwa mpiga kura
  9. Ana maslahi katika Halmashauri au Kampuni yenye mkataba na Halmashauri na hajatangaza kwenye gazeti juu ya maslahi hayo
  Masharti ya Uteuzi wa Mgombea Udiwani

  1. Awe amedhaminiwa na watu wasiopungua kumi walioandikishwa kupiga kura katika Kata.
  2. Awe amekula kiapo mbele ya hakimu kuthibitisha kwamba anazo sifa zinazotakiwa kugombea Udiwani na kujaziwa fomu ya uteuzi namba 8C.
  3. Awe na dhamana ya Shilingi Elfu tano (5,000/=).
   
 4. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Utoaji wa Fomu za Uteuzi kwa Wagombea Udiwani

  1. Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatoa fomu chache Makao Makuu ya kila chama cha Siasa kilichopata usajili kamili kwa taarifa.
  2. Wasimamizi wa Uchaguzi watatumiwa fomu kwa ajili ya kuwapa Wagombea. Wagombea watakaopatiwa fomu kutoka kwa Wasimamizi wa Uchaguzi au Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ni wale tu ambao watawasilisha uthibitisho wa maandishi kwamba wao ndio waliopendekezwa na vyama vyao kugombea udiwani katika Kata inayohusika.
  Fomu ya uteuzi namba 8C itatolewa kwa wagombea udiwani ikionyesha:-

  1. Idadi ya wapiga kura waliomdhamini Mgombea
  2. Tamko la kisheria la Mgombea
  3. Maelezo binafsi ya Mgombea
  4. Uthibitisho kuwa amelipa dhamana ya shilingi elfu tano (5,000/=).
  Kila Mgombea atapewa nakala nne za kila moja ya fomu hizo.

  Akishapatiwa fomu hizo afanye yafuatayo:

  1. Apate watu wasiopungua 10 atakaomdhamini kwa kumjazia nakala nne za Fomu ya uteuzi. Watu hao sharti:-

  1. Wawe wamejiandikisha kuwa wapiga kura katika Kata anayogombea
  2. Wawe hawajamdhamini mgombea mwingine wa Udiwani
  Si lazima wawe ni wanachama wa Chama kilichompendekeza; wala si lazima wawe wanachama wa Chama chochote cha siasa.

  1. Aapishwe na hakimu akiwa na nakala zote nne za Fomu ya uteuzi ili kuthibitisha kwamba ana sifa za kugombea udiwani.
  2. Alipe dhamana na shilingi Elfu tano (5,000) fedha taslimu kwa Msimamizi wa Uchaguzi.
  Uwasilishaji wa Fomu ya Uteuzi
  Wagombea Uchaguzi wa Udiwani wawasilishe fomu za uteuzi, picha za rangi zenye ukubwa wa 'post card' ("3x4") na dhamana ya shilingi elfu tano (5,000/=) kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi katika ofisi yake.

  1. Fomu zinaweza kuwasilishwa na mgombea mwenyewe au yeyote kati ya watu 10 waliomdhamini.
  2. Fomu hizo sharti ziwasilishwe kabla ya saa kumi (10.00) jioni ya siku ya Uteuzi.
  Dokezo: Mgombea akipenda anaweza kurudisha fomu zake kuanzia siku tatu kabla ya siku ya uteuzi iliyopangwa na Tume lakini uteuzi kamili utafanywa siku ya uteuzi.
  Ukaguzi wa Fomu

  1. Msimamizi wa Uchaguzi atazikagua Fomu ya uteuzi pamoja na viambatisho vyake.
  2. Mgombea ahakikishe kwamba nyuma ya picha hizo ameandika jina lake, Kata anayogombea, na chama kilichompendekeza. Jambo hilo ni muhimu sana ili katika karatasi za kura picha ya mgombea 'X' isipewe jina la mgombea 'Y'
  Kubandika Fomu ya Uteuzi
  Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atabandika kwenye ubao wa matangazo mahali pa wazi nje ya ofisi ya Kata nakala moja moja ya fomu zote na picha ili ziweze kukaguliwa.
  Uteuzi wa Wagombea
  Siku ya Uteuzi
  Siku ya Uteuzi wa Wagombea Urais, Ubunge na Udiwani hupangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Wagombea uchaguzi katika ngazi zote sharti wawe ni wanachama wa Chama cha Siasa na wawe wamependekezwa na Vyama vya Siasa kwa maandishi. Kwa uchaguzi wa mwaka 2005 uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 20 Agosti 2005.
  Mamlaka zitakazoshughulikia uteuzi wa wagombea ni kama ifuatavyo:

