Foleni za Viongozi

Foleni za Viongozi

Mfikirishi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
10,403
Reaction score
12,095
Wakuu,
Nauliza hivi: Je, viongozi wetu, watendaji na wakuu wa hitifaki za viongozi wanajua kuwa wananchi nao wana mipango, mahitaji na malengo yao yanayotegemea na kubanwa na MUDA (WAKATI)?? Je, wanajua kwamba misafara ya viongozi inawatia wananchi hasara?

Iweje wananchi wanasimamishwa kwenye foleni kwa zaidi ya masaa kisa eti kusafisha njia msafara wa magari ya kiongozi mmoja... kiongozi mmoja upite!

Hivi hakuna namna nzuri wanaweza kuwasafirisha hao viongozi zaidi ya hizi road-show-offs zinazotatiza shughuli mbalimbali za kijamii?

Dar, Arusha, Mwanza, Mbeya... Ni miji inayoongoza kwa hizi kero za foleni za viongozi!
Pale Dodoma washazoea utasikia hiyo ni foleni ya Waziri Mkuu...

Gharama za hizo road-shows zinakuwa kubwa hasa kwa wale wenye safari za kuunga na vikao/mikutano. Mfano...Zaidi ya mara moja nishajikuta nacheleweshwa flight na kulazimika kulipia mara mbili!
Hapo fikiria kuhusu wagonjwa, wafanyabiashara, wageni watalii n.k wenye miadi mbalimbali isiyotambua dharura za kihitifaki!

Kinachoudhi ni kwamba barabara inasafishwa pande zote one to two hours before ukute hata kiongozi husika hajamalizia vikao vya ndani!

Ni kwamba matumizi ya akili ndo yamefikia mwisho katika kuratibu safari za viongozi? Au mnahitaji D ngapi kubaini kuwa tunawasababishia wananchi hasara?

Najiweka mbali kuzungumzia idadi ya magari kwenye misafara make kina jingalao hawachelewi kusema tuna wivu.

View attachment 3089934View attachment 3089935
 
Unaijua gharama ya kupoteza kiongozi wa nchi?
Unafahamu thamani ya kiongozi wa nchi?
Unajua muda unaotumika kmpika au kumtengeneza kiongozi wa nchi?
unajua hasara kiasi gani kiongozi wa nchi akidhurika?

Kamwe usifananishe ulinzi wa kiongozi wa nchi na upuuzi wa kuwahi sehemu.

by the way ni scenario ipi inakufanya utake kuwahi kuliko msafara wa kiongozi??
 
Kwani hakuna njia mbadala ya kuwasafirisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine?
Hakuna helicopter kwa mfano?
Na kwanini wasipange hizo safari zao muda ambao hawatakwamisha shughuli za wengine?
 
Kwani hakuna njia mbadala wa kuwasafirisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine?
Hakuna helicopter kwa mfano?
Na kwanini wasipange hizo safari zao muda ambao hawatakwamisha shughuli za wengine?
Ni shughuli gani hukwama wakati wa msafara au mmezoea nongwa tu
 
Kwani ikitolewa taarifa kwamba kuna motorcade itapita barabara fulani kwa muda fulani kuna tatizo gani?? Watumiaji wengine wa barabara husika wakapewa njia mbadala au kama barabara husika ni moja basi watumiaji wengine walazimike kuwahi/kuchelewa zaidi ya muda wao.
 
Unaijua gharama ya kupoteza kiongozi wa nchi?
Unafahamu thamani ya kiongozi wa nchi?
Unajua muda unaotumika kmpika au kumtengeneza kiongozi wa nchi?
unajua hasara kiasi gani kiongozi wa nchi akidhurika?

Kamwe usifananishe ulinzi wa kiongozi wa nchi na upuuzi wa kuwahi sehemu.

by the way ni scenario ipi inakufanya utake kuwahi kuliko msafara wa kiongozi??
Kumbe mwanchi kuwahi sehemu ni upuuzi?
 
Kwa hiyo wewe ukiwa umelala ndani unaposti uchawa unafikiri huko barabarani hakuna shughuli za watu?
Shughuli gani?Be specific.
Dunia ya leo unaweza kufanya mengi ukiwa kitandani.
 
Mkuu some tunategemeana. Kila mmoja anapaswa kuheshimu nafasi na muda wa mwezake. Bila Viongozi wananchi/raia hatutaona njia vivyo hivyo bila wananchi/raia Viongozi hawatakuwa na wakuwaonyesha njia.
 
Ni shughuli gani hukwama wakati wa msafara au mmezoea nongwa tu
Kuna siku natoka Dodoma kwenda Dar naibu waziri mkuu anatoka Morogoro..tuliwekwa pembeni zAidi ya masaa 2 .. ni kero ! Nchi za wenzetu hakuna hizo mambo
 
Imekutokea mara ngapi kwa mwaka?
ni mara ngapi Dodoma to Dar kunatokea foleni kwa sababu ya ajali?
By the way sasa hivi tuna S.G.R hivyo hiyo kero imefutika
 
Unaijua gharama ya kupoteza kiongozi wa nchi?
Unafahamu thamani ya kiongozi wa nchi?
Unajua muda unaotumika kmpika au kumtengeneza kiongozi wa nchi?
unajua hasara kiasi gani kiongozi wa nchi akidhurika?

Kamwe usifananishe ulinzi wa kiongozi wa nchi na upuuzi wa kuwahi sehemu.

by the way ni scenario ipi inakufanya utake kuwahi kuliko msafara wa kiongozi??
Kiongozi Hadi anadhurika ujue hatimizi majukumu yake.kwa maana ni jizi na fisadi ambayo hupelekea kuwa na maadui lakini kama anatimiza majukumu yake vizuri hakuna atakaye hangaika kumdhuru.Unasema gharama ya kumpika kiongozi!viongozi wetu wanapatikana Kwa njia za wizi wa kura Sasa hapo unapikwa vipi kuwa kiongozi wa haki kama tu kupatikana kupatikana Kwa wizi?
 
Back
Top Bottom