Upo sahihi kabisa, japo mimi nafikiri kuwe na zonal bus stands, kila zone iwe na stand kubwa yenye standards za ile ya Magufuli. Tegeta/Bunju kuwe na stand kubwa yenye viwango, Temeke/Mbagala kuwe na stand ya viwango vikubwa. Hii inq maana kuwa kama kampuni ya mabasi ya Shabbiby(mfano) anaweza kuwa na mabasi yake kwenye stands zote, mtu anayeishi Mbagala/Temeke akitaka kwenda Dodoma asilazimike kufika Mbezi, safari yake inaanzia Mbagala hadi anakoenda, mtu anaishi Mbezi/Tegeta, hana sababu ya kufata bus huko Mbagala ili kwenda Mtwara, safari yake ianzie Tegeta na kwenda anakotaka.Tatizo ni Fikra za hovyo za kuwa na stand Moja ya MBEZI inayolazimisha mabasi zaidi ya mia nane kuanzia safari zao pale.
Mabasi zaidi ya mia nane yenye abiria 50 ni idadi kubwa sana ya watu kuanzia safari sehemu Moja. Ikiwa na maana Kuna watu zaidi ya 40,000 wanaotakiwa kufika eneo Moja la MBEZI kila siku Kwa ajili ya safari TU achilia mbalili wanaokwenda Kwa ajili ya shughuli za kibiashara n.k.
Hali hii inasababisha tatizo lililokuwa Ubungo liwe limehakishiwa MBEZI. Daladala karibu Jiji Zima zinakua na Ruti ya Kwenda MBEZI Kwa wakati mmoja na Kwa Lengo Moja.
Haya ni matumizi mabaya ya akili ya Wataalamu wetu wanaohusika na jamii na miundo mbinu yao.
Miundo Mbinu inapaswa kulenga Ustawi wa watu na mazingira mazuri ya jamii kuishi vizuri bila Karaha ya kukosa hewa na Joto kwenye daladala Kwa masaa zaidi ya matatu. Kuchelwa kufika makazini na kwenye Biashara.
Kukosa muda wa kuwahi kufika majumbani na kupumzisha akili na kutafakari vyema masuala ya kazini na ufanisi wa kazi. Ndio maana utendaji unakua uko chini sana Kwa sababu watu hawapati muda wa kufikiri sawasawa zaidi ya kufika nyumbani saa Tano za usiku na kuamka saa Tisa. Kutumia muda Mwingi kwenye Foleni na mafuta kutumika sana kwenye magari hivyo kuwafanya watu kutumia ujanja ujanja wa kupata pesa za ziada za Kununua mafuta. Daladala kutanua Barabara na kuharibu miundo mbinu na kuisababishaia serikali hasara ya kukarabati miundo mbinu Kwa muda mfupi.
Tatizo ni wajanja wachache walioko kwenye mamlaka ya miji na majiji . Ubinafsi wa kutafuta tenda za kusimamia Standi na makusanyo ya ushuru ndio unaowaumiza watanzania.
Kwa Nini kila Wilaya Isiwe na Stand yake na mabasi yakaanzie Huko Huko na kuendelea na safari zao badala ya kulazimisha kila basi kuanzia na kuishia Sehemu Moja. Pangekua na Stend Kinondoni ,Ubungo (MBEZI), Ilala, Temeke na Kigamboni . Daladala zigawanyike kupeleka watu kwenye stand hizo ili huduma kubwa ibaki kuwa ni ya kuwapeleka watu maofisini na kwenye baisahara zao sio kuwapeleka watu standi Kwa ajili ya safari.
Tunamshukuru Mama Dr. Samia Suluhu Kwa kuimarisha Democrasia. Tunaomba aendelee kuimarisha na mfumo mzima wa Uchaguzi na Katiba ili tupate viongozi wenye uwezo na wazalendo halisi . Uchaguzi uwe huru na haki tuwapate viongozi makini sio Hawa wa kuwaza tenda za Jiji ndio maana chaguzi za madiwani na mameya zinageuka kuwa vita kubwa. Sio Kwa ajili ya kutatua Kero za wananchi Bali kupata tenda kwenye miradi na usimamizi wa ushuru.
Watanzania tufanye maamuzi sahihi wakati wa Uchaguzi . Tusiangalie Rangi za mashati na vyama Bali uwezo na hoja na maono ya mtu. Vyama vimetuangusha sana na vimekua ni kichaka Cha wezi kupitia na kujitajirisha kupitia fedha za umma huku wananchi wakiteseka .