  1. Mgombea Urais na Umakamu wa Rais - Tume ya Taifa ya Uchaguzi
  2. Mgombea Ubunge - Msimamizi wa Uchaguzi
  3. Mgombea Udiwani - Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi
  Wajibu wa Vyama vya Siasa, Wagombea na Mawakala
  Wajibu wa Vyama vya Siasa

  1. Wajibu wa Vyama vya Siasa ni kupendekeza wagombea wa Vyama vyao. Ni vizuri Vyama navyo vijiridhishe kwamba wagombea wanaowapendekeza wanazo sifa zote zinazotakiwa kwa mujibu wa Sheria. Chama kikishampendekeza mgombea kimpatie mgombea huyo barua ya kumtambulisha rasmi kwa Msimamizi wa Uchaguzi. Vyama ambavyo vina mgawanyiko wa uongozi, vihakikishe kwamba fomu za mgombea wao zinatiwa saini na viongozi wa kitaifa kwa wanaogombea nafasi ya Ubunge na Uongozi wa Mkoa kwa upande wa Wagombea Udiwani ngazi ya Kata. Uongozi wa kitaifa ni ule unaotambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.
  Wajibu wa Wagombea

  1. Kuhakikisha na kujiridhisha kwamba wanazo sifa zote zinazotakiwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Uchaguzi, na kwamba hawajaondokewa na sifa yoyote.
  2. Kuelewa barabara aina za fomu zote zinazohitajika kwa uteuzi rasmi; zinapatikana wapi na kwa masharti gani; zinatakiwa kurudishwa lini, wapi na kwa masharti gani. Fomu zinapatikana kwa Msimamizi wa Uchaguzi na zinarudishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi au Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Zile zinazohusu uchaguzi wa Wabunge na Madiwani zinarudishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi na zile zinazohusu uchaguzi wa Rais zinarushwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
  3. Kuzielewa haki zao, pamoja na masharti na utaratibu wa uteuzi. Haki hizo ni pamoja na kutoa pingamizi kwa Msimamizi wa Uchaguzi dhidi ya uteuzi wa mgombea yeyote, na kukata rufaa kwa Tume dhidi ya uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi kuhusu pingamizi.
  Utaratibu wa kushughulikia wapigia kura wanaodhamini mgombea zaidi ya mmoja
  Mpiga kura aliyeandikishwa, ataruhusiwa kumdhamini mgombea mmoja kwa kila uchaguzi. Kwa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani mpiga kura mmoja anapodhamini zaidi ya mgombea mmoja kwa kila uchaguzi na wagombea hao wakateuliwa na Msimamizi wa Uchaguzi, udhamini huo hautabatilisha uteuzi wa wagombea waliodhamini isipokukwa itakuwa ni kosa la jinai kwa mpiga kura aliyedhamini wagombea hao.

  Mpiga kura aliyedhamini mgombea zaidi ya mmoja akikubali kosa kwa maandishi, Msimamizi wa Uchaguzi anawaweza kutoa adhabu ya kumtoza faini isiyozidi Shs 200,000/=. Mpiga kura akikataa shauri hilo litapelekekwa Mahakamani na Msimamizi wa Uchaguzi.
   
 5. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Pingamizi dhidi ya Uteuzi wa Mgombea Ubunge

  Wanaoruhusiwa kutoa pingamizi

  1. Mgombea yeyote wa Jimbo la Mgombea anayepingwa
  2. Mkurugenzi wa Uchaguzi
  3. Msimamizi wa Uchaguzi

   Mtu mwingine yeyote haruhusiwi
  Muda wa kutoa pingamizi
  Baada ya saa kumi (10.00) jioni ya siku ya uteuzi, mpaka saa kumi (10.00) jioni ya siku inayofuata

  Sababu za pingamizi
  Sababu ya pingamizi inaweza kuwa yoyote kati ya zifuatazo:

  1. Maelezo yaliyopo katika fomu ya uteuzi hayatoshi kumtambulisha mgombea;
  2. Fomu ya uteuzi haitimizi au haikuwasilishwa kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Sheria;
  3. Kutokana na maelezo yaliyoandikwa katika Fomu ya uteuzi ni dhahiri kwamba Mgombea Uchaguzi hana sifa zinazotakiwa;
  4. Uthibitisho wa Msimamizi wa Uchaguzi unaopaswa kutolewa haukutolewa;
  5. Mgombea hana sifa zote zinazohitajika;
  6. Hakuna picha ya mgombea;
  7. Hakuna uthibitisho kuwa mgombea amelipa dhamana ya shilingi Elfu hamsini (50,000/=)
  Utaratibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Kutoa Pingamizi
  Kwa mujibu wa kifungu cha 40(5) cha Sheria ya Uchaguzi namba 1/85 endapo Msimamizi wa Uchaguzi atakuwa na pingamizi dhidi ya mgombea, ataweka pingamizi na kumwarifu Mgombea kwa maandishi kabla ya kutoa uamuzi wake. Kama mgombea ana maelezo atayawasilisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi. Baada ya Msimamizi wa Uchaguzi kutoa uamuzi atawasilisha uamuzi wake Tume ya Taifa ya Uchaguzi akiambatisha maelezo ya mgombea.

  Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi
  Kabla ya kutoa uamuzi juu ya pingamizi, Msimamizi wa Uchaguzi atamjulisha mgombea nayepingwa ili aweze kuitolea maelezo kama atakuwa nayo. Baada ya kupata taarifa za pande zote, Msimamizi wa Uchaguzi anaweza kuendelea kutoa uamuzi wake. Hata kama anayepingwa hatatoa majibu, Msimamizi wa Uchaguzi anaweza kutoa uamuzi wake.

  Rufaa dhidi ya pingamizi

  1. Msimamizi wa Uchaguzi atamweleza aliyetoa pingamizi, kukata rufaa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi endapo hakuridhika na uamuzi wa Msimamimzi wa Uchaguzi katika muda wa saa 48 tangu kutolewa kwa uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi. Rufaa itawasilishwa kwa kutumia Fomu namba 12.
  2. Msimamizi wa uchaguzi atapokea rufani hizo na kuziwasilisha Tume pamoja na maelezo yake.
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135


  Kipindi cha Kampeni

  Kwa mujibu wa Sheria, kipindi cha kampeni hutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kipindi hiki cha kampeni ni kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani. Kampeni huanza siku moja baada ya siku ya uteuzi na humalizika siku moja kabla ya uchaguzi.

  Wajibu wa Vyama au Wagombea na Mawakala

  Wakati wa kampeni, Vyama vya Siasa vinatakiwa kueleza sera zao na kunadi Wagombea wao kwa kuzingatia Sheria za uchaguzi, Kanuni na Maadili ya Uchaguzi. Kwa mujibu wa kifungu cha 51(2) cha Sheria ya Uchaguzi namba 1/85 na kifungu cha 53(1)(b) cha Sheria ya Uchaguzi wa Madiwani namba 4/79 jukumu la kuendesha kampeni za uchaguzi ni la Mgombea, Chama cha Siasa cha Mgombea au Wakala wa Mgombea. Hivyo basi kila Mgombea, Chama cha Siasa au Wakala anatakiwa apange ratiba yake ya kampeni na kuiwasilisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi tayari kwa kuoanishwa na ratiba nyingine za Wagombea au Vyama vya Siasa au Mawakala.
  Kwa upande wa Uchaguzi wa Rais, ratiba za Kampeni zitaratibiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi. Hivyo Vyama vya Siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi wa Rais vitawasilisha mapendekezo ya ratiba za mikutano ya Kampeni. Mapendekezo hayo yataonyesha tarehe, muda, mkoa na wilaya. Mkurugenzi wa Uchaguzi baada ya kupokea mapendekezo hayo ataitisha mkutano wa Wakilishi wa Vyama vinavyoshiriki uchaguzi wa Rais ili kujadiliana na kuratibu ratiba hiyo. Nakala ya ratiba hiyo itapelekwa kwa:

  • Vyama vya Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi wa Rais
  • Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa
  • Mkuu wa Mkoa
  • Inspekta Jenerali wa Polisi kwa ajili ya kuandaa taratibu za usalama
  Vyama vya Siasa vinatakiwa kuzingatia ratiba hiyo kikamilifu. Pamoja na ratiba hiyo, Vyama vya Siasa vinaruhusiwa wakati wa kipindi cha kampeni kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba.
  Wajibu wa Msimamizi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi

  Wajibu wa Msimamizi wa uchaguzi ni kuvitaka Vyama vya siasa viwasilishe mapendekezo ya ratiba wakionyesha tarehe, mahali na saa ya kufanya mikutano ya kampeni. Baada ya hapo msimamizi wa uchaguzi ataitisha mkutano wa vyama kujadili ratiba zao ili kumwezesha Msimamizi wa Uchaguzi kuandaa ratiba rasmi ya mikutano ya kampeni. Msimamizi wa uchaguzi atampatia Mkuu wa Wilaya na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ratiba hiyo kwa ajili ya ulinzi katika mikutano. Vyama vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi navyo vipatiwe nakala ya ratiba hiyo.

  Maelekezo ya Jumla
  1. Ni marufuku kwa mgombea, Chama cha Siasa au Wakala, kufanya kampeni siku ya Uchaguzi. Mpiga kura au mtu mwingine yeyote haruhusiwi kwenda katika kituo cha kupigia kura na alama au vazi au bango linaloashiria kukipigia kampeni chama fulani au Mgombea.
  2. Endapo Vyama vya Siasa, au mgombea yeyote atahitaji kutumia mabango au vipeperushi vyenye matangazo ya kampeni, aombe kwa Msimamizi wa Uchaguzi kwa ajili ya kupata idhini. Kwa upande wa Uchaguzi wa Rais maandishi hayo yapate kibali cha Tume ya Uchaguzi. Mabango ambayo hayajaidhinishwa na mamlaka husika hayaruhusiwi kutumika katika kampeni.
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  Taratibu za Upigaji Kura


  Wajibu wa Vyama vya Siasa katika kupanga Vituo vya Kupigia Kura na Uteuzi wa Wasimamizi wa Vituo

  1. Kupanga Vituo
  Msimamizi wa Uchaguzi atavipatia Vyama vya Siasa orodha ya vituo anavyotarajia kuvitumia kwa ajili ya upigaji kura. Vyama vya Siasa vina haki ya kutoa maoni kuhusu mahali vilipo vituo hivyo.

  1. Uteuzi wa Wasimamizi wa Vituo
  Msimamizi wa Uchaguzi atatangaza kwenye ubao wa matangazo mahali pa wazi nje ya ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi orodha ya majina ya watu anaotarajia kuwateua kama Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura. Vyama vya Siasa vina haki ya kuota pingamizi kama wanazo dhidi ya jina lolote lililomo katika orodha hiyo kaika siku nne toka Msimamizi wa Uchaguzi alipotangaza orodha hiyo.
  Msimamizi wa Uchaguzi atakuwa na uamuzi wa mwisho katika kuteua Wasimamizi wa vituo.
  Haki ya kuteua Mawakala
  Kila Chama cha Siasa, baada ya kushauriana na Wagombea, kina haki ya kuteua Wakala mmoja kwa kila kutuo cha kupigia kura. Ni vema Mawakala wapangwe vituo vya upigaji kura ndani ya kata wanakoishi ili waweze kuangalia vizuri maslahi ya wagombea. Majina ya Mawakala, anuani zao na vituo walivyopangiwa yawasilishwe kwa Msimamizi wa Uchaguzi siku saba kabla ya siku ya kupiga kura.

  Vyama au Wagombea kushuhudia ugawaji wa vifaa

  1. Vifaa vinavyotumika siku ya kupiga kura vitakabidhiwa kwa Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura mbele ya Mgombea au Wawakilishi wao.
  2. Chama kitapatiwa orodha kamili ya vifaa muhimu vitakavyotolewa kwa kila kituo vikiwemo, namba za masanduku ya kura, idadi ya namba za karatasi za kura.
  Mafunzo kwa Mawakala
  Vyama vya Siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi vitawajibika kutoa mafunzo kwa Mawakala kwa gharama zao.

  Wajibu wa Mawakala
  Mawakala wa Upigaji kura wana wajibu ufuatao:-

  1. Kuhakikisha kwamba anayepiga kura ndiye aliyejiandikisha
  2. Kushirikiana na Msimamizi wa kituo cha kupigia kura katika kuhakikisha kwamba upigaji kura unafanywa kwa kuzingatia sheria
  3. Kulinda maslahi ya mgombea anayemwakilisha kituoni.
  Hata hivyo kutokuwepo kwa wakala wa upigaji au kuhesabu kura kituoni hakutazuia wala kubatilisha shughuli yoyote itakaoendeshwa kwa mujibu wa Sheria.
  Mawakala waliojiandikisha kupiga kura, ambao watapangwa katika vituo ambavyo hawakujiandikisha kupiga kura, wanaweza kumjulisha Msimamizi wa Uchaguzi mapema kabla ya siku ya uchaguzi ili awapatie shahada za utumishi.
  Mawakala wanawajibika kujaza fomu zote ambazo zimewekwa kisheria ili kuonyesha kuridhika au kutoridhika na mwenendo wa uchaguzi. Fomu hizo ni namba 14 na 16.
  Kwa mujibu wa maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mawakala wa upigaji au kuhesabu kura watakaosimamia vituo vya mwisho ambako misafara ya kukusanya masanduku na vifaa vingine itaanzia, ndio pia watakaosindikiza na watakaoshuhudia makabidhiano ya vifaa hivyo kwenye kituo cha kujumlisha kura.