Sasa hivi pameboreshwa hakuna jam wameweka njia za juu kwa wanaokatiza morogoro roadSema Ile stend ya magufuli ibomolewe ndoinaleta jam
Pale pana shida bado kuna siku foleni ya malori inafika uwanja wa taifaHii ya Tazara ndio sijawaelewa mana TAZARA ilibd pawe na kitu kama Ubungo sasa sijui ilikuaje wakaeka upuz pale
Ni kweli,hapo ingepigwa ile highway aliokua anaiongelea magu ya kutoka chalambe hadi chalinze..sasa cjuì kama bado mpango ule upoMtoa mada mbona umesahau barabara yetu ya mbagala rangi 3 Hadi mmbande? Hii barabara inahitaji maboresho makubwa ya utanuzi pia baada miezi kadhaa mbele mwendokasi itaanza najua Ile foleni ya kariakoo - mbagala utahamia huku kwetu
Unaongelea ya kuanzia korogwe?Wameindoa foleni ubungo wameipeleka kimara mwisho.
Wameitoa mbezi wameipeleka kimara mwisho.
Pale kimara mwisho panahitaji suluhisho la foleni iwe ni daraja au upanuzi wa barabara
Iwe kubwa kuliko zote DarMwenge,Morocco pawekwe flyovers,pia buguruni chama/shell patafutiwe suluhishi japo pawekwe round about.
Umenena vyemaTatizo ni Fikra za hovyo za kuwa na stand Moja ya MBEZI inayolazimisha mabasi zaidi ya mia nane kuanzia safari zao pale.
Mabasi zaidi ya mia nane yenye abiria 50 ni idadi kubwa sana ya watu kuanzia safari sehemu Moja. Ikiwa na maana Kuna watu zaidi ya 40,000 wanaotakiwa kufika eneo Moja la MBEZI kila siku Kwa ajili ya safari TU achilia mbalili wanaokwenda Kwa ajili ya shughuli za kibiashara n.k.
Hali hii inasababisha tatizo lililokuwa Ubungo liwe limehakishiwa MBEZI. Daladala karibu Jiji Zima zinakua na Ruti ya Kwenda MBEZI Kwa wakati mmoja na Kwa Lengo Moja.
Haya ni matumizi mabaya ya akili ya Wataalamu wetu wanaohusika na jamii na miundo mbinu yao.
Miundo Mbinu inapaswa kulenga Ustawi wa watu na mazingira mazuri ya jamii kuishi vizuri bila Karaha ya kukosa hewa na Joto kwenye daladala Kwa masaa zaidi ya matatu. Kuchelwa kufika makazini na kwenye Biashara.
Kukosa muda wa kuwahi kufika majumbani na kupumzisha akili na kutafakari vyema masuala ya kazini na ufanisi wa kazi. Ndio maana utendaji unakua uko chini sana Kwa sababu watu hawapati muda wa kufikiri sawasawa zaidi ya kufika nyumbani saa Tano za usiku na kuamka saa Tisa. Kutumia muda Mwingi kwenye Foleni na mafuta kutumika sana kwenye magari hivyo kuwafanya watu kutumia ujanja ujanja wa kupata pesa za ziada za Kununua mafuta. Daladala kutanua Barabara na kuharibu miundo mbinu na kuisababishaia serikali hasara ya kukarabati miundo mbinu Kwa muda mfupi.
Tatizo ni wajanja wachache walioko kwenye mamlaka ya miji na majiji . Ubinafsi wa kutafuta tenda za kusimamia Standi na makusanyo ya ushuru ndio unaowaumiza watanzania.
Kwa Nini kila Wilaya Isiwe na Stand yake na mabasi yakaanzie Huko Huko na kuendelea na safari zao badala ya kulazimisha kila basi kuanzia na kuishia Sehemu Moja. Pangekua na Stend Kinondoni ,Ubungo (MBEZI), Ilala, Temeke na Kigamboni . Daladala zigawanyike kupeleka watu kwenye stand hizo ili huduma kubwa ibaki kuwa ni ya kuwapeleka watu maofisini na kwenye baisahara zao sio kuwapeleka watu standi Kwa ajili ya safari.
Tunamshukuru Mama Dr. Samia Suluhu Kwa kuimarisha Democrasia. Tunaomba aendelee kuimarisha na mfumo mzima wa Uchaguzi na Katiba ili tupate viongozi wenye uwezo na wazalendo halisi . Uchaguzi uwe huru na haki tuwapate viongozi makini sio Hawa wa kuwaza tenda za Jiji ndio maana chaguzi za madiwani na mameya zinageuka kuwa vita kubwa. Sio Kwa ajili ya kutatua Kero za wananchi Bali kupata tenda kwenye miradi na usimamizi wa ushuru.