  Kiapo cha Kutunza Siri
  Kwa mujibu wa kifungu cha 93(1) cha Sheria ya Uchaguzi namba 1/85 na kifungu cha 92(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Madiwani namba 4/79 Mawakala wa upigaji kura wanatakiwa kula kiapo cha kutunza siri mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi. Kila Chama au Mgombea ahakikishe kuwa Mawakala wake wanakula kiapo kabla ya siku ya uchaguzi.
  Mawakala wanaruhusiwa kuwepo katika vituo vya kupiga kura walivyopangiwa tangu mwanzo wa hatua za upigaji kura hadi matokeo ya uchaguzi katika kituo hicho yatakapotangazwa ili waweze kutekeleza majukumu yaliyotajwa. Hata hivyo, kisheria shughuli za upigaji kura zitaendelea hata kama Mawakala hawatakuwepo. Mawakala hao watagharamiwa na vyama vyao.

  Wanaoruhusiwa kuwepo katika kituo cha kupigia kura

  1. Msimamizi wa Kituo
  2. Msimamizi Msaidizi wa Kituo
  3. Wakala
  4. Mpiga kura
  5. Mtu anayemsaidia mpiga kura asiyeweza kupiga kura mwenyewe kwa sababu ya ulemavu au asiyejua kusoma
  6. Mtazamaji wa Uchaguzi aliyeidhinishwa na Tume, kwa maandishi
  7. Mjumbe wa Tume
  8. Mkurugenzi wa Uchaguzi
  9. Afisa wa Tume
  10. Msimamizi wa Uchaguzi na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi
  11. Askari wa Polisi au Mlinzi wa Kituo
  Kabla ya upigaji kura kuanza Mawakala au Wagombea waliopo watalazimika kujaza Fomu namba 14 kuonyesha kuridhika au kutokuridhika na maandalizi ya kituo cha upigaji kura.
  Baada ya upigaji kura kukamilika Mawakala au Wagombea watajaza tena fomu namba 14 kuonyesha kuridhika au kutokuridhika kwao na mwenendo wa upigaji kura.

  Shahada ya Utumishi / Maalumu
  Watendaji na Mawakala ambao kutokana na majukumu yao katika uchaguzi hawataweza kupiga kura katika vituo walivyopangiwa watapatiwa Shahada za Utumishi ili waweze kupiga kura katika vituo watakapofanyia kazi. Endapo mtendaji au Wakala anayehusika atapangiwa kufanya kazi kwenye kata nyinigne ambako hakujiandikisha hatapiga kura ya Diwani. Vilevile atakayepangiwa nje ya jimbo alipojiandikisha hatapiga kura ya Mbunge wala Diwani bali atapiga kura ya Rais tu.
  Wagombea watapatiwa Shahada Maalumu ambazo zitawawezesha kupiga kura katika kituo chochote katika Kata kwa Mgombea Udiwani au Jimbo kwa Mgombea Ubunge. Endapo Mgombea Ubunge atahitaji kupiga kura katika kata ambako hakujiandikisha hatapiga kura ya Diwani.

  Mambo yasiyoruhusiwa kufanyika siku ya kupiga kura

  1. Hairuhusiwi kufanya kampeni ya aina yoyote
  2. Kuvaa sare au alama za chama, kubeba au kubandika matangazo na kuimba nyimbo za vyama
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Utaratibu wa Kuhesabu Kura

  Zoezi la kuhesabu kura kwa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani litafanyika katika vituo vya kupiga kura isipokuwa kutokana na sababu za kiusalama Msimamizi wa Kituo baada ya kushauriana na Msimamizi wa Uchaguzi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi au Mawakala anaweza kuamua kura zihesabiwe mahali pengine. Lakini katika kuhesabu kura itahakikishwa kwamba hazitachanganywa na hesabu ya kura za vituo vingine.
  Zoezi la kuhesabu kura litafanywa kwa mpangilio ufuatao:- Kura za Rais ndizo zitakazohesabiwa kwanza na zitakazofuatia ni kura za Wabunge na mwisho zitahesabiwa kura za Madiwani.

  Dokezo
  Msimamizi wa kituo atakamilisha kujaza Fomu namba 13 atakapokamilisha hesabu ya kura kwa masanduku yote. Wakati wa kuhesabu kura, endapo atakuta kuro yoyote imo katika sanduku ambalo sio la Uchaguzi huo ataihamishia na kuihesabu katika sanduku la uchaguzi unaohusika.

  Wanaoruhusiwa kuwepo katika kituo cha kuhesabu kura

  1. Msimamizi wa Kituo
  2. Msimamizi Msaidizi wa Kituo
  3. Wakala wa Kuhesabu Kura
  4. Mgombea
  5. Askari wa Polisi au Mlinzi wa Kituo
  6. Msimamizi wa Uchaguzi na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi
  7. Mratibu wa Uchaguzi wa Mkoa
  8. Mjumbe wa Tume
  9. Mkurugenzi wa Uchaguzi
  10. Afisa Uchaguzi
  11. Mtazamaji wa Uchaguzi aliyeidhinishwa na Tume ya Uchaguzi kwa maandishi
  Baada ya Upigaji Kura kukamilika:

  1. Mawakala wa upigaji kura watabadilika na kuwa mawakala wa kuhesabu kura
  2. Wasimamizi wa Vituo na Wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya kupigia kura ndio watakaohesabu kura
  3. Wakati wa kuhesabu kura, mawakala au wagombea waliopo wana haki ya kuomba kura zirudiwe kuhesabiwa hadi mara mbili. Kwa mara ya tatu, Msimamizi wa kituo atakataa ombi la tatu endapo hesabu ya mara ya kwanza na ya pili zililingana.
  Baada ya zoezi la kuhesabu kura kukamilika Mawakala au Wagombea watajaza Fomu namba 16 kuonyesha kama wameridhika au hawaridhiki na mwenendo mzima wa kuhesabu kura.

  Matokeo ya Uchaguzi katika Kituo
  Matokeo ya Uchaguzi kwa kila kituo yataandikwa kwenye fomu zifuatazo na kutiwa sahihi ya Mawakala au Wagombea watakaokuwepo pamoja na Msimamizi wa Kituo na kubandikwa nje ya kituo cha kupiga kura:-

  1. Uchaguzi wa Rais - Fomu namba 21A
  2. Uchaguzi wa Wabunge - Fomu namba 21B
  3. Uchaguzi wa Madiwani - Fomu namba 21C
  Mawakala au Wagombea watakaokataa kutia saini Tamko kwenye fomu hizo watatakiwa kutoa sababu za kukataa kwa maandishi, Kwa Msimamizi au Msimamizi Msaidizi wa kituo.

  Mawakala au wagombea watakaokuwepo watapatiwa nakala za Fomu za matokeo ya uchaguzi kwa kila uchaguzi

  Wakala mmoja wa kituo cha mbali zaidi wa kila chama kwa kila kata ndiye atakayesindikiza masanduku ya kura zilizokwishahesabiwa na fomu za matokeo ya uchaguzi hadi kwa Msimamizi au Msimamizi Msaidizi katika Jimbo au Kata.
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ujumlishaji wa Kura

  Wanaoruhusiwa kuwepo katika kituo cha kujumlishia kura kwa Uchaguzi wa Rais na Wabunge ni

  1. Msimamizi wa Uchaguzi
  2. Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi
  3. Mratibu wa Uchaguzi wa Mkoa
  4. Mjumbe wa Tume
  5. Mkurugenzi wa Uchaguzi
  6. Afisa wa Tume
  7. Mgombea au Wakala wake
  8. Askari wa Polisi au Mlinzi wa Kituo
  9. Mtazamaji wa Uchaguzi aliyeidhinishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa maandishi

  Ujumlishaji wa Kura kwa Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jimbo

  1. Ujumlishaji wa kura kwa uchaguzi wa Rais na Bunge utafanyika Makao Makuu ya Jimbo
  2. Msimamizi wa Uchaguzi atawaarifu wagombea siku, mahali na saa atakayofanya ujumlishaji wa kura
  3. Msimamizi wa Uchaguzi atapokea masanduku, fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais na Bunge kutoka kwenye vituo vyote vya kupigia kura vilivyomo katika Jimbo.
  4. Ujumlishaji wa kura utaanza mara baada ya masanduku yote ya kura na fomu za matokeo kuwasilishwa kwenye kituo cha kujumlishia kura

  Kabla ya kuanza ujumlishaji Msimamizi wa Uchaguzi atafanya yafuatayo:

  1. Atatoa taarifa kuhusu matukio muhimu
  2. Atawapa Wagombea au Mawakala wao nafasi ya kutoa taarifa kuhusu matukio mengine muhimu ambayo hayakutajwa na Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi
  3. Atazitolea uamuzi kura zenye mgogoro
  4. Atatangaza kwa sauti kubwa matokeo ya kituo kimoja kimoja kwa vituo vyote vya kupigia kura katika jimbo

  Matokeo ya Uchaguzi wa Rais katika Jimbo

  1. Msimamizi wa Uchaguzi atajumlisha kura za Rais na atakapomaliza atajaza matokeo hayo ya jimbo katika Fomu namba 24A. Msimamizi wa uchaguzi na Mawakala au Wagombea watakaokuwepo wataweka saini zao nyuma ya fomu hiyo
  2. Msimamizi wa Uchaguzi atampatia Wakala au Mgombea nakala ya matokeo ya Uchaguzi katika jimbo
  3. Atabandika nakala ya Fomu namba 24A katika ubao wa matangazo
  4. Msimamizi wa Uchaguzi atawasilisha haraka sana matokeo hayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi

  Matokeo ya Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo
  Baada ya kukamilisha ujumlishaji wa Kura za Rais, Msimamizi wa Uchaguzi atafanya ujumlishaji wa Kura za Wabunge hatua kwa hatua na atakapomaliza ujumlishaji atafanya yafuatayo:

  1. Atajaza matokeo ya Uchaguzi ya Jimbo kwenye fomu namba 24B. Msimamizi wa Uchaguzi na Mawakala au Wagombea watakaokuwepo wataweka saini zao
  2. Atamtangaza Mgombea aliyeshinda na kumpatia hati ya kuchaguliwa
  3. Atabandika nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi katika ubao wa matangazo
  4. Atawasilisha matokeo haraka iwezekanavyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi

  Uchaguzi wa Madiwani

  1. Ujumlishaji wa kura kwa uchaguzi wa Madiwani utafanyika kwenye Kata
  2. Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atawaarifu Wagombea siku, mahali na saa atakayoanza ujumlishaji wa kura za madiwani
  3. Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi wa kata atapokea masanduku ya kura na fomu za matokeo ya uchaguzi kutoka kwenye vituo vya kupigia kura
  4. Ujumlishaji wa kura utaanza mara baada ya masanduku yote ya kura na fomu za matokeo kuwasilishwa kwenye kituo cha kujumlisha kura
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ujumlishaji wa Kura (Madiwani)

  Wanaoruhusiwa kuwepo katika kituo cha kujumlishia kura kwa Uchaguzi wa Diwani ni:

  1. Msimamizi wa Kituo
  2. Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi
  3. Mratibu wa Uchaguzi wa Mkoa
  4. Mjumbe wa Tume
  5. Mkurugenzi wa Uchaguzi
  6. Afisa wa Tume
  7. Mgombea Udiwani au Wakala wake
  8. Askari wa Polisi au Mlinzi wa Kituo
  9. Mtazamaji wa Uchaguzi aliyeidhinishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa maandishi

  Kabla ya kuanza ujumlishaji:-

  1. Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atatoa taarifa ya matukio muhimu
  2. Atazitolea uamuzi kura zenye mgogoro
  3. Atatangaza kwa sauti kubwa matokeo ya kituo kimoja kimoja kwa vituo vyote vya kupigia kura vilivyomo kwenye Kata

  Baada ya hapo atajumlisha kura na mara atakapomaliza atajaza matokeo katika fomu namba 24C na kuweka saini yake. Mawakala waliopo wataweka saini zao.

  1. Atampatia Mgombea au Wakala atakayekuwepo nakala ya matokeo ya uchaguzi wa kwenye Kata
  2. Atamtangaza Mgombea aliyeshinda na kubandika nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi katika ubao wa matangazo
  3. Atamtaarifu rasmi Mgombea aliyeshinda na kumpatia hati ya kuchaguliwa
  4. Atawasilisha taarifa zote, masanduku ya kura na matokeo ya Uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi
  5. Msimamizi wa Uchaguzi atatuma matokeo ya Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara moja.

  Ujumlishaji wa Kura za Uchaguzi wa Rais kwa nchi nzima
  Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndiyo itakayojumlisha Kura za nchi nzima za Uchaguzi wa Rais
  Tume ya Taifa ya Uchaguzi itawajulisha Wagombea siku, mahali na saa itakapofanya ujumlishaji wa kura za Wagombea Urais baada ya kupokea matokeo ya uchaguzi wa Rais kutoka kwenye majimbo yote ya Uchaguzi. Tume itahakiki na kutangaza matokeo hayo kadri yatakavyokuwa yanapokelewa kutoka kwenye majimbo.  Wanaoruhusiwa kuingia mahali pa kujumlishia kura

  1. Mjumbe wa Tume
  2. Mkurugenzi wa Uchaguzi
  3. Afisa wa Tume
  4. Mgombea
  5. Wakala wa Chama
  6. Askari wa Polisi au Mlinzi wa Kituo
  7. Mtazamaji wa Uchaguzi aliyeidhinishwa na Tume kwa maandishi
  8. Mtu mwingine yeyote aliyeidhinishwa na Tume, kwa maandishi
  Kabla ya kuanza ujumlishaji Tume ya Taifa ya Uchaguzi itafanya yafuatayo:

  1. Itatoa taarifa kuhusu matukio muhimu
  2. Itawapa nafasi wagombea ya kutoa taarifa za matukio yaliyotokea wakati wa upigaji kura
  3. Itatangaza kwa sauti matokeo ya uchaguzi wa Rais kutoka majimbo yote ya uchaguzi kuanzia jimbo la kwanza hadi la mwisho
  Tume ya Taifa ya Uchaguzi itajumlisha matokeo ya kura za majimbo yote na itakapomaliza ujumlishaji itajaza matokeo ya kila Mgombea katika Fomu namba 27. Mwenyekiti wa Tume, Wagombea au Mawakala watakaokuwepo wataweka saini zao kwenye fomu hiyo.