Watanzania tufanye maamuzi sahihi wakati wa Uchaguzi . Tusiangalie Rangi za mashati na vyama Bali uwezo na hoja na maono ya mtu. Vyama vimetuangusha sana na vimekua ni kichaka Cha wezi kupitia na kujitajirisha kupitia fedha za umma huku wananchi wakiteseka .
Hawa Bajaji wanamatumizi mabaya ya barabara, Kwa mfano ukitokea kibaha, baadhi ya vituo ambavyo viko upande wa kushoto, na kuna mataa, bajaji hupaki barabarani kungojea abiria, ila wanatizamwa tu.Kingine ni matumizi mabovu ya barabara, mfano kutoka Mbezi kwenda Magomeni, bajaj zipo nyingi sana na hazihitajiki kupita hiyo njia kuu zenyewe zinatakiwa kutumika katika njia za ndani ndani, bajaj zinajaza foleni kwa baadhi ya maeneo zikishindana na daladala hata kusimama mahali ambapo si kituo cha daladala/kupakia abiria.
Matumizi ya barabara ni mabovu, bajaj hazitakiwi hii njia kuu, zimejaa nyingi sana, sasa chukulia miaka 5 na zaidi mbele wakiacha hivihivi njia itakuwa na kiwango kikubwa cha karaha!!
Aaaaaaaaaaaaaaah wapii unawaza tumboNichagueni mimi hayo yote ntayatatua wiki tu.
Kwahiyo foleni inawakera wenye vyombo vya usafiri tu, sababu dalsdala linapaa eti.Mleta mada huna hata baiskeli,sasa hiyo foleni inakupa shida ya nini??
Kuna ya Magomeni kwenda Jitegemee Sec kurasini. Kuna ya Mbagala mpaka Kariakoo au Stesheni. Kuna ya VETA kuelekea Tazara, etcKama hii ya kisutu kwenda kurasini haloo[emoji848]
Mpaka sasa bado unapanda daladala??Kwahiyo foleni inawakera wenye vyombo vya usafiri tu, sababu dalsdala linapaa eti.
Haya ndo matumizi mabovu ya barabara, bajai hazitakiwi njia kuu zile zilitakiwa kutumiwa na daladala na mwendokasi tu, njia kuu lazima iheshimike na matumizibyake kazima izingatiwe.Hawa Bajaji wanamatumizi mabaya ya barabara, Kwa mfano ukitokea kibaha, baadhi ya vituo ambavyo viko upande wa kushoto, na kuna mataa, bajaji hupaki barabarani kungojea abiria, ila wanatizamwa tu.
Ukianzia pale kwa Msuguri, pakingia yao ni kwenye mistari ya Zebra pale.
Wameua njia moja eneo lile.
Pale tembonij ndiyo balaa, wanaanzia kabla kuvuka taa, hata daladala hazipakii ndani ya kituo, hapa wanaua njia mbili wanabakiza njia moja tu, ila eneo la paki hubaki wazi kabisa.
Hahala pengine ni pale Suka na Korogwe, kituo cha mwendo kasi bajaji hutega zebra ya mwisho wa kituo, na huzima kabisa engine.
Uhamisho Dodoma na mikoa mingine utiliwe mkazoJapan wamekuja na mpango wa kugawa fedha ili watu waondoke Tokyo na kwenda kuendeleza miji mingine ili kupunguza msongamano,Population ya Tokyo ni milioni 37+
Traffic jam ni janga la miji yote mikubwa Duniani,Mji kama Dar ni vizuri kuimprove public transport hasa Treni ili kupunguza msongamano wa magari na kuimprove Air quality.
Hizo bajaj zinatafutiwa dawa yake, wao na pikipiki.Kingine ni matumizi mabovu ya barabara, mfano kutoka Mbezi kwenda Magomeni, bajaj zipo nyingi sana na hazihitajiki kupita hiyo njia kuu zenyewe zinatakiwa kutumika katika njia za ndani ndani, bajaj zinajaza foleni kwa baadhi ya maeneo zikishindana na daladala hata kusimama mahali ambapo si kituo cha daladala/kupakia abiria.
Matumizi ya barabara ni mabovu, bajaj hazitakiwi hii njia kuu, zimejaa nyingi sana, sasa chukulia miaka 5 na zaidi mbele wakiacha hivihivi njia itakuwa na kiwango kikubwa cha karaha!!
Hivi jpm kajenga miundombinu gani wazee Hadi asifiwe hivyo!?Hizi harakati za ujenzi wa miundo mbinu aliziweza Jpm..sa100 yeye ni mtaalamu wa 4R.
Ukosefu wa ajira rasmi unafanya miji yetu kutokupangika. Ngumu sana kupanga jiji lililojaa umasikini na ufukara.Hizo bajaj zinatafutiwa dawa yake, wao na pikipiki.