  Kumtangaza Mshindi wa Uchaguzi wa Rais
  Tume itatangaza idadi ya kura alizopata kila Mgombea na Mgombea aliyepata kura nyingi zaidi atatangazwa kuwa mshindi wa kiti cha Urais na Tume itampatia hati ya kuchaguliwa.
   
 11. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  Viti Maalumu vya Wabunge Wanawake


  Kulingana na Ibara Na. 66 na 78 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 Vyama vya Siasa vitapendekeza kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi majina ya wanawake ambao Tume inaweza kuwatangaza kuwa Wabunge kama ikiridhika kwamba wana sifa zinazostahili.

  Tume inatakiwa kutangaza majina ya wanawake kwa idadi isiyopungua asilimia 30 ya Wabunge wote kwa ajili ya viti maalumu kwa wanawake. Mgawanyo huo utazingatia uwiano wa kura ambazo kila chama kimepata katika uchaguzi wa Bunge. Endapo mgombea ubunge amepita bila kupingwa, kura za mgombea Urais wa chama cha mbunge zitachukuliwa kuwa ndizo kura halali za mbunge huyo. Kama hakina mgombea Urais, asilimia 51 ya idadi ya wapiga kura walioandikishwa zitachukuliwa kuwa ndizo kura halali za mbunge wa chama husika. Hata hivyo, chama kinaweza kupata nafasi ya viti maalumu cha mbunge mwanamke endapo kimepata 5% ya kura zote halali za uchaguzi wa wabunge.

  Ili kutekeleza hilo hapo juu, Vyama vya Siasa vina wajibu wa:

  1. Kupendekeza majina ya wanawake kwa idadi itakayopendekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kulingana na Ibara ya 66(1b) na Ibara ya 78 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kwa mpangilio wa upendeleo (preference) na kuituma Tume siku 30 kabla ya Uchaguzi.
  2. Kuhakikisha kwamba wanaopendekezwa wanajaza Fomu za Uteuzi
  Dokezo: Kujaza Fomu za Uteuzi

  Wanawake watakaopendekezwa hawatakiwi kuweka dhamana ya shilingi Elfu Hamsini (50,000/=).
  Viti Maalumu vya Madiwani Wanawake
  Viti maalumu kwa upande wa madiwani, vinapatikana kutoka kwa kila chama kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya viti ambavyo kila chama kimepata katika uchaguzi wa Madiwani katika Halmashauri ya Jiji, Manispaa, Mji na Wilaya.
  Viti hivyo ni theluthi moja ya jumla ya madiwani wa kuchaguliwa na wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi katika eneo husika.
  Ili kutekeleza hayo:

  1. Vyama vipendekeze majina ya wanawake ambao watakuwa ni theluthi moja ya jumla ya madiwani wote wanaowakilisha kata na wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi. Orodha ya majina hayo ipelekwe siku 30 kabla ya siku ya upigaji kura.
  2. Vyama vya Siasa vihakikishe kwamba vinapendekeza wanawake wenye sifa za kuwa Madiwani
  3. Wanawake wa viti maalumu vya Madiwani wanaopendekezwa na vyama vya Siasa wanajaza Fomu za Uteuzi
  4. Wanawake hawatakiwi kuweka dhamana ya Shilingi Elfu tano (5,000/=).
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mwaka huu inahitajika kazi ya ziada ya kujitoa mhanga kupambana na makundi hayo hapo juu
   
 13. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Na iwe hivyo
   
 14. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2010
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,963
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 180
  Wanaoruhusiwa kuwepo katika kituo cha kujumlishia kura kwa Uchaguzi wa Rais na Wabunge ni

  1. Msimamizi wa Uchaguzi = CCM
  2. Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi = CCM
  3. Mratibu wa Uchaguzi wa Mkoa = CCM
  4. Mjumbe wa Tume = CCM
  5. Mkurugenzi wa Uchaguzi = CCM
  6. Afisa wa Tume = CCM
  7. Mgombea au Wakala wake = (Hongo+wakala=CCM)
  8. Askari wa Polisi au Mlinzi wa Kituo = CCM
  9. Mtazamaji wa Uchaguzi aliyeidhinishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa maandishi =CCM

  Karibu wote ni waajiriwa wa serikali ya chama cha mapinduzi. Chadema ni lazima ijipange vizuri kupambana na serikali kwenye uchaguzi huu.
   
Loading